Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Hongera sana. Kadiri unavyo invest kwa muda mrefu zaidi, ndivyo return inavyokuwa kubwa. Mimi tangu nianze ajira yangu ya kwanza mwaka 2015, niliazimia monthly kuweka zaidi ya asilimia 70 ya mshahara wangu UTT kwa sababu sikuwa na sina muda wa kusimamia biashara actively. Nikatumikia committment yangu kwa uaminifu mkubwa.

Kuna miezi nilikuwa nje ya ajira lakini sikutoa hela yangu UTT. Mwishoni wa mwaka 2023, nilikuwa na milioni 200 kwenye account yangu ya Liquid fund.

January 2024 nikatoa milioni 70 nikanunua kiwanja cha square meter 1900 bunju B chenye foundation ya ujenzi tayari.

Malengo yangu ifikapo mwaka 2030 niwe na hela isiyopungua milioni 700 kwenye account yangu ya UTT liquid + hela yangu ya nssf nitakuwa na kama milioni 800 hivi.

Then nimepanga baada ya hapo kutoa milioni 200 nijenge kwenye hicho kiwanja na hela inayobaki nahamishia mfuko wa bond ili niweze kupata mshahara wangu wa kila mwezi from UTT bila jasho. I want to retire at age 42. Tuendelee kufukuzia malengo mkuu...
Ningepata hii akili back then

Big up
 
Wakuu kuna mtu wa karibu nyangu kaomba nimuulize swala, ikiwa mtu anazo 80m kwa mwezi anaweza akachukuwa ngapi?
UTT asante
 
Wakuu kuna mtu wa karibu nyangu kaomba nimuulize swala, ikiwa mtu anazo 80m kwa mwezi anaweza akachukuwa ngapi?
UTT asante
Itakuwa 800k
Sbb ni 1% yake
Ila kwa pesa mingi sijui..
 
Habari,

Lengo sio kujitamba Bali ni kupeana chachu ya kuendelea kupambana. Leo nimefikisha 50ml lengo langu mwaka huu ni 65ml kutokana na saving zangu.

Sihitaji high return business bora nipate low return with minimal risk. Coz biashara imewahi nichakaza nikachanganyikiwa now sitaki kurudia makosa yaliopita. Kwangu UTT ni Bora zaidi! Nimewekeza Umoja, Jikimu, na Bond
Kuna mutual fund nyengine inaitwa FAIDA FUND.
Unaijua?

Nayo ijaribu.

#YNWA
 
Nakubaliana na wewe 100%. Kila mtu ana choice yake na anafanya reseach kwa namna yake. Hii UTT nilikuwa naisikia tu ila mwezi uliopita nikaona niingie kwenye website yao (ambayo nayo sikuipenda sana). Nimesoma soma sehemu ya ''about us'' lakini sikuweza kujua ni nani wamiliki/mmiliki; na hisa za ownership (kama zipo) zikoje. Nikadhani labda ni hiki kiingereza changu kibovu, hivyo ngoja niulizie.
UTT haina mmiliki ila UTT inasimamiwa na Wizara ya Fedha.
Inachofanya UTT ni kukusanya mitaji kwa watu na kuwasaidia kuwekeza.

#YNWA
 
Asante sana. Ni kampuni ya serikali. Bunge lilihusishwa wakati wa uanzishwaji au ni wizara tu au ni nani hasa? Kwa vifungu gani vya sheria? Board of directors na watendaji wake wakuu wanachaguliwa/kuteuliwa na nani?
To cut long story short, unauliza maswali ya kindezi!
 
Asante sana. Ni kampuni ya serikali. Bunge lilihusishwa wakati wa uanzishwaji au ni wizara tu au ni nani hasa? Kwa vifungu gani vya sheria? Board of directors na watendaji wake wakuu wanachaguliwa/kuteuliwa na nani?
UTT ni taasisi inayohusika na ukusanyaji wa mitaji na kuwekeza kwenye low risk areas.
UTT Amis husimamiwa na serikali kupitia Wizara ya Fedha.
Na si kampuni.

#YNWA
 
Nikweli kabisa ..usije ukashangaa utt mbeleni wakaikopesha selikari ikawa ndo bas tena
mkuu,
Kama ulikuwa haujui serikali ya Tanzania
  • ina historia nzuri ya kulipa madeni yake.
  • Tangia uhuru haijawahi shindwa kulipa madeni
  • Pitia data za uchumi na siyo siasa
  • Benki kubwa zote nchini zinatengeneza faida kwa kuikopesha serikali
  • Kama wabisha kasome financial statements za CRDB na NMB
 
Yan nchi bado sana kwenye financial markets...
Pale wizarani tunahitaji wabobezi wenye ku-promote hili suala katika jamii.
Kuna watu Hawajui kuhusu
  • fixed deposit za benki
  • Investment bank
  • Mutual fund
  • Hedge fund
  • External traded fund
  • Stock market
  • Treasury bonds and Bill's
  • Mercantile market
Na lack ya hii knowledge ina kwamisha biashara za bongo zisivuke mipaka.
Wahindi na waarabu ndipo wanapotukamatia uchumi...
 
Habari,

Lengo sio kujitamba Bali ni kupeana chachu ya kuendelea kupambana. Leo nimefikisha 50ml lengo langu mwaka huu ni 65ml kutokana na saving zangu.

Sihitaji high return business bora nipate low return with minimal risk. Coz biashara imewahi nichakaza nikachanganyikiwa now sitaki kurudia makosa yaliopita. Kwangu UTT ni Bora zaidi! Nimewekeza Umoja, Jikimu, na Bond
Hongera mkuu,mi nimepambana nimefika 98M now.mfuko ni liquid fund.Kwa mwezi napata faida ya kama 900k au zaidi.
Niko tempted kuitoa na kujeng nyumba za kupangisha ila nahofia kuanza upya savings as it wasn't easy.Nimeanza more than 4 years ago nimepambana kusave kwa machozi jasho na damu.Najinyima haswa.Nyumba ya makazi ninayo ila biashara zilishanipiga mno kipindi cha nyuma.sina nguvu kabisa ya kurudi humo.Bado najitafakari
 
Unamoyo mwanangu Mimi nina saving 20m Nina miaka 25
 
Unamoyo mwanangu Mimi nina saving 20m Nina miaka 25
Usijali anza mapema utafika mbali,mi ningeanza wakati nna umri wako ningekuwa mbali sana ila hiyo elimu sikuwa nayo, kwa umri wangu najiona nimechelewa.So nakutia moyo usiache ukija kufika uzeeni utafurahia
 
Back
Top Bottom