NMB ni vyema mkaja huku kujibu maswali na dukuduku za wateja, vinginevyo uzi huu hauna sababu ya kuwepo!
Sent using
Jamii Forums mobile app
...
hawa NMB sio kabisa. Kaka yangu mstaafu na ana matatizo ya kisukari, alikwenda pale tawi la Bank House meska jana kati ya mwezi wa saba na wa kumi na akamueleza mama aliyekuwa kwenye ofisi pale counter kwamba yeye alikuwa ni mstaafu anayesubiri pensheni yake na kitambulisho pekee alichokuwa nacho ni cha Ustaafu cha kampuni moja kubwa ya mawasiliano ya nchini.
akamueleza ukweli kwamba yeye hajapata kumiliki cheti cha mpiga kura hata siku moja na alikuwa akisubiri taratibu za kupatiwa kitambulisho cha taifa na aliisha jaza form zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Alichokuwa nacho kingine ni barua tu ya utsmbulisho kutoka serikali ya Mtaa.
Akamuomba mama yule amsaidie kufungua account ili pensheni yake iwe inapitia humo wakati akiendelra kusubiri kitambulisho chake cha taifa.
Bahati nzuri mama yule akawa mwelewa na kumuelekeza brother afungue account ya NMB KWIK.
Akafanikiwa kufungua account hiyo na mwezi December pensheni yake ikaanza kuingia na angalau krismas yake ikawa njema huku akiweza angalau kuwa na uhakika wa matibabu ya kisukari chake.
Mwana wa mbuzi kamba ni yake.
Mwezi uliofuata tu NMB wakaifunga account ya brothet na kumtaka awasilishe vitambulisho vyake ili account yake iweze kufunguliwa.
Kska akatoka huko aliko na kufika pale NMB House kuomba kufinguliwa account yake ili aweze kupata hicho kidogo cha kumsaidia matibabu yake.
Bahati mbaya sana kwake hakumkuta yule mama aliyekuwa amemsaidia kumfungulia acvount.
Aliyekuwepo hakutaka hata kusikiliza maelezo ya brother. Alichokuwa anataka ni kitambulisho cha mpiga kura, ama cha taifa, ama leseni, ama passport, basi. Barua ya utambulisho ya Serikali za Mitaa mamas hskutaka hata kuiangalia!
Ngoma imelala. Huu ni mwezi wa Tatu Pensheni inaingia kwenye acvount ya brother lakini hawezi kuichukua maana NMB walioahidi kumsaidia wameipiga Pini.
Sina haja ya kueleza kuwa miezi mitatu hii kisukari cha brother kinamsumbua maradufu.
Brother anasononeka kwamba kwa pensheni zao zimekuwa na mikutano mingi na kila mtu sasa amekuwa ni mtemi wa pensheni za wastaafu.
Sent using
Jamii Forums mobile app