Acheni ujuaji wa kushauri vitu ambavyo hamvijui. TAKUKURU akafanye nini?
The best solution ni kumuona Wakili ambaye atamuandikia demand notice and an intention to sue au Kwa Kiswahili inaitwa HATI YA MADAI NA KUSUDIO LA KUSHTAKI.
WAKILI aipe Benki siku kadhaa (30 zinatosha) kuhakikisha kwamba wame-release Hati ya nyumba ya mteja wake, aombe na fidia ya usumbufu na gharama za huduma ya Wakili (Mimi hapo ningeomba 10 million) ili waki-bargain watoe hata 7 million.
Niliwahi kuwa na scenario kama hii Dodoma, Benki ilikuwa CRDB, niliwachapa demand notice ya siku 21 nikaomba na fidia ya million 7, ilivofika siku ya 9 Meneja wa Tawi akanipigia simu niende ofisini kwake nikiwa na mteja wangu. Kufika akaanza kuwa mpole, ooh unajua wateja wakikopa Huwa hati tunazipeleka Makao makuu ya benki Dsm
Baadaye wakabembeleza wakatoa mil 3 na kuahidi kui-release hati baada ya siku 3, tukasepa zetu na mteja wangu na kibunda chetu, baada ya siku 3 akarudishiwa hati yake.
Hao sio wa kuwachekea.