North Korea Cars

So mtu mmoja anarepresent Taifa? South wana matatizo yao kama North, matatizo yanayoletwa na Ubepari na Income inequalities, kuna Mafukara wa Kutupwa huko south kitu ambacho huwezi kukikuta North.
North Korea hii hii ambayo miaka ya 1990 ilipata njaa kubwa na serikali yao yenyewe ikasema watu 250,000 walikufa, tuachane na makadirio ya UN ambayo wanasema ni zaidi ya milioni. North Korea ambayo hupokea misaada ya chakula, ambayo ni cheap labour wa China na makampuni ya South Korea yaliyokuwa yamewekeza kwenye factory ya mpakani iliyofungwa miaka kama 7 iliyopita. Hata South wenyewe walikuwa wanafurahia kuwafanyisha kazi ndugu zao wa Kaskazini kwa robo ya ujira na bila mikataba.

Kiongozi wao miaka michache kama mitatu nyuma hapo aliwaambia raia wale kidogo chakula hakitoshi. Mwaka jana au juzi alienda kuzindua kiwanda cha mbolea kwa mbwembwe nyingi na bashasha, kiwanda chenyewe walikijenga kwa kusuasua maana priority zao ni silaha. South Korea huwezi kuta Rais wao anazindua kiwanda cha mbolea kama mkombozi. Ni viwanda vya kitoto hata vikifunguliwa havitangazwi
 

Hapa ndio huwa naipenda JF
Only facts
Bravo
 
Kiduku ni noma juzi kabeba jeneza la mtu aliyekufa kwa korona wenzie wamevaa barakoa yeye walaaaa kama jiwe tu ,yule mwamba mtata sana
 
Kiduku ni noma juzi kabeba jeneza la mtu aliyekufa kwa korona wenzie wamevaa barakoa yeye walaaaa kama jiwe tu ,yule mwamba mtata sana
Atakufa kizembe kama huyo mwenzie ambaye sasa hayupo.
 
North Korea Ina njaa muda Mrefu sana, ila jiulize njaa ya North Korea imetoka wapi? Njaa imetokana na Mabomu ya Marekani.

Marekani Alipiga Mabomu na kuua watu Takriban Milioni 8, na Kuifanya Ardhi yote isilimike. For years Wakorea wanabadili Ardhi yao kutoka Ardhi isiolimika mpaka Sasa North Korea Ni kati ya nchi zinazoongoza Uzalishaji wa matunda Duniani.

Hivyo Kuijudge North Korea ya miaka ya zamani kuwa na njaa bila kumponda alieleta hio njaa Na kuua mamilioni ya watu si fair.

Sasa hivi
 
1. Mkuu kwako wewe Magari ndio Standard yako ya Maisha Mazuri, ila wangapi wana Magari na Manyumba wakipata Kigonjwa kidogo tu kama Cancer wanauza kujitibu mpaka wanakufa maskini? Vitu kama Elimu bora, Afya Nzuri ni vizuri kuliko Magari na Vitu Vyengine luxury visivyo na maana

2. Sijaelewa Logic ya Syria huko kuna Vita sijui mfano huo unAingiaje hapa.

3. North Wengi wanaokuja South wanajuwa, Wengine wanataka Kurudi wanazuiwa Kiufupi ni propaganda kwenda Mbele, Soma hapa

Mambo muhimu kwenye hio Article
-kuna watu kibao wametoka North Kuja South ila wanajuta
-ukija South wanakataa Kukurudisha North
-wa North wanafanya Hadi maandamano Kurudi kwao hawaruhusiwi
-wengi wa North Wanadanganywa wakija South watapiga Hela ila matokeo yake wanaishi kwenye Slums na wanakuwa Treated kama Second citizens, kila wanapokwenda wanabaguliwa.

4. Issue ya Media it's So funny eti Tunaziita Media za North Ni za Kipropaganda wakati West kila Siku wanadanganya, kiufupi west ni Clueless kwa Kinachoendelea North.
 
Gari ni nyenzo ya kurahisisha usafiri. Naona wewe unachukulia kumiliki gari ni utajiri.
 
Gari ni nyenzo ya kurahisisha usafiri. Naona wewe unachukulia kumiliki gari ni utajiri.
Gari wanazooongelea wao ni luxury cars, North Korea hawasafirishi Mahindi na mikono ama Mikokoteni, Wanaenda Makazini na Baiskeli ama Magari ya Uma Kutegemeana na Umbali.

Zipo Video Nyingi TU YouTube Zinaonesha Lifestyle yao.

Wana magari kama Mwendokasi zetu, Tena yanatumia umeme, Sisi hata Hatujafika Huko,

Pia wanaotumia Train za umeme,


Kiufupi kwao hakuna Foleni, Husubirii masaa kwenda Kazini ama Nyumbani.


Angalia Mwendokasi Chache zilivyosaidia kupunguza Foleni Morogoro Road, Imagine dar Nzima iwe na Magari machache Binafsi na Mwendokasi kila sehemu na Train za Chini Ya Ardhi.

Pyongyang ina watu kama Milioni 3 si jiji dogo.
 
Magari 30,000 ni mengi sana kwa nchi yenye watu 25 milioni. Ukitaka kujua kuwa hayo magari ni mengi tafuta idadi ya magari nyaliyopo Tanzania yenye watu 60 milioni!!
 
Wapi wamesema wao wanazungumzia luxury cars!? Kwenye post yako niliyoi_quote wewe umeonesha kuwa kumiliki gari ni aina fulani ya utajiri.

Na kuhusu foleni hiyo ni changamoto tu ya wingi wa magari na watu na wala hai_justify hii hoja yako ya kuwa huko North Korea hakuna foleni. Ndio maana miundombinu inaimarishwa kila kukicha kukabili hizo changamoto.
 
Korea ya kaskazini si maskini vile kama tunavyoaminishwa na nchi za magharibi!! Nchi maskini haiwezi kuwa na nguvu hivyo kijeshi. Lakini usisahau kuwa korea ya kaskazini ina vikwazo lukuki ilivyowekewa vya kiuchumi!! Lakini bado inasonga mbele!! Fikiri kama isingekuwa na vikwazo ingefika wapi? Korea ya kaskazini na Cuba ndiyo nchi pekee zilizobaki zinazofuata falsafa ya kujitegemea per se!! Marekani inashangaa wanawezaje? Imekataa hata msaada wa corona!!
 
Hio comment yangu ni response ya Mtu alieshangaa Hoteli maarufu haina Magari ambayo Tayari imelink uwezo wa Kipesa.

Kama North Korea kuna Foleni you are welcome Shusha data
 
Kuna watu watasema Tz ni tajiri kuliko korea ya kaskazini!! Kisa eti kwa kuwa kuna watu kibao wanamiliki vits!! tena second hand!!
 
Hio comment yangu ni response ya Mtu alieshangaa Hoteli maarufu haina Magari ambayo Tayari imelink uwezo wa Kipesa.

Kama North Korea kuna Foleni you are welcome Shusha data
Mara hii suala limekuwa ni foleni tena!
 
Korea kaskazini sio soko la western wana amini katika kukuza uchumi wao kwa Ku boost uzalishaji wa ndani, lkn pia uchumi wa north Korea ni government controlled (Communist model) share the little you have ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…