NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

Kuna kitabia cha wanaume fulani kazi yao nisifia wanawake na kukuza sifa sizostahiki hawa wanaitwa madume jike..wewe unayesifia umefanya nini...NMB wamewalazimisha wafanyakazi wa serikali miaka michache nyuma wachukue mishahara na mikopo kwao kupitia mbereko ya serikali,huo msingi ndio inafanya wawe na wateja wengi mpaka sasa especial waalimu..hususani waalimu.
Mtu yeyote akiwa mkurugenzi wa hiyo bank ataonekana anafanya vizuri..mishahaa hewa zinapoteleaga huko.
 
CRDB nini wamekukosea chief?
Nilikopa fedha kiasi kadhaa, ila kwenye salary slip yangu inaonekana nimekopa fedha nyingi sana kuliko tulivyoandikishana mkataba.

Nilimfata Manager tukaongea, akakiri kuna walifanya (Afisa Mikopo wao na Afisa Utumishi wangu). Wakaahidi kurekebisha. Hadi sasa hakuna walichokwishafanya.
 
Kuna kitabia cha wanaume fulani kazi yao nisifia wanawake na kukuza sifa sizostahiki hawa wanaitwa madume jike..wewe unayesifia umefanya nini...NMB wamewalazimisha wafanyakazi wa serikali miaka michache nyuma wachukue mishahara na mikopo kwao kupitia mbereko ya serikali,huo msingi ndio inafanya wawe na wateja wengi mpaka sasa especial waalimu..hususani waalimu.
Mtu yeyote akiwa mkurugenzi wa hiyo bank ataonekana anafanya vizuri..mishahaa hewa zinapoteleaga huko.
Hahaha povu la nini?

Umeona lakini kilichoandikwa hapa?


Sifa ziko wapi hapo zisizostahili kwa Ruth?


Tujifunze kukubali wanachofanya wengine
 
Nilikopa fedha kiasi kadhaa, ila kwenye salary slip yangu inaonekana nimekopa fedha nyingi sana kuliko tulivyoandikishana mkataba.

Nilimfata Manager tukaongea, akakiri kuna walifanya (Afisa Mikopo wao na Afisa Utumishi wangu). Wakaahidi kurekebisha. Hadi sasa hakuna walichokwishafanya.
Kabla hujaenda mahakamani wapelekee barua ya notice kwanza.
 
Nadhani ubunifu anaoweza kusifiwa nao ni kuanzisha mawakala wa benki. Sina hakika kama ni yeye alianzisha au aliikuta hiyo program. Zaidi ya hayo, haya mabenki mawili hayana lolote. Yanaletewa bashara za kutosha na serikali.
 
Please ukubwa in terms of what? Kama ni total assets CRDB ina Trillion 11.64 ila NMB ina Trillion 10.4!! Umetumia parameters zipi. Utusaidie kwa faida ya wote.

Kuna kitu kinaitwa efficiency, unaweza kuwa na asset kubwa zisikuwa na maana yeyote.

Kabla hata hatuja ingia kiundani kujua aina ya hizo asset ukijibu hapo juu inatosha kabisa kukupa picha.

Lakini pia tazama ile single lending limit kwa kuzingatia mtaji wa bank. Bila shaka nmb inaweza kuwa juu zaidi ya benk zote hizo.
 
Hongera zao japo NMB pia inafaidika na mfumo...
  1. Fikiria mishahara ya watumishi wa umma karibia wote hupitia huko
  2. Mikopo ya watumishi hao wakiwemo Waalimu hupitia kwao na ina riba kubwa tu
  3. Matawi karibia kila mahala ni suala tu la kuyasimamamia kimkakati nk
  4. Serikali hupitisha hela nyingi tu huko; Chukulia malipo ya watalii/TANAPA, nk
Ukiangalia vizuri kuna benk hapo nafikiri hazina hata miaka 15 zinashindanishwa na Benk yenye zaidi miaka ya 60
Benki nyinginezo zingefungua kesi kwenye tume ya ushindani. Kwa upande mwingine kulinda chako dhidi ya ushindani ni jambo zuri japo linadumaza akili.
 
CRDB wana nyodo sana, hata ukitaka huduma mfano nilitaka kuandikiwa barua ya kupeleka kwa mwajiri wangu mpya. Barua ilikuwa inahusu mwenendo wa account yangu, walinitoza 59,000/= eti service fee wakati Mimi ni mteja wao miaka nenda rudi. Ninatabili CRDB itakimbiwa na wateja wengi.
Chaga empire
 
Hata kama ni mimi ningepewa NMB ningetengeneza faida kubwa kuzidi huyu mama. Unajua ni kwa kiasi gani hiyo benki inafanya biashara na serikali? Unajua mishahara inayopita humo kutoka serikalini? Unajua ina akaunti ngapi za mapato ya serikali? Acha kabisa
 
View attachment 2805767
MS Ruth Zaipuna Mkurugenzi Mkuu NMB.

======
Wasalaam Jf team,

Waswahili tunasema " Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake Mpeni "

Sote tunakumbuka baada ya NBC Bank kuvunjwa Mwaka 1997 na baadae kuanzishwa kwa Benki mpya ya Makabwera ya NMB na baadae Benki hiyo kubinafsishwa kwa Rabobank ya Uholanzi iliyomiliki hisa asilimia 49.

Wakati wote NMB PLC imekuwa ikiongozwa na watu kutoka nje ya nchi tu isipokuwa huyu Mkurugenzi wa Sasa Bi Ruth Zaipuna aliyekabidhiwa nafasi hiyo ya Ukurugenzi Mkuu rasmi mwaka 2020.

Kumbukumbu zinaonesha wakati mama huyu anaingia madarakani NMB bank ilikuwa na matawi yapatayo 100 tu nchi nzima na ATMs zipatazo 500 nchi nzima.

Leo NMB bank imefikisha matawi zaidi ya 200 na ATMs zaidi ya ATMs 1,000 nchi nzima hii ni sawa na kusema mama huyu ameikuza bank hii ya Makabwera kwa zaidi ya marambili, yaani ukuaji wa 100% au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema NMB bank PLC imefika katika Kila Jimbo la Uchaguzi la kiserikali haba bara.

Kutoka katika tovuti ya NMB taarifa zinaonesha NMB bank ilikuwa na wateja wasiozidi 600,000 miaka kumi iliyopita na wakati huu wa Ruth Zaipuna banki hii imefikia wateja zaidi ya 2.5M nchi nzima,karibu mara nne zaidi.

Kuhusu Uzalendo & Uzawa Kunajambo la kujifunza kwa hawa wanawake watatu yaani Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Spika wa bunge la JMT na IPU Mhe Dkt Tulia Aksoni na Mkurugenzi Ruth Zaipuna kwa namna wanavyoleta mabadiliko ya kasi kwenye taasisi wanazoziongoza,

Hebu tazama orodha hii ya faida kwa mabenki kumi ya Tanzania yaliyofanya vizuri katika robo ya tatu tu ya mwaka huu wa 2023 ndio utaelewa vizuri nachosema kuhusu huyu Mkurugenzi.

1. NMB Bank: TZS 398 billion

2. CRDB Bank: TZS 280 billion

3. Stanbic Bank: TZS 95 billion

4. StanChart: TZS 64 billion

5. NBC Bank: TZS 62 billion

6. Citibank TZS 44 billion

7. PBZ TZS 41 billion

8. Exim Bank TZS 40 billion

9. Absa Bank TZS 37 billion

10. KCB Bank TZS 35 billion

Taarifa zinaonesha faida ya Jumla kwa mabenki yote Tanzania ni shilingi trilioni moja katika robo hii ya tatu, Hii ni sawa na kusema NMB PLC pekee anamiliki 40% ya faida yote huku ikimpiku kwa mbali mshindani wake wa karibu CRDB bank kwa zaidi ya TZS 118 BL sawa na 70% ya faida yake.

Wakati Ruth Zaipuna anakuwa Mkurugenzi Mkuu Benki hii ilikuwa na wastani wa faida ya TZS 200BL baada ya kodi wakati Leo faida imekuwa na kufikia wastani wa karibu TZS 400BL kwa mwaka yaani sawa na marambili zaidi.

Pia, taarifa zinaonesha Benki ya NMB inashika nafasi ya sita kwa Ukubwa katika nchi zote Kusini mwa jangwa la Sahara na ndio Benki pekee toka Tanzania inayoshindana kimataifa,

Watanzania tuna la kujivunia toka kwa Mkurugenzi huyu mzawa akisaidiwa na management nzima ya NMB PLC pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa NMB PLC chini ya Dkt Edwin Mhede, Hakika Mmestahili Heshima.

Kwa matokeo haya, Huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt Tulia mwingine ni huyu Ruth Zaipuna wa NMB PLC deserves better.
Mbona bandari yule gigy money anagawa anasema eti hatuwezi mpka waarabu watusaidie
 
Back
Top Bottom