NMB wagoma kurudisha hati ya nyumba, japo deni lao limeshalipwa lote

Status
Not open for further replies.
Juzi rafiki yangu alikuwa ananipa stori kuhusu mama yake. Alichukua mkopo NMB kama miaka 5 iliyopita, akaweka hati ya nyumba yake kama dhamana.

Uyo Mama kahangaika sana hadi akalipa deni lote, AJABU NMB SENGEREMA hawataki kumpa hati yake. Mbona kama nanusa mchezo mchafu? Inakuwaje benki kubwa hivi hawajahifadhi hati ya huyu mteja kwamba akimaliza mkopo wamrudishie mali yake?

Ziadi ya miaka 4 wanamzungusha mama wa watu amejaribu hata kutafuta watu anaojuana nao huko NMB ila nao hawasaidii kitu hebu anayeweza kufikisha taarifa, afikishe.

NMB tawi la SENGEREMA kuna mtu anataka kumpiga huyo Mama nyumba yake. Sio sawa

Pia soma
Naomba msaada wa wakili mzuri aliyepo Sengerema, Mwanza atakayeweza kusaidia hili suala la NMB kugoma kutoa hati ya mteja wao kwa miaka mitano
Msaada ukipatikana, toa mrejesho
 
aende mahakamani, asije akawa time barred kufungua kesi, and the case will be based on breach of contract and therefore time limitation is six years. Mshauri aende mahakamani upesi
Ushauri mzuri, lakini naona 'Nyabukika' nadhani anayake mengine
Wanaleta utani na mali za watu. Nipigie simu kwenye Namba hihi 0742231570 nikawasha fire watatoa TU!
Watu wametoa hadi namba za simu hapa! Huyo mama hatoi hela yoyote kwa wakili, hadi hapo shauri litakapo amriwa, kama Benki wataweka ngumu na kutaka kwenda mahakamani.
Kutokana na yaliyoelezwa na mleta mada, kama hakuna mengine nyuma ya pazia, huyo mama hana sababu hata kidogo ya kuogopa kuwashtaki Benki.

Lakini inawezekana 'Nyabukika' anayo mambo mengine katika mada hii.
 
Umesikiliza upande wa rafiki yako

Vipi umewasikiliza NMB wanasemaje?
Lakini, miaka mitano; kungekuwa na shauri upande wa Benki, hiyo nyumba ingekuwa tayari imepigwa mnada.
Hawawezi kusubiri miaka mitano bila huyo mama kulipa chochote, kama kuna chochote alicho daiwa.
 
Wewe ndo mjuaji sasa, Hakuna wakili anakupa demand notice ya siku 21, kisheria ni siku 90. Na Takukuru anaenda kudai kwamba anatengenezewa mazingira ya rushwa kabla hajachukua hatua zaidi. Kama mkopo kamaliza, kwanini wanamcheleweshea hati yake..?
Unaleta personal feelings kwenye kazi ambazo tunazifanya kila siku na watu wanasaidika. Hii njia ya wakili kuna gharama ndo maana tunamshauri apite PCCB kwanza then baada ya hapo kuna hatua za kufuata kama kuiandikia BOT au kwenda moja kwa moja mahakamani. Hii ya kupitia BOT ina pro na cons zake ambazo sina tu muda wa kuanza kukuelezea hapa.
SAWA.''Personal feelings" haziepukiki, labda uwe 'robot'. Wewe mwenyewe hapa unazionyesha hisia zako tayari!
Lakini hii yako pia (TAKUKURU) unajuwa kuna urasimu vilevile, na fursa ya kupigwa zaidi. Mama hana anachojuwa. Takukuru wenyewe nao wataanza kutafuta fursa iliyowaijia kupiga pesa.
Unasema aende Takukuru; lakini hadi hapo haijaelezwa kama huyo mama ameombwa na maofisa wa BENKI KUTOA CHOCHOTE. Sasa kwa nini aende Takukuru? Kwa dhana tu kwamba kuna mazingira yanatengenezwa?

Ya wakili, huyo uliyemjibu, labda ni hiyo siku 21, uliyomsahihisha, lakini inaonekana ni njia sahihi kabisa kwa huyo mama.
Malipo ya wakili yatatokana na madai yatakayodaiwa kufidia usumbufu kwa huyo mama.
 
NMB wenyewe wanasemaje?
Kwa mjibu wa mleta mada ni kuwa Mama kila akienda benki anaambiwa arudi nyumbani watampigia simu.
Ni vigumu sana kuamini hili; miaka mitano yote mtu unaahidiwa kupigiwa simu; halafu wewe huchoki unaendelea tu na safari za kwenda Benki kupata jibu lile lile?
Hii mada imeanza kuonekana kuwa ni ya kibabaishaji.
 
SAWA.
Lakini hii yako pia (TAKUKURU) unajuwa kuna urasimu vilevile, na fursa ya kupigwa zaidi. Mama hana anachojuwa. Takukuru wenyewe nao wataanza kutafuta fursa iliyowaijia kupiga pesa.
Unasema aende Takukuru; lakini hadi hapo haijaelezwa kama huyo mama ameombwa na maofisa wa BENKI KUTOA CHOCHOTE. Sasa kwa nini aende Takukuru? Kwa dhana tu kwamba kuna mazingira yanatengenezwa?

Ya wakili, huyo uliyemjibu, labda ni hiyo siku 21, uliyomsahihisha, lakini inaonekana ni njia sahihi kabisa kwa huyo mama.
Malipo ya wakili yatatokana na madai yatakayodaiwa kufidia usumbufu kwa huyo mama.
Mlengo wa criminality ni hoja tosha kufungua jalada. Takukuru hawana shida (urasimu), punguza kuskiliza maoni ya vijiweni. Najaribu kumpa njia fupi sababu case za breach of contract mahakamani zina time limitation ambayo ni 6 years, hapo tayari kashafikisha 5 years hapewi hati yake. Ukiangalia vizuri kwa macho makali utaona nini kinatafutwa na hao ma afisa wa benki, washaona mama hana anachokijua kuhusu sheria.
 
Ushawahi ku deal na wakili kwenye case..? Au ni presumptions unafanya..?
 
Wewe ndo mjuaji sasa, Hakuna wakili anakupa demand notice ya siku 21, kisheria ni siku 90. Na Takukuru anaenda kudai kwamba anatengenezewa mazingira ya rushwa kabla hajachukua hatua zaidi. Kama mkopo kamaliza, kwanini wanamcheleweshea hati yake..?
Unaleta personal feelings kwenye kazi ambazo tunazifanya kila siku na watu wanasaidika. Hii njia ya wakili kuna gharama ndo maana tunamshauri apite PCCB kwanza then baada ya hapo kuna hatua za kufuata kama kuiandikia BOT au kwenda moja kwa moja mahakamani. Hii ya kupitia BOT ina pro na cons zake ambazo sina tu muda wa kuanza kukuelezea hapa.
Acha kuendelea ku-comment ili kuthibitisha kwamba wewe ni mjinga mkuu.

Demand notice ya siku 90 ni kama unataka kuishtaki Local au Central government. Siku 90 ni compulsory.

Demand notice kwenye MADAI mengine ya kawaida ni sisi Mawakili tunatumia busara kulingana na uzito wa MADAI yenyewe. Kama unamdai mtu billion Moja huwezi kumpa mdeni wako siku 21 kwasababu kiasi cha fedha ni kikubwa, so common sense ina-suggest umpe siku nyingi zaidi.

Hizi ni taaluma za watu acheni ujuaji na ukapuku, mnapotosha watu. Rubbish!!
 
Wewe huna akili, i am done with you. Ujuaji mwingi, maneno machafu na huna unachokijua.
 
Mlengo wa criminality ni hoja tosha kufungua jalada. Takukuru hawana shida (urasimu), punguza kuskiliza maoni ya vijiweni. Najaribu kumpa njia fupi sababu case za breach of contract mahakamani zina time limitation ambayo ni 6 years, hapo tayari kashafikisha 5 years hapewi hati yake. Ukiangalia vizuri kwa macho makali utaona nini kinatafutwa na hao ma afisa wa benki, washaona mama hana anachokijua kuhusu sheria.
Mbona wewe mtu ni 'judgemental' sana? Umejuaje nasikiliza mambo vijiweni.
Punguza joto la sivyo utaharibu mada hii.
Watu wamekwisha toa ushauri mzuri tu, halafu wewe ndiye unakuja na 'much know attitude'! Why?
 
Ushawahi ku deal na wakili kwenye case..? Au ni presumptions unafanya..?
hata kama ni 'presumption', kwani mawakili siku zote hawahusiki na maswala ya kesi?
Kwenye kesi kama hii sihitaji kuogopa kumwana wakili aisimamie kesi.
 
Wewe huna akili, i am done with you. Ujuaji mwingi, maneno machafu na huna unachokijua.
[emoji23][emoji23][emoji23]

Kaka mimi ni wakili, tena prominent, naandika ninachokijua.

Na ni mwandishi wa vitabu vya Sheria kwa LUGHA ya Kiswahili. Ndo mana nimechukia kuona ma-bush lawyer mnavamia taaluma za watu na kuanza kupotosha watu.

Nimekaa darasani Miaka 4 plus mmoja wa Law School, it's not a joke! Acheni ujuaji.

ID yangu ni AMICUS CURIAE, hii ni latin maxim yenye maana 'a friend of the court'.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom