NMB wagoma kurudisha hati ya nyumba, japo deni lao limeshalipwa lote

Status
Not open for further replies.

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Juzi rafiki yangu alikuwa ananipa stori kuhusu mama yake. Alichukua mkopo NMB kama miaka 5 iliyopita, akaweka hati ya nyumba yake kama dhamana.

Uyo Mama kahangaika sana hadi akalipa deni lote, AJABU NMB SENGEREMA hawataki kumpa hati yake. Mbona kama nanusa mchezo mchafu? Inakuwaje benki kubwa hivi hawajahifadhi hati ya huyu mteja kwamba akimaliza mkopo wamrudishie mali yake?

Ziadi ya miaka 4 wanamzungusha mama wa watu amejaribu hata kutafuta watu anaojuana nao huko NMB ila nao hawasaidii kitu hebu anayeweza kufikisha taarifa, afikishe.

NMB tawi la SENGEREMA kuna mtu anataka kumpiga huyo Mama nyumba yake. Sio sawa

Pia soma
Naomba msaada wa wakili mzuri aliyepo Sengerema, Mwanza atakayeweza kusaidia hili suala la NMB kugoma kutoa hati ya mteja wao kwa miaka mitano

Yule mama amerejeshewa hati yake iliyokaa bank ya NMB kwa miaka 5
 
Awahusishe vyombo vya usalama polisi, waingilie kati
 
Jitahidi R&L mkuu
 

Aende takukuru, maana hapo wanaonekana wanatengeneza mazingira ambayo si sawa.
 
aende mahakamani, asije akawa time barred kufungua kesi, and the case will be based on breach of contract and therefore time limitation is six years. Mshauri aende mahakamani upesi
 
Wanatoa jibu gani kwamba hati ipo wapi ? Haya mambo inabidi yaende kimaandishi yeye awaandikie barua ya kuomba Hati yaki kimaandishi na wenyewe wamjibu kimaandishi ili shida ijulikane ipo wapi ili parekebishwe.... bila hivyo inaweza ikawa ni Hisia au hata Slander...., Au uzembe wa wafanyakazi jambo ambalo top management inaweza kurekebisha kwa haraka sana
 
Ungefuata taratibu ungewasiliana na bank husikia unaweza ukawa umekurupuka kuja mtandaoni kuleta lawama, ungemtafuta mkurugenzi mkuu kama unataka kusaidia
 

Si kuna utaratibu wa kurejesha hatii? Kama ilivyo kwa kupeleka hati ili kulinda mkopo?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…