NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mimi nataka nifungue Account ya Bank NMB, ila nataka nijue kwanza makato ya kila mwezi na makato ya kutoa pesa kwenye ATM. Nitashukuru kwa majibu yenu mazuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niwapongeze kwa huduma nzuri kwa wananchi. Mara nyingine tunaotumia NMB mobile services huwa tunapata ujumbe kuwa huduma hii kwa sasa haipatikani au muamala haujakamilika.

Cha ajabu unakuta fedha zimehamishwa kutoka akaunti ya mteja Ila hazijafika kule zilikotumwa,!
Wakati mwingine unakuta huduma haijakamilika lakini mteja amekatwa gharama kama vile amepata huduma aliyoikusudia.

Naomba wahusika mliangalie hili.
Hongera kwa kazi nzuri



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi nzuri yenyewe ndio hiyo uliyo ilalamikia? Huna tofauti na yule ambaye maelezo yake yote anaiponda bajeti inayowasilishwa, halafu mwisho wa maelezo anasema Naiunga mkono 100 kwa 100

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hello nilitaka kuuliza kiwango maximum cha pesa ambacho nnaweza kudraw kutoka katika account yangu kwa mara moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmebweteka sana ninyi hasa kwenye mikopo kwa wafanyakazi ktk taasisi zao, hebu jifunzeni kwa Crdb!

Crdb Wanafukunyua wateja na kuingia mikataba ya mikopo kwa kila aina ya wafanyakazi, wa muda, mikataba, na kudumu! Sijui shida ni hela za kuwakopesha hamna au ni uzembe na upoyoyo wenu...nyambafu!
 
mikopo bado riba kubwa kwa sisi watumishi vp kuna mipango yeyote ya kupunguza riba ili tukope tujikomboe kimaisha na uchumi wa nchi ukue
 
Naomba maelekezo jinsi ya kubadili namba ya simu ya kwenye account kupitia ATM machine ikiwezekana kwa maelekezo yaambatane na picha maana nimejaribu mara kadhaa na sikufanikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmb ilikuwa Kati ya Benki zenye utendaji uliowapendeza wateja wengi lakini siku hizi inatiwa kasoro na baadhi ya wafanyakazi wasiozingatia maadili ya kazi yao!

Nimekuwa mteja wa nmb kwa zaidi ya miaka 25 na mshahara wangu umekuwa ukipita hapo kwa miaka yote hii.

Pia nilikuwa na mikopo ambayo niliilipa August mwaka jana. Cha ajabu Sasa ni kuwa kila nikiprocess mkopo wa mshahara wangu mashine zao zinanirudishia majibu kuwa nadaiwa na ama mshahara wangu haupiti nmb kitu ambacho sio kweli!

Nimwaandikia email za kutosha na hata nimefika kwa branch manager wa magomeni lakini amekuwa akiahidi tu kuwa nenda Kisha jaribu baada ya saa 24 utapata! Mtindo umekuwa ni hvi Hadi Sasa na nimekata tamaa.

Suluhu ya Jambo hili haijulikani kwangu kwani Kama nadaiwa mbona hawakati kwenye mshahara wangu unaopitia kwenu?

Au nmb inachagua na kubagua wateja wa kuwapa huduma hata Kama wanakidhi vigezo?

Niliahirisha suala la kuhamishia mshahara wangu kwenye Benki nyingine na bado natafakari Kama nipo sahihi au la!

Wahusika, mtakimbiza wateja kwa utendaji wenu huu kwani nikikopa nalipa ili nanyi muweza kusustain!
 
Huu ni mfano wa kuigwa. Taasisi zenye uongozi imara ziko hivi. Nakupendeni sana NMB. Nina akaunti kwenu (japo mimi si mwalimu) mwaka wa saba sasa. Na sijawahi kujuta.
Kwani umesikia nmb ni Benki ya walimu peke yao au una shida na walimu? Mbona Haina ubaguzi wa kada za utumishi? Acha kuwashwa na walimu na Kama unawapenda Sana kaolewe nao!
 
Nimekuwa nikitumia nmb mobile app ila tatizo hili hapa chini mpka sasa sijapata suluhisho.



Kama wahusika wapo humu au yeyote mwenye shida hiyo na anajua suluhisho tafadhali naomba kupata muongozo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari, mm naomba muongozo WA kufungua akaunt nmb ,nipo buguruni rozan dar ,lkn Kitambulisho cha uraiya bado kupata.naomba kama inawezekana nijibiwe mp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…