NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

markbusega

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2015
Posts
826
Reaction score
848
Niende moja kwa moja kwenye mada,

leo nimekwenda kuchukua fedha kwenye ATM zao na nikaomba risiti, kiwango kilichokatwa nikikubwa mno (sh 10,000). Hii gharama ya huduma ya kibenki ni kubwa mno, sikuamini macho yangu, ilibidi niangalie mara mbili kama ni sh 10,000 au 1,000.

Nawashauri NMB waangalie upya makato hayo. Labda kama hawa "encourage" huduma hiyo kutumiwa na wateja wengi.

Nilikuwa naomba kujua makato yakoje kwenye benki zingine kwa huduma kama hiyo wakuu.
 
10000/= serious?

Aisee kama niivo nimepigwa sna[emoji28][emoji28]

Yaani mimi lazima niombe risiti nikienda ATM!

Mkuu unaweza kukuta 1000 umeangalia vbya!
Ngoja na Mimi nilifanyie kazi
Hivi nani aliletaga huu uongo kwamba ukiomba risiti kuna gharama?

Gharama ni moja tu ya kutumia ATM basi unakatwa kila unapotumia na haizidi sh 2000 labda kama utumie huduma zile za MasterCard/Visa

Hii ya elfu kumi sijawahi kuisikia na siamini mpaka nitakapothibitishiwa
 
Mmmh vile naogopaga kutoa hela kwa hawa ma wakala bank na kukimbilia ATM kumbe napo ni tatzo

Usiamini kirahisi uzushi wa huyu jamaa, kwa wakala ndo makato makubwa ni kama kutolea pesa dirishani…. ATM haijawahi kufika huko.

Let alone tozo ya risiti.
 
Hiyo ni ada ya risiti au stetement, sijakuelewa vizuri, unaombaje risiti kwenye ATM wakati ukitoa hela risiti huwa inatoka automatic hela zikisha toka!
 
Back
Top Bottom