Nyinyi mnaomfahamu huyo mama na munao uelewa wa kutosha, msaidieni.Ipo hivi huwa anaenda Bank kufuatilia hati lakini akifika anaambiwa "NENDA TUTAKUPUGIA SIMU" KWA MIAKA 5 SASA na ameshaonana hadi na meneja wa Benk akampa kijana wa kufatilia huyo kijana na yeye kamwambia siku fulani urudi utakuta tayari, hiyo siku imefika amerudi anaambiwa "MAMA WEWE NENDA TU NITAKUPIGIA SIMU NITAITAFUTA" kwa hiyo akiendelea kusubiri kupigiwa simu si itachuka miaka 10 aiseee
Kwanza kabisa, maneno ya mdomoni tu hayasaidii chochote. Inatakiwa pawepo na kitu, karatasi ya ushahidi kuwa hivyo alivyo ambiwa kwa miaka mitano ndivyo kweli.
Ni lazima aweke katika maandishi lawama zake zote tokea alipoanza kuzungushwa. Majina ya watu alioonana nao huko Benki anayo?
Ni lazima pawepo na ushahidi wa kimaandishi. Kama Benki hawajibu, hilo litakuwa tatizo lao, siyo lake.
Nyaraka za mkopo zipo, hakupewa mkopo kwa kutumia maneno ya mdomoni tu. Malipo kafanya, natumaini siyo kwa mdomo tu, bali stakabadhi zote anazo; na pengine hata barua ya Benki kuonyesha kwamba hadaiwi tena baada ya kulipa kila kitu, anayo.
Tahadhari: Asije kuwa analipa na pesa haiingizwi kwenye 'account' yake. Asije akashangaa mwisho wa siku anaambiwa mkopo bado haujalipwa.
Awahusishe na viongozi wa kijamii, kama hawezi kwa sasa kwenda mahalkamani.
Kwenda Benki na kupewa taarifa ya mdomo anapoteza tu muda wake.