No body cares: Watu tupo bize mtandaoni, tume-lose touch na human connection

No body cares: Watu tupo bize mtandaoni, tume-lose touch na human connection

de Gunner

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
2,044
Reaction score
4,558
Katika hii generation, ambayo watu wapo bize mitandaoni tume loose touch na human connection. Hakuna health relationship na watu wa karibu.

Watu tumegeuka maroboti na mazombie. Hatuna mawazo chanya. Kutwa kuilaumu serikali, maisha magumu, sijui mmomonyoko wa maadili, kumbe wachawi ni sisi wenyewe.

Upweke umekithiri kwasababu, tumeruhusu Technology iweze kureplace maisha halisi. Tunajenga mahusiano na watu artificial mitandaoni, kujilinganisha na watu wasio level zetu. Hii imesababisha tuhisi kama hatuna thamani endapo tutashindwa kufikia level za hao waliopo Mitandaoni.

Sipo hapa kukosoa watu, bali kama tujuavyo vijana ndo nguzo ya taifa na kusema kweli kama kijana naona kabisa tuendako si pazuri
 
Mimi naona ifike pahala tukubaliane tu na hali halisi kwamba dunia imeshabadilika, kushindwa kukubali nako kunafanya mtu azidi kujiongezea stress tu, hakuna namna hapa ndipo dunia ilipofikia and there is nothing we can do about it
 
kuna katoto kakaangu kufika home tu kanyakua simu yangu,akuna cha salamu wala nini.
Ningekanyoosha kanyooke nyoki, watoto tunawaharibu wenyewe wanakosea hatuwaelekezi kipi ni sahihi na kipi si sahihi. Wao kwa umri wao hawayatambui hayo na wa kufanya watambue hayo ni sisi wakubwa kwa kuwapa miongozo kimalezi tangu wakiwa wadogo, ni rahisi kuelekezeka kwa sasa kuliko wakikua.

Kuna wale wazazi wanawalea watoto kwa kuwaonea huruma wanashindwa hata kuwafokea, kuwaadhibu wanapokosea mwisho wa siku anakuwa na tabia za hovyo inakua mzigo hadi kwenye jamii.
Nawapenda sana watoto

NB: SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI.
 
kuna watoto wengine ni kina Junior, ukimpa maelekezo tena kwa staha huku kama unacheza nae mzazi wake hataki.anakua mkali mpaka unashangaa.

mwisho wa siku mtoto anakua shoga au madawa ya kulevya mzazi anapoteza mtoto kwa malezi ya kijinga.
 
Kweli mkuu malezi yanachangia pakubwa sana kumjenga/kumbomoa mtoto.
 
Back
Top Bottom