Lah!
Mwambie huo mama achunge namba sana.
Kumbukumbu zake zote zinazohusiana na mkopo na ulipaji wa mkopo awe nazo karibu sana. hao Benki wasije kuibuka na kutaka kunadi nyumba.
Lakini kwa maelezo yako, hujasema lolote Benki wanasemaje kuhusu mkopo huo. Wanamwambia mama nini kuhusu kurudishiwa hati yake. Wewe umesema "anazungushwa tu", anazungushwa vipi, na nani kwenye hiyo Benki. Ni nani hasa anashughulikia swala lake moja kwa moja. Kisha fika kwa meneja wa tawi? Kaambiwa nini, tueleze nasi tujue kabla hujatushirikisha katika kuwalaumu Benki.