NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

CRDB wana nyodo sana, hata ukitaka huduma mfano nilitaka kuandikiwa barua ya kupeleka kwa mwajiri wangu mpya. Barua ilikuwa inahusu mwenendo wa account yangu, walinitoza 59,000/= eti service fee wakati Mimi ni mteja wao miaka nenda rudi. Ninatabili CRDB itakimbiwa na wateja wengi.
 
Duuuh ndio maana NMB wanawaburuza kwenye faida
 
Halfu kuna baadhi ya ofisi za serikali wanakualazimisha kabisa mshahara wako lazima upitie crdb
 
CCM imewaharibu sana vijana wa kesho na kuwajaza akili za kusifia kichawa.

Badala ya mtu kuandika ni namna gani huyo mama kakuza bank ni kusifia tu, amna mention ya performance za financial products zinazofanya vizuri na kuongeza faida kuwazidi wengine.

Mwandishi mwanzo mwisho anasifia tu kwa kulinganisha assets na accessibility ya bank tofauti na wengine. But no mention of business contexts za msingi wa hayo mafanikio; halafu anajiita financial intelligence.

Bila ya kuitoa CCM nchi inapokwenda ni pabaya sana; jamaa wanatengeneza vijana wenye tabia za utegemezi wa watu wengine, kuamini kwenye fadhila ya mtu, kupata ni bahati na mambo mengine ya hovyo yanayohusishwa na poverty culture (sociologically), it’s just appalling.

Worst, haya mambo ya uchawa yanaanza kukubalika kama sehemu ya maisha ya kawaida.
 
Mkuu kumbuka kuwa na matawi kila mahali tafsiri yake hata gharama za uendeshaji ni kubwa lakini bado wameweza kutengeneza faida kubwa. Huyo mama anastahili pongezi zake.
 
tarakimu zako zimejaa ushabiki na uwongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…