Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana! Sina hakika kama ni maombi ya Watanzania au ni mapenzi ya Mungu tu, bali kikubwa kuliko yote ni kwamba mwisho wa CCM umefika rasmi baada ya wananchi kuikataa bila huruma.
Asikudanganye mtu yeyote , msingi wa ushindi ni kukubalika kwa wananchi, nimefanya uchunguzi tangu kampeni za mwaka huu zianze , ni dhahiri mgombea urais wa CCM amekataliwa na wananchi, hakuna mwananchi yeyote wa kawaida anayemfagilia mgombea huyu , wengi wa wanaomfagilia japo ni kwa shingo upande kabisa ni viongozi wa chama chake, wagombea wa chama chake na watoto wa baadhi ya viongozi ambao kuishi kwao kunategemea kudra za CCM, vinginevyo raia wengi ambao ni wapiga kura hawataki mtu huyu aongoze tena hata kwa wiki mbili, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni umasikini wa wananchi na kukosekana kwa sera yoyote ya CCM inayonadiwa sasa ya kuwakwamua wananchi kuanzia kwenye Viwanda, biashara kubwa na ndogo ama ajira, Magufuli ameshindwa kabisa kuzungumzia ajira kwa vijana kwenye kampeni zake.
Tumaini kubwa kwa wananchi sasa limebakia kwa Tundu Lissu pekee , ambaye anasifika kwa kunadi sera zake za ajira na uwekezaji wenye tija kwa kiwango ambacho hata mwananchi mwenye uwezo wa chini kabisa wa elimu anaelewa, Lissu ameweka wazi kuhusu sera ya chama chake ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu kiasi cha kurahisisha mno ushindi wake, hofu pekee waliyonayo wananchi ni Wizi wa Kura basi.