PreGE2025 No Reforms No Election? Litakuwa kosa la miaka 5!. Simamisheni wagombea acheni kususa

PreGE2025 No Reforms No Election? Litakuwa kosa la miaka 5!. Simamisheni wagombea acheni kususa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kushiriki uchaguzi kwa sheria na kanuni hizi ni kubariki dhambi ya CCM ya dhurma na mauaji.

Ni ujinga kushiriki uchaguzi ambao unajua mshindi atakuwa nani, afu wewe unapangiwa uwe na wabunge wangapi madiwani wangapi
Baada ya uchaguzi unahesabu una vifo vya wanachama wako wangapi, vilema wangapi waliopotea wangapi na wenye kesi za uchaguzi waliopo ndani wangapi.ukipima yote hayo utaona ni mtu mjinga pekee anaweza kusema CDM ishiriki hivyo hivyo.
Hayo ma vyama mengine ni mapandikizi yao - yatakwambia reform zimeshafanyika vizuri na yapo tayari kwa uchaguzi
 
Maneno ya Mkosaji hayo.

CCM chama

ushajiuliza baada ya ‘no reforms, no election’ CDM isipokuwa na ruzuku ya kura za uchaguzi hiko chama kitaendeshwa kwa mapato gani.
Cdm sio taasisi ya fedha, bali ni chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Ni wendawazimu kushiriki chaguzi za kishenzi ili kupata ruzuku za hisani, wakati unaweza kuzipata kihalali.

Narudia tena, ccm ni chama kikubwa kwa sababu za kihistoria na sio sababu ya ubora wake kisiasa. Na kinga yake pekee ni vyombo vya dola, maana vyama vingine vimekubali kubaki kufanya siasa bila kushika silaha kama M23. Siku vyama vingine vikishika silaha ili kifanya siasa kama wafanyavyo ccm, uje tuendelee na mjadala.
 
Lissu ataifelisha chadema kiasi itaishiwa kabiiisa hela na ita-seaze ku- operate!!
Labda ijekumuomba tena Mbowe aisaidie uongozi sio maneno mengine uongozi ni strategies na unahitaji fedha!

..hata sasa hivi Chadema haina fedha, kwa hiyo ni busara wajifunze kutafuta fedha bila kumtegemea mtu mmoja.
 
Yes tunatambua mifumo ya uchaguzi ni mibovu. Inatoa mianya ya rushwa, unyanyasaji kwa wagombea, wizi wa kura na mengine mengi yanayosababisha wapinzani kupokwa haki zao.

LAKINI..

Hawa CCM ukiwaachia upenyo kwa kuwaambia no reform no election hali ukijua kabisa CCM hawana aibu hata wakisimama wao peke yao siku ya uchaguzi.. Utakuwa unafanya kosa jingine la miaka 5. Ambapo tutakuwa na bunge jingine kibogoyo lililojaa ukijani , uchawa na kujipendekeza.

Napendekeza no reform no election, iende sambamba na kuandaa wagombea ili watanzania wenye nia ya dhati waoneshe nguvu ya umma kupitia kura zao.
View attachment 3288363
Kusimamisha wagombea nakwenda kushindwa niupotevu wa muda na pesa kwani mnapubgukiwa na nini vegetables mkienda na uchaguzi peke yenu au muendelee kubali madalakani hela mkafanye shughuli za maendeleo kuliko kupotezea muda wananchi na viini macho
 
Uwe unaelewa,

Bila katiba mpya na time huru ya uchaguzi,

Uchaguzi utayeyuka.

Uchaguzi bila kuwepo sanduku la kura halali ni uwendawazimu,

Wananchi tutakataa ujinga huu usifanyike.
 
Safari hii mambo ni magumu sana kwa CHADEMA. Wanakabiliwa na tishio la kufa na kupona (existential threat).

Mwaka 2019 na 2020 yule mkuu alibuni na kutekeleza mkakati wa KIGAIDI wa kuimaliza CHADEMA kwa mabavu ya dola. CHADEMA walipoteza kabisa kwenye serikali za mitaa na, kwenye uchaguzi mkuu, wakapata mbunge mmoja tu (tena wa kupewa). Wananchi wote walinywea.

Kwa ujasiri na jeuri kubwa, yule mheshimiwa na watu wake walipanga na matokeo yote ya uchaguzi. Kura zilitupiliwa mbali. Waliamua mapema nani awe mbunge na nani asiwe mbunge katika vyama vyote vya siasa (including CCM!). Hata ndani ya CCM wako waliopotezwa. Kisha akaamua kuwapa baadhi ya wanawake wa CHADEMA viti maaumu - kwa mabavu!

Mwaka 2024, awamu ya sita imethibitisha kukumbatia ule mkakati muhimu wa kigaidi kumaliza upinzani. Vitendo na matokeo yalionekana. CHADEMA WASAHAU KABISA KUREJEA STATUS WALIYOFIKIA 2010-2015. Serikali imekuwa na ujasiri MKUBWA zaidi. Kuna uwezekano safari hii hata kile kiti kimoja alichopewa Aida nacho kikachukuliwa - NA WAPIGA KURA WASIFANYE KITU! Kura halisi hazina maana yoyote. Watu wanakupa idadi ya kura zilizopigwa; idadi ya kura za kila mgombea; na idadi ya kura zilizoharibia - toka mezani (desktop)!

Sasa, CHADEMA wakiamua kukomaa na No Reform, No Election, watapuuzwa na serikali itamwaga pesa kurubuni baadhi yao na wapinzani wengine kugombea kinafiki. Hii inaweza kukibomoa zaidi chama kwa ndani na kuzidi kukiondoa kwenye anga za siasa nchini. Au, kutegemeana, na msimamo thabiti wa makada wengi, kinaweza, ANGALAU, kubakia na heshima kubwa ya utimilifu (High moral integrity) mbele ya Watanzania hata kikinyimwa haki yake na kutoonekana kwenye taasisi za uwakilishi tena. (Kingine kinachohuzunisha zaidi ni hizi tetesi nzito za makada wengi kuwa compromised na "pesa za Abduli" zilizoathiri sana chaguzi za ndani hivi majuzi.)

Bila shaka, CHADEMA wakitetereka muda huu, wakabwaga manyanga na kuachana na No Reform, No Election, wakajitosa kwenye uchaguzi watapoteza kila kitu - hata kile kiti kimoja kitachukuliwa - na hawatakuwa na moral authority tena (mbele ya wadau) ya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania. Watapewa label ya wachumia tumbo wakubwa na hawataweza kujitetea na kufanikiwa. Inashauriwa ukitishia kuua basi fanya kweli.

CHADEMA wakomae na No Reform, No election. Hakuna namna.
 
CCM ina huruma, CDM msiache ruzuku ya kura.

Lakini hamna ushawishi wa kuzuia uchaguzi kwa sababu za kipuuzi:

Kabisa CCM wa kutishiwa nyau kwa sababu za kufirika kutoka kichwani kwa Lissu, Heche na Lema.

Hao watu lazima wanaishi lala land.

CCM ni chama kikubwa
20250324_102827.jpg

Kwa msaada wa policcm na sio kwa ushindani.
 
Bado miezi minne. Sawa na wastani wa siku 124! Niwajuavyo CCM hakuna aliyetayari kuafanya mabadiliko ya maana wakati hata wao wenyewe walipigwa butwaa namna mgombea wao alivyo patikana hivi karibuni.

Nakumbuka chaguzi wakati wa kikwete na awamu ya kwana ya maguguli.. Raia walikuwa na uwezovwa kulinda kura za wagombea walio wachagua japo mifumo ilikuwa hii hii mibovu. Swala hapa ni kupandisha morali ya UMMA wa watakao piga kura pamoja na ujasiri wa kusimamia kura zao.

Ni vyema kupigania no reform no election ukiwa anagalau na wabunge 30 bungeni. Kuliko kutokuwa na mbunge hata mmoja
Raia watakaojitokeza kulinda kura zao huoni watakuwa kwenye hatari ya kudhuriwa na vyombo vya dola pamoja na green guard kama tulivyowahi shuhudia chaguzi za huko nyuma !
 
Bora kutokuwa na mbunge hata mmoja historia itawaandika vema kwamba mlisimamia jambo jema kwa taifa na bila uchu wa vyeo na nzi wa kijani wakibaki peke yao hiyo ni aibu kwao na wananchi watazidi kuelewa ubaya wa ccm hii itainua public anger na italeta matarajio Bora sana. Kuliko kushiriki ushirikina huo wa kwenda kwenye uchaguzi huku watu wengine wakiwa;
1. Wameuwawa.
2. Wametekwa.
3. Wana kesi za kusingiziwa.
4. Wameharibiwa mali zao.
5. Wamefungwa jela. Nk

Baada ya yote haya wataiba Tena kura na nyie mtakuwa mmewapa uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani. The only solution ni kuwaacha wafanye uchaguzi wao wenyewe na ccm B wao. Dunia itaelewa.
Itakuwa ni kosa kubwa sana iwapo chadema itaamua kushiriki uchaguzi huu kwani hawawezi ambulia chochote zaidi ya kuja kutambishiwa na masisiyemu kwamba tumeshinda kwa kishindo.Waacheni na uchaguzi wao na tuvyama rafiki twa ccm mtakuwa mmefikisha ujumbe kwamba kuna uonevu chaguzi za Tanzania
 
Matumizi ya vyombo vya dola ktk zama hizi ni makubwa kupita kiasi ndio maana Ccm wanaweza kushinda kwa asilimia 99%, na wapinzani hawana uwezo wa kushindana na mabavu hayo.
Mtu mmoja lisikika akisema ''Na sisi tumo"' huku akiwa amevalia sare na kuonyesha ishara ya kushika bunduki na kupiga saruti. Na mwingine akatamba akisema " kuna kura halali na haramu,na zote zinaweza kutumika ili mradi baada ya hapo unaenda kutubu" Akamalizia kwa kicheko cha kejeli kukejeli wanaoenda kuwafanyia maombi haramu.
Ndo maana tunasema :Safari hii ni mwendo wa NO REFORM,NO ELECTION.
 
Ysani unakiri mifumo ya uchaguzi ni mibovu, then unawashauri kushiriki uchaguzi? Wewe ni CHAWA , unauza sura wakati mshindi anajulikana? Sasa unasema hwana aibu, wameweza kuengua wagombea wote, wamewapa ushindi walioshindwa then unasema wekeni wagombea? Mtu wa hovyo kabisa ww. Kama unajua yote hayo, kwa nini ushamasishe kususia uchaguzi, mpaka mizania iwe sawa. ?
 
Ysani unakiri mifumo ya uchaguzi ni mibovu, then unawashauri kushiriki uchaguzi? Wewe ni CHAWA , unauza sura wakati mshindi anajulikana? Sasa unasema hwana aibu, wameweza kuengua wagombea wote, wamewapa ushindi walioshindwa then unasema wekeni wagombea? Mtu wa hovyo kabisa ww. Kama unajua yote hayo, kwa nini ushamasishe kususia uchaguzi, mpaka mizania iwe sawa. ?
Ngoja tuone!
 
Back
Top Bottom