Nmeibiwa simu, kesi iko mahakamani. Maswali gani ya kumuuliza mtuhumiwa?

Nmeibiwa simu, kesi iko mahakamani. Maswali gani ya kumuuliza mtuhumiwa?

Humu tu umeshindwa kutushawishi iwapo umeibiwa simu sembuse mahakamani jamaa
 
Wakuu mimi kuna mtu aliniibia simu yangu usiku wa saa tisa nilimuona dirishani(kuna taa imefifia mwanga lakini unaweza kumuona mtu na mlangoni(pale mlangoni kuna ka duara hivi kwahiyo kabla ya kufungua mlango nilimuona na penyewe kuna taa ambayo inamulika vizuri) sasa zikapita siku nikawa namuona sehemu. Ikabidi niende kumshtaki.

Wakauliza anapokaa anasema mtaa ule ule ninaokaa mimi, ila kijana akakataa kata kata kwamba siyo yeye, wakati yeye ndiye niliyemuona ila anabisha. Basi wakasema kesi ipelekwe mahakama. Ndiyo tunasubiria week ijayo.

Vipi ni maswali gani ya kumuuliza mtuhumiwa?
1. Kwa upande wangu, kama una risiti ya kuonyesha ulinunua hiyo aina ya simu na namba zake za kuonyesha ni hiyo sawa na hiyo iliyoibiwa na imekutwa na huyo mtu unayedai aliiba, the angalau una mahali pa kuanzia.
2. Maana kama wewe una original risiti ya kuonyesha mahali uliponunua, sidhani kama na yeye atakuwa na risiti ya kuonyesha alikonunua simu ileile unayodai ni ya kwako.
3. Kama anadai ni ya kwake au aliinunua kwa mtu, mwombe risiti na kasha lake kama bado ni mpya na kama wewe bado unalo.
4. Baadhi ya watu baada ya kununua simu, huweka alama fulani wanayoijua wewe. Kama uliweka hiyo alama, na bado ipo, inaongeza uzito kuonyesha ni simu yako.
 
Anhaa nmekuelewa. Je kama nmeibiwa kweli alafu ikaenda kujulikana aliyeiba siyo yeye au nmemfananisha, ila nmeibiwa kweli kweli. Hiyo nayo inakuaje?
Hiyo sio malicious prosecution kwasababu haukuwa na nia ovu ama ya kumsingizia.

Malicious prosecution ni kumshtaki mtu kwa hila ama bila sababu ya msingi. Lakini ukimshtaki mtu huku ukiamini kabisa aliyekuibia ndiye uliyemshtaki basi hata akishinda kesi hawezi kukushtaki kumlipa fidia kwasababu hukuwa na nia mbaya dhidi yake.
 
KITAKURAMBA, una kesi ya kujibu kwa Jamhuri

Usiku wa saa tisa ulikuwa macho unafanya shughuli gani??

Huyo mwizi uliweza kumuona vipi? Je, kama ni wenge la usingizi? Sababu muda huo kibinadamu unakuwa umechoka unahitaji kupumzika…

Tutakuamini vipi km wewe si mmojawapo wa wezi?

Je, ulikabwa au ulivamiwa?

Wakati tukio linatokea mlikuwa wangapi?
Utaweza kuithibitishia vipi mahakama km mtuhumiwa ni yeye??

Ukijibu hayo maswali umeshinda, otherwise samehe saba mara sabini… simu imelala yoooooo.
Wazee wa baraza watakulia hela na kesi utashindwa mapema sana.
 
Nmeelezea hapo juu jamani, kwamba, NILIKUWA NMELALA, GHAFLA NIKAHISI KAMA KITU KIMENIGUSA MGUUNI, kuja kushtuka nikaangalia dirishani, nikakuta dirisha liko waziiiii simu haipo( nilikuwa nmeiweka juu ya kitanda upande wa ninapoweka miguu nikilala kitandani) nikasimama kulisogelea dirisha nikamuona mwizi chini dirishani, hapo hapo nikaanza kusema simu yangu, naomba unirudishie simu yangu, nikaendelea kumsihi anirudishie simu( niliendelea kumsihi airudishe nikiamini kwamba kwasababu tumeonana angeirudisha) lakini hakufanya hivo badala yake akajibanza ukutani pembeni ya dirisha na kuniomba pesa(laki na hamsini) ili nimpatie simu, me nikamwambia, kwa usiku ule hiyo hela ningeitoa wapi? Tumaendelea kuulizana hivo mwisho wa siku nikamwambia nina elfu kumi. Akanijibu elfu kumi kweli??? Anipatie simu kwa elfu kumi???….. inaendelea( yaani kiufupi ndivyo ilivokuwa.


Pia wewe unayesema nilikuwa nina wenge la usingizi ni hapana. Kwasababu niliamka nikakuta dirisha liko wazi, nikamuona, nikaongea naye, tukakubariana nitoke nje nimpatie pesa( yaani kiufupi nilikuwa nmelala peke yangu ndiyo maana alifanya na hayo yote) sidhani kama ningekuwa na mtu mwingine angediliki kubakia pale hata kuendelea kutaka pesa)

Pia nitaithibitishia mhakama kwamba ni yeye kwasababu nilimuona.!
KITAKURAMBA, una kesi ya kujibu kwa Jamhuri

Usiku wa saa tisa ulikuwa macho unafanya shughuli gani??

Huyo mwizi uliweza kumuona vipi? Je, kama ni wenge la usingizi? Sababu muda huo kibinadamu unakuwa umechoka unahitaji kupumzika…

Tutakuamini vipi km wewe si mmojawapo wa wezi?

Je, ulikabwa au ulivamiwa?

Wakati tukio linatokea mlikuwa wangapi?
Utaweza kuithibitishia vipi mahakama km mtuhumiwa ni yeye??

Ukijibu hayo maswali umeshinda, otherwise samehe saba mara sabini… simu imelala yoooooo.
Wazee wa baraza watakulia hela na kesi utashindwa mapema sana.
 
Unaweza kuileza mahakama muda wa saa 6 usiku ulikuwa macho unafanya nini? Na kama ulimuona mwizi ulichukua hatua gani?
 
Unaweza kuileza mahakama muda wa saa 6 usiku ulikuwa macho unafanya nini? Na kama ulimuona mwizi ulichukua hatua gani?
Usiku wa saa tisa siyo saa sita.( saa 9 siyo saa 9). Nilikuwa nmelala nikashtushwa na kitu kimenigusa mguuni
 
Unaweza kuileza mahakama muda wa saa 6 usiku ulikuwa macho unafanya nini? Na kama ulimuona mwizi ulichukua hatua gani?
Na kwasababu nilimuona mwizi nilichukua hatua za kumsihi airudishe huku nikijua, kwakuwa nimemuona, angeweza kuirudisha
 
Kwa hiyo wote hao hata akili ya ku record sauti yake kama ushahidi au kielelezo hamkuwa nayo 🤣🤣❓
Hatukuweza kurecord kwasababu yule kaka anatumia kiswaswadu. Na niseme ukweli hii ya kurecord hata angekuwa na simu kubwa sikuwa na mawazo hayo muda huo
 
Wewe mwenyewe umeandika usichokielewa sisi ndio tutakuelewa?
 
Hiyo kuhusu simu ya aina gani sijui bei gani, hayo nmeshayaelezea mahakamani wanaijua aina ya simu yangu na bei yake! Kuhusu kwenda police nilikuwa nmeshaenda mara kadhaa lakini sikupata muafaka wa kuipata, lakini mtuhumiwa namuona, hicho kitendo kilikuwa kinaniuma sana ikabidi nikareport police tena kwamba nmemuona mtuhumiwa………… mambo yakaendelea hadi kesi ikapelekwa mahakamani na police. Siyo mimi niliyeipeleka kesi( nilijua kwamba wangemkamata labda angesema hata alipoiweka tu ili niifate lakini alikataa kata kata kwamba hajachukua)!
Ni simu ya aina gani?. Ni ya bei gani?. Ungekuwa umecheza pele sana kuja hapa kabla ya kumpeleka polisi. Utapoteza gharama kubwa kuliko hiyo simu.
Unasema ni yeye mwenyewe ulimuona,je kuna mwingine alimuoma? Hakuna. Hiyo haitoshi. Hiyo kesi achana nayo mapema kabla hujafika mbali
 
Back
Top Bottom