NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

CRDB wana nyodo sana, hata ukitaka huduma mfano nilitaka kuandikiwa barua ya kupeleka kwa mwajiri wangu mpya. Barua ilikuwa inahusu mwenendo wa account yangu, walinitoza 59,000/= eti service fee wakati Mimi ni mteja wao miaka nenda rudi. Ninatabili CRDB itakimbiwa na wateja wengi.
 
CRDB wana nyodo sana, hata ukitaka huduma mfano nilitaka kuandikiwa barua ya kupeleka kwa mwajiri wangu mpya. Barua ilikuwa inahusu mwenendo wa account yangu, walinitoza 59,000/= eti service fee wakati Mimi ni mteja wao miaka nenda rudi. Ninatabili CRDB itakimbiwa na wateja wengi.
Duuuh ndio maana NMB wanawaburuza kwenye faida
 
Halfu kuna baadhi ya ofisi za serikali wanakualazimisha kabisa mshahara wako lazima upitie crdb
 
CCM imewaharibu sana vijana wa kesho na kuwajaza akili za kusifia kichawa.

Badala ya mtu kuandika ni namna gani huyo mama kakuza bank ni kusifia tu, amna mention ya performance za financial products zinazofanya vizuri na kuongeza faida kuwazidi wengine.

Mwandishi mwanzo mwisho anasifia tu kwa kulinganisha assets na accessibility ya bank tofauti na wengine. But no mention of business contexts za msingi wa hayo mafanikio; halafu anajiita financial intelligence.

Bila ya kuitoa CCM nchi inapokwenda ni pabaya sana; jamaa wanatengeneza vijana wenye tabia za utegemezi wa watu wengine, kuamini kwenye fadhila ya mtu, kupata ni bahati na mambo mengine ya hovyo yanayohusishwa na poverty culture (sociologically), it’s just appalling.

Worst, haya mambo ya uchawa yanaanza kukubalika kama sehemu ya maisha ya kawaida.
 
Hongera zao japo NMB pia inafaidika na mfumo...
  1. Fikiria mishahara ya watumishi wa umma karibia wote hupitia huko
  2. Mikopo ya watumishi hao ni kupitia huko
  3. Matawi karibia kila mahala ni suala tu la kuyasimamamia kimkakati nk
Ukiangalia vizuri kuna benk hapo nafikiri hazina hata miaka 15 zinashindanishwa na Benk yenye zaidi miaka ya 60
Mkuu kumbuka kuwa na matawi kila mahali tafsiri yake hata gharama za uendeshaji ni kubwa lakini bado wameweza kutengeneza faida kubwa. Huyo mama anastahili pongezi zake.
 
View attachment 2805767
MS Ruth Zaipuna Mkurugenzi Mkuu NMB.

======
Wasalaam Jf team,

Waswahili tunasema " Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake Mpeni "

Sote tunakumbuka baada ya NBC Bank kuvunjwa Mwaka 1997 na baadae kuanzishwa kwa Benki mpya ya Makabwera ya NMB na baadae Benki hiyo kubinafsishwa kwa Rabobank ya Uholanzi iliyomiliki hisa asilimia 49.

Wakati wote NMB PLC imekuwa ikiongozwa na watu kutoka nje ya nchi tu isipokuwa huyu Mkurugenzi wa Sasa Bi Ruth Zaipuna aliyekabidhiwa nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu rasmi mwaka 2020.

Kumbukumbu zinaonesha wakati mama huyu anaingia madarakani NMB bank ilikuwa na matawi yapatayo 100 tu nchi nzima na ATMs zipatazo 500 nchi nzima.

Leo NMB bank imefikisha matawi zaidi ya 200 na ATMs zaidi ya ATMs 1,000 nchi nzima hii ni sawa na kusema mama huyu ameikuza bank hii ya Makabwera kwa zaidi ya marambili, yaani ukuaji wa 100% au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema NMB bank PLC imefika katika Kila Jimbo la Uchaguzi la kiserikali haba bara.

Kutoka katika tovuti ya NMB taarifa zinaonesha NMB bank ilikuwa na wateja wasiozidi 600,000 miaka kumi iliyopita na wakati huu wa Ruth Zaipuna banki hii imefikia wateja zaidi ya 2.5M nchi nzima,karibu mara nne zaidi.

Kuhusu Uzalendo & Uzawa Kunajambo la kujifunza kwa hawa wanawake watatu yaani Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Spika wa bunge la JMT na IPU Mhe Dkt Tulia Hassan na Mkurugenzi Ruth Zaipuna kwa namna wanavyoleta mabadiliko ya kasi kwenye taasisi wanazoziongoza,

Hebu tazama orodha hii ya faida kwa mabenki kumi ya Tanzania yaliyofanya vizuri katika robo ya tatu tu ya mwaka huu wa 2023 ndio utaelewa vizuri nachosema kuhusu huyu Mkurugenzi.

1. NMB Bank: TZS 398 billion

2. CRDB Bank: TZS 280 billion

3. Stanbic Bank: TZS 95 billion

4. StanChart: TZS 64 billion

5. NBC Bank: TZS 62 billion

6. Citibank TZS 44 billion

7. PBZ TZS 41 billion

8. Exim Bank TZS 40 billion

9. Absa Bank TZS 37 billion

10. KCB Bank TZS 35 billion

Taarifa zinaonesha faida ya Jumla kwa mabenki yote Tanzania ni shilingi trilioni moja katika robo hii ya tatu, Hii ni sawa na kusema NMB PLC pekee anamiliki 40% ya faida yote huku ikimpiku kwa mbali mshindani wake wa karibu CRDB bank kwa zaidi ya TZS 118 BL sawa na 70% ya faida yake.

Wakati Ruth Zaipuna anakuwa Mkurugenzi Mkuu Benki hii ilikuwa na wastani wa faida ya TZS 200BL baada ya kodi wakati Leo faida imekuwa na kufikia wastani wa karibu TZS 400BL kwa mwaka yaani sawa na marambili zaidi.

Pia,taarifa zinaonesha Benki ya NMB inashika nafasi ya sita kwa Ukubwa katika nchi zote Kusini mwajangwa la Sahara na ndio Benki pekee toka Tanzania inayoshindana kimataifa,

Watanzania tunalakujivunia toka kwa Mkurugenzi huyu mzawa akisaidiwa na management nzima ya NMB PLC pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa NMB PLC chini ya Dkt Edwin Mhede, Hakika Mmestahili Heshima.

Kwa matokeo haya, Huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt Tulia mwingine ni huyu Ruth Zaipuna wa NMB PLC deserves better,
tarakimu zako zimejaa ushabiki na uwongo.
 
Back
Top Bottom