November 25 yagombaniwa, Efm/TvE vs Clouds Media

Kataa kuwa kaa anamaanisha nn?
yani tusiwe na tabia ya kaa,mfano

kaa ukimuweka mwenyewe kwenye ndoo hufiki mbali utamkuta ametoka nje ya ndoo ila ukimuweka na wenzake hawezi kutoka kwa sababu wenzake wanamvuta arudi kwenye ndoo

nadhani mpaka hapo utakua umemuelewa ruge
 
Reactions: SDG
Usijitoe ufahamu kujisahaulisha hao clouds walipopanga show ya Mwana Fa wakati siku hiyo Ladyjaydee alikuwa na uzinduzi wa albamu yake na wasanii aliowaalika Jide hawakwenda wakaenda show ya clouds
Muosha huoshwa [emoji28]
 
yani tusiwe na tabia ya kaa,mfano

kaa ukimuweka mwenyewe kwenye ndoo hufiki mbali utamkuta ametoka nje ya ndoo ila ukimuweka na wenzake hawezi kutoka kwa sababu wenzake wanamvuta arudi kwenye ndoo

nadhani mpaka hapo utakua umemuelewa ruge
Mwambie ruge aache ufala ye wakati anawabania vinega, jide na wengine yeye hakuwa kaa.. now ni mwendo wa kaa tu mpaka iwe moto kaa
 
Clouds washenzi,waonevu,wanyanyasaji etc,walimfanyizia jide kwa kuorganize show the same day ili wammalize hide,walimfanyia sugu the same thing lkn sugu alidhulumiwa mradi wa malaria na ruge hali iliyosababisha sugu kuanzisha harakati za antivirus akawa anashawishi watu wasiangalie wala kusikiliza clouds,lkn yeye akifanyiwa analialia kila mahali. Hakuna namna ya kumfundisha ruge zaidi ya hivi.
 
Kwanza kbla ya yote leo wametaja list ya wasanii watakaoimb fiesta,mr blue,vanesa mdee,jux,weusi,be pol,stamina,rma,ali kiba,maua sama, aslay,na bdo list inaendlea sasa swali show ya efm uend kumwangalia msanii gani mda mwngne tjiulize au ndo kna dula makabila,ishu so bure ishu unaenda kumwngalia nani wa maana
 
Walianza kutangaza Clouds kuwa Ruge atakua Live kwny vyombo vyao ndo hao TV E wakafuata..! Na hio tarehe 25 toka wiki iliyopita Clouds wanaimba kuwa Fiesta Dar wao wametangaza leo tamasha la bure tar 25 unahisi nani mchokozi?
 
Nakumbuka aisee, ni hawahawa kina majay kipindi hicho wana E masters mwananyamala,wanafanya vipindi vya tv vinaruka channel ten kimoja alikuwa anatangaza vj penny...aisee ilikuwa nooma majay alilia siku ile na boys 2 men walipata udhuru wakaahirisha kuja..kuna ile pia haohao Entertainment masters kipindi wameshafungua maisha club wakamleta T PAIN na MIMS..T pain kurudi marekani akakandia sana maandalizi ya ile show ya Tanzania basi kina B12 ACHA WASHADADADIE kwenye xxl...sasa naona Majay yupo kazini kulipa kisasi
 
izo tuzo za eatv mwaka huu zipo?????????????
Tuzo hizo hazipo,na si hizo tu zote hazipo.
Ila Eatv ndo station ya kwanza kuandaa tuzo hapa nchini,jambo la kupongezwa hilo si la kubeza na tuliona zilifana.
 
Mngewauliza Channel ten walichofanyiwa na clouds show ya fally ipupa Arusha..au Mama sakina wa mashujaa band alichofanyiwa siku ya show ya Jb Mpiana mpaka akazimia,watu wanafanya fitna umeme unakatwa show inapoanza ,jenereta lako la standby linakuwa limechezewa,muda huo ukipaniki uanze kuulizia sehemu za kukodi nako fitna ishapita
Na kama hujajiandaaaaa kichawi hata mvua unaletewa
 
Walianza kutangaza Clouds kuwa Ruge atakua Live kwny vyombo vyao ndo hao TV E wakafuata..! Na hio tarehe 25 toka wiki iliyopita Clouds wanaimba kuwa Fiesta Dar wao wametangaza leo tamasha la bure tar 25 unahisi nani mchokozi?
Ina maana ni kosa kuwa na event same day?
 
ngoma inawageukia wao sasa full kupagawa
 
Ndoo maana Leo karibia watangaz wote wa clouds walikuwa wamekazana na kaa na tabia zao kumbe ilikua kijembe kwa Efm
 
Siwapendi kabisa Clauds Media, ni kama wachawi hivi, ni watu wa fitina sana. Wanajifanya wao ndio kila kitu katika burudani. Kama hii fiesta yao itachacha nitafurahi sana.

Pamoja na yote hayo pia siwapendi kabisa Efm/TVe kwa sababu ya upuuzi wao wa kumkumbatia Bashite. Hawa ni sawa na washirikina tu wa kawaida.

Ninaomba matamasha yote haya mawili yavurugike kabisa, Kama ni mvua basi inyeshe kupita maelezo siku hiyo, kama ni vikwazo basi ikiwezekana Magufuli atangaze kabisa kuzuia hayo matamasha ya kihuni.

Mimi sio mnafiki.
 
Kwahiyo wewe ukitaka kwenda kujisaidia huko chooni kwako ndio ulazimishe na mimi nijipangie muda mwingine wa kujisaidia eti kwasababu mimi nawewe ni mapacha? Hahahahaha not to that extent
 
Kama kumbukumbu zangu zitakuwa vizuri fiesta haikuwa brand ya clouds bali ilikuwa ya east Africa Kwa udhamini wa sigara ya sm na vanue yake ilikuwa daimond jubilee.

Ruksa kunisahihisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…