NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

Hivi nani aliletaga huu uongo kwamba ukiomba risiti kuna gharama???

Gharama ni moja tu ya kutumia ATM basi unakatwa kila unapotumia na haizidi sh 2000 labda kama utumie huduma zile za MasterCard/Visa

Hii ya elfu kumi sijawahi kuisikia na siamini mpaka nitakapothibitishiwa

Mkuu, hebu fafanua kidogo hapo…. mimi pia ni mmoja wa wanaoamini ukiomba risiti kuna some extra charges.
 
Hiyo ni ada ya risiti au stetement,sijakuelewa vizuri,unaombaje risiti kwenye ATM wakati ukitoa hela risiti huwa inatoka automatic hela zikisha toka...!
yap uko sahihi, huyu mdau ameleta chenga, risiti inatoka yenyewe na hakuna mahala pa kukataa risiti.
inatakiwa ajieleze vizuri sana au tuombe MODS wampige BAN ya nguvu kwa kusababsisha taharuki na sintonfahamu.

Mi nashauri asiponyoosha maelezo apigwe BAN ili iwe fundisho kwa wengine.
&&&&&&&&&&&&&&&&*&&&&&&&

Ok nilisahau ipo sehemu ya kukubali au kukataa risiti. Ila bado
10k atoe maelezo
 
Mkuu, hebu fafanua kidogo hapo…. mimi pia ni mmoja wa wanaoamini ukiomba risiti kuna some extra charges.
Ukiomba risiti kuna pesa unakatwa lakini ni ndogo sana tofauti na madai ya mleta mada! CRDB kwa mfano, wao wanakata Sh. 300/=.
 
Kwa mtu ulie mji mkubwa wenye bank nyingi..

Kutumia crdb na nmb ni ujinga.. maana wana makato ya ajabu mengi sana.. benki sahihi ni equity bank ama bank zingine za kigeni
Sasa Equity Bank utaikuta Kakonko? Nyie wa mijini ndio angalau mnapata hizo faida za kuwa na mabenki anwai.

Vv
 
Hivi gharama zipoje kwa
Anayetoa ndani kwa Bank teller?
Anayetoa kwenye ATM
anayetoa kwa wakala
Anayeivuta kwenye simu kutoka Bank
 
Mimi natumia Crdb bank wanachofanya hawa jamaa gharama z a bank wanaongeza double zero lakn hazina dhamani mfano ukiangalia salio weather umechukua risit au la 18000 hapo wana maanisha T sh 180.00, mimi ndo ninacho jua withdraw wanacharge 120000 ambayo ni sawa na Tsh 1200, sasa sijui kwa nini zile zero 2 hawatenganish
 
Mkuu, hebu fafanua kidogo hapo…. mimi pia ni mmoja wa wanaoamini ukiomba risiti kuna some extra charges.
Hakuna gharama ya risiti mkuu. Gharama ni ya kutumia ATM tu. Ukishaingiza kadi ukachora PIN yako hata ukitoa bila kufanya chochote unakatwa. Ila huduma zote unazofanya ndani ya huo mchomeko ziko covered hapo. Unless uwe unahamisha fedha au huduma zingine. Hakuna makato ya risiti kwa uzoefu wangu wa benki hizi Azania,Exim,Equity,NMB,CRDB

Labda niambiwe vinginevyo leo hii
 
Duh aise kwahyo wik iliyopita nimepigwa 30k kwenye risit tu? Daah sitarudia tena
 
Siamini!! Nadhani una matatizo ya macho! Vile vikaratasi, kama charge yake ni Sh.100, itaandikwa 100.00, sasa hiyo nukta inakuwaga ngumu sana kuiona!

Hiki ndo kinamtesa mleta mada, ila kwa maksudi kabisa anaendelea kukaza fuvu.

Itakuwa amekatwa 100.00 tu, ni uono hafifu tu japo kupitia mada yake kuna vitu vya kujifunza.
 
yap uko sahihi, huyu mdau ameleta chenga, risiti inatoka yenyewe na hakuna mahala pa kukataa risiti.
inatakiwa ajieleze vizuri sana au tuombe MODS wampige BAN ya nguvu kwa kusababsisha taharuki na sintonfahamu.

Mi nashauri asiponyoosha maelezo apigwe BAN ili iwe fundisho kwa wengine.
Acha ubish risit unaweza kuomba au kukataa na mashine zingine Kuna muda huwa hazina risit kabisa ukiomba wanakwambia ATM haina risit kote NMB Na CRDB
 
Back
Top Bottom