Noti ya shilingi mia tano kubadilishwa kuwa sarafu

Noti ya shilingi mia tano kubadilishwa kuwa sarafu

Skillionare

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
1,190
Reaction score
526
Baada ya noti ya shilingi mia tano kuwa kwenye mzunguko mkubwa hivyo kuchakaa mapema,benki kuu ya Tanzania imeamua kuleta sarafu ya shilingi miatano mwaka huu wa fedha inayotamiwa kudumu kwa miaka zaidi ya ishirini
============================================



tanzania-2011-500.jpg

Noti ya shilingi mia tano

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza mchakato wa kufanyia mabadiliko ya noti mpya ya Sh500, ili iwe ya sarafu baada ya kujiridhisha kuwa inachakaa kwa haraka zaidi.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Arusha, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, alisema mchakato kuifanyia mabadiliko na noti hiyo ili iwe katika sarafu, inazingatia ukweli kwamba fedha iliyoko katika mzunguko mkubwa katika jamii.

Profesa Ndulu alisema noti ya Sh500 inatumika kwa kiasi kikubwa na wananchi wengi, jambo linalosababisha kuchakaa haraka kabla ya wakati uliopangwa.

"Tunafanya mchakato wa mabadiliko ya noti hizi zinazochakaa kwa haraka kwa sababu zenyewe zinatumika zaidi," alisema Profesa Ndulu.

Alisema hatua hiyo haitaathiri mzunguko wa fedha na kwamba sarafu ya Sh500 itakapoanza kutumika, noti hiyo itaondoka polepole.
Alisema sarafu hiyo ya Sh 500 itaanza kupatikana katika kipindi kifupi kijacho na kuwawezesha wananchi kuitumia.

"Watanzania wasishituke mabadiliko hayo ya noti za Sh500 kwenda sarafu maana hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watoa chenji,"alisema.
 
Noti ya shilingi mia tano, shilingi ya shilingi mia tano!
 
ina alama ya freemason bora waitoe tu
_
_
 
Do they think that, that will boost up the economy?

By the way, is this Lowasa's project?
 
Mbona hata noti ya shilingi 1000,2000 nazo zinachakaa mapema na pia zinanuka
 
natabiri: kwenye wallet kutajaa misarafu tu mwaka 2025
 
hujaelewa nini

noti ya 500 imeandikwa 'FEDHA HALALI KWA MALIPO YA SHILINGI MIA TANO' wewe unasema noti ya mia tano inaondoka inakuja shilingi. Shilingi iyo inayokuja ikoje? maana hata noti elfu ya elfu kumi...10,000/= ni shilingi.
 
Uchumi wetu unapanda kila mwaka.Je ni kweli unapanda kama mpaka shilingi mia tano inawekwa kwa mtindo wa sarafu? Hii ni hatari sana.
 
Tunako elekea Buku kuwa sarafu muda sio mrefu.
 
Back
Top Bottom