NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

Ingekuwa analysis nzuri kama ungesema as compared to what? Maana banking industry yote ya Tanzania miamala ya ATM, mobile banking, branches zimekua zaidi ya mara mbili!! Yaani hata Maendeleo bank imekua zaidi ya Mara mbili ilihali ina assets ndogo zaidi.

Yes ilikuwa na assets nyingi miaka na miaka wala sio sababu ya

Analysis ya faida za kibenki hatupimi kwa billion hizi na hizi, maana obvious mtaji ukikua lazima faida ikue. So huwa wanapima kwa return on assets, au return on equity, sasa tukienda huko ndio ungetupa picha kamili kwamba kwa kila ongezeko la mtaji je kazalisha shingapi. ROA, ROE, au NIM.

Yeah apewe pongezi kwa kumaintain ukubwa wa NMB lakini kama mnamfanyia branding ili ateuliwe na Mama samia kwenye siasa mtampoteza. She might be good sababu ya ukubwa wa taasisi ila mkimpeleka sijui wizara ya uchumi, au sijui biashara na viwanda she'll be exposed of her weaknesses na atapoteza status yake.

Waacheni wabaki kwenye corporate world wana mchango mkubwa huko ila kwenye siasa atakua kama Kimei au Muhongo

CRDB Nmb
ROA 4.6%. 5%

ROE 25.4%. 28%

Basic EPS 38,5. 1,091

Loan to total asset
63%. 61%
 
Swali la Maana zaidi ni How did she Accomplish that ?!!!; Sababu kuna wakati watumishi ilikuwa ni lazima kuwa na Account NMB; au that was before her time ?

Tusiangalie faida tu, vipi kuhusu huduma, matawi n.k.
 
Kazi ya benki kuu ni kusimamia hizi benki za kibiashara kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wananchi ili waweze kupata maendeleo jibu lako kuwa kukopa siyo lazima ni kweli lakini ni jibu la kishenzi.

Kama unaelewa kuna benki kuu inasimamia ni vipi uone riba juu na kuzilaumu hizi benki bila kuiuliza benki kuu?
Riba kuwa juu inachangiwa na sababu nyingi sana, tuyaelewe haya mabenki lakin tuendelee kupiga mbiu yatoe nafuu.
Leo tunazungumzia riba hadi ya 9%, 10% , 13% kutoka 24% huko.

Nadhani tupiga hatua nzuri ya kupata nafuu za riba. Ingawa muda woote zinabadirika pia ama kuongezeka ama kupungua.

Mfano kwa riba za usd hazikamatiki, heri kuchukua Tzs.
 
Kuna vichwa pale NMB ni balaa ukiacha ZAIPUNA Kuna kichwa kinaitwa MPONZI Jamaa mmoja hivi ana upara ni hatari. Kuna DONATUS Richard mkuu wao wa biashara yaani wapo creative balaa I wish hivi vichwa vije vimsaidie mama kwenye uchumi pia vipewe uhuru wa kufanya kazi aiseee tutatoboa
Mtu hawezi kuteuliwa halafu akawa na uhuru wa kufanya kazi.
Rais mwenyewe hana uhuru huo.
 
Kuna kitabia cha wanaume fulani kazi yao nisifia wanawake na kukuza sifa sizostahiki hawa wanaitwa madume jike..wewe unayesifia umefanya nini...NMB wamewalazimisha wafanyakazi wa serikali miaka michache nyuma wachukue mishahara na mikopo kwao kupitia mbereko ya serikali,huo msingi ndio inafanya wawe na wateja wengi mpaka sasa especial waalimu..hususani waalimu.
Mtu yeyote akiwa mkurugenzi wa hiyo bank ataonekana anafanya vizuri..mishahaa hewa zinapoteleaga huko.
Hahahaha brother mbona kama povu jingi sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] akisifiwa Ruth kuna shida gani brother, mbona waliopita hawakufanya bidii hizi
 
Kuna kitu kinaitwa efficiency, unaweza kuwa na asset kubwa zisikuwa na maana
Mkuu kwenye scholarly paper zote duniani bank size mara nyingi inapimwa based on market share/penetration/concentration ama total assets. Kibongo bongo ikiwemo NMB operational efficiency inapimwa kwa kuchukua mapato kabla ya kodi na kugawa kwa namba ya wafanyakazi. Tukienda hivyo CRDB is better.

Otherwise ROA measures the efficieny in terms of how assets are returning profits. Sasa 4.7 percent ya Trillion 11.64 ni kubwa kuliko 5 percent ya Trillion 10.4!! Ni sawa na kusema Tanzania tuna uchumi mkubwa kisa unakua kwa 7% ila USA unakua kwa 4%!!!

Realistically CRDB is ahead mkuu percent zisikuchanganye though zinatoa picha tu vizuri kuliko figures za profit in terms of monetary value.
 
Mkuu kwenye scholarly paper zote duniani bank size mara nyingi inapimwa based on market share/penetration/concentration ama total assets. Kibongo bongo ikiwemo NMB operational efficiency inapimwa kwa kuchukua mapato kabla ya kodi na kugawa kwa namba ya wafanyakazi. Tukienda hivyo CRDB is better.

Otherwise ROA measures the efficieny in terms of how assets are returning profits. Sasa 4.7 percent ya Trillion 11.64 ni kubwa kuliko 5 percent ya Trillion 10.4!! Ni sawa na kusema Tanzania tuna uchumi mkubwa kisa unakua kwa 7% ila USA unakua kwa 4%!!!

Realistically CRDB is ahead mkuu percent zisikuchanganye though zinatoa picha tu vizuri kuliko figures za profit in terms of monetary value.
difference ni 0.3 which is almost equally
 
Hili haliko sawa kibiashara, Siku tiGO akiamua kupandisha bei zaidi hata kwa 100% hawezi pata mpinzani kama regulator
Exactly!! Bei za bundle zante zilikua cheap ila menu ya sasa ni copy and paste ya tigo sasa bila ushindani gharama haziwezi shuka... kuna wakati huwa sielewi huko makazini wanashughulikia nini kama mambo obvious hivi wanapotezea!
 
View attachment 2805767
MS Ruth Zaipuna Mkurugenzi Mkuu NMB.

======
Wasalaam Jf team,

Waswahili tunasema " Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake Mpeni "

Sote tunakumbuka baada ya NBC Bank kuvunjwa Mwaka 1997 na baadae kuanzishwa kwa Benki mpya ya Makabwera ya NMB na baadae Benki hiyo kubinafsishwa kwa Rabobank ya Uholanzi iliyomiliki hisa asilimia 49.

Wakati wote NMB PLC imekuwa ikiongozwa na watu kutoka nje ya nchi tu isipokuwa huyu Mkurugenzi wa Sasa Bi Ruth Zaipuna aliyekabidhiwa nafasi hiyo ya Ukurugenzi Mkuu rasmi mwaka 2020.

Kumbukumbu zinaonesha wakati mama huyu anaingia madarakani NMB bank ilikuwa na matawi yapatayo 100 tu nchi nzima na ATMs zipatazo 500 nchi nzima.

Leo NMB bank imefikisha matawi zaidi ya 200 na ATMs zaidi ya ATMs 1,000 nchi nzima hii ni sawa na kusema mama huyu ameikuza bank hii ya Makabwera kwa zaidi ya marambili, yaani ukuaji wa 100% au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema NMB bank PLC imefika katika Kila Jimbo la Uchaguzi la kiserikali haba bara.

Kutoka katika tovuti ya NMB taarifa zinaonesha NMB bank ilikuwa na wateja wasiozidi 600,000 miaka kumi iliyopita na wakati huu wa Ruth Zaipuna banki hii imefikia wateja zaidi ya 2.5M nchi nzima,karibu mara nne zaidi.

Kuhusu Uzalendo & Uzawa Kunajambo la kujifunza kwa hawa wanawake watatu yaani Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Spika wa bunge la JMT na IPU Mhe Dkt Tulia Aksoni na Mkurugenzi Ruth Zaipuna kwa namna wanavyoleta mabadiliko ya kasi kwenye taasisi wanazoziongoza,

Hebu tazama orodha hii ya faida kwa mabenki kumi ya Tanzania yaliyofanya vizuri katika robo ya tatu tu ya mwaka huu wa 2023 ndio utaelewa vizuri nachosema kuhusu huyu Mkurugenzi.

1. NMB Bank: TZS 398 billion

2. CRDB Bank: TZS 280 billion

3. Stanbic Bank: TZS 95 billion

4. StanChart: TZS 64 billion

5. NBC Bank: TZS 62 billion

6. Citibank TZS 44 billion

7. PBZ TZS 41 billion

8. Exim Bank TZS 40 billion

9. Absa Bank TZS 37 billion

10. KCB Bank TZS 35 billion

Taarifa zinaonesha faida ya Jumla kwa mabenki yote Tanzania ni shilingi trilioni moja katika robo hii ya tatu, Hii ni sawa na kusema NMB PLC pekee anamiliki 40% ya faida yote huku ikimpiku kwa mbali mshindani wake wa karibu CRDB bank kwa zaidi ya TZS 118 BL sawa na 70% ya faida yake.

Wakati Ruth Zaipuna anakuwa Mkurugenzi Mkuu Benki hii ilikuwa na wastani wa faida ya TZS 200BL baada ya kodi wakati Leo faida imekuwa na kufikia wastani wa karibu TZS 400BL kwa mwaka yaani sawa na marambili zaidi.

Pia, taarifa zinaonesha Benki ya NMB inashika nafasi ya sita kwa Ukubwa katika nchi zote Kusini mwa jangwa la Sahara na ndio Benki pekee toka Tanzania inayoshindana kimataifa,

Watanzania tuna la kujivunia toka kwa Mkurugenzi huyu mzawa akisaidiwa na management nzima ya NMB PLC pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa NMB PLC chini ya Dkt Edwin Mhede, Hakika Mmestahili Heshima.

Kwa matokeo haya, Huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt Tulia mwingine ni huyu Ruth Zaipuna wa NMB PLC deserves better.
Mkuu nisaidie kuna uhusiano gani kati ya huyu mama na rais? Mama samia kawa rais tayari huyu mama ni md,
 
Mkuu nisaidie kuna uhusiano gani kati ya huyu mama na rais? Mama samia kawa rais tayari huyu mama ni md,
1. Wote ni Viongozi wa taasi kubwa, eg CCM, Serikali, NMB et el

2. Wote ni wanawake

3. Wote ni wanaCCM

4. Wote wanaongoza kwenye awamu ya sita

5. Wote wamekuza uchumi kwa kasi kwenye taasisi zao

6. Wote ni wanadiplomasia wa kiuchumi

7. Wote ni wazawa

8. Wote ni wabunifu

9. Wote wanaamini katika democracy

10. Wote ni wazalendo
 
Back
Top Bottom