Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Kununua viwanja na kuwekeza utt kipi ni bora? Na kwanini umesema bora hicho
Me naona UTT, viwanja inabidi uwe na extra mind kabla ya kufanya maamuzi ya kununua, me nlianza kununua viwanja kwenye hzi real estate companies
nlichokuja ku notice bei wanazoweka ni mara mbili ya uhalisia wa thamani ya viwanja, then kiwanja ili uwe na uhakika wa umiliki kwa 100% ni lazima uwe na hati ya wizarani
Sasa watu wanaoenda kununua viwanja kichwa kichwa ni rahisi kupigwa
 
Habari,

Lengo sio kujitamba Bali ni kupeana chachu ya kuendelea kupambana. Leo nimefikisha 50ml lengo langu mwaka huu ni 65ml kutokana na saving zangu.

Sihitaji high return business bora nipate low return with minimal risk. Coz biashara imewahi nichakaza nikachanganyikiwa now sitaki kurudia makosa yaliopita. Kwangu UTT ni Bora zaidi! Nimewekeza Umoja, Jikimu, na Bond
Hongera sana pambana u dabo kabisa kitu kisome 100. Kisha kama uko Bond uanze uanze kula 900k za kila Mwez huku mtaji Unapanda tu

NB: ushauri wa bure.. ikifika mia toa nunua Govt Bond za 15 au 20 years zinakuwaga na return ya 15% kisha hiyo retuen ubairudisha UTT

Mfano kwa 100m Govt Bond ya 15 years to 20 yrs unapata btwn 14% to 15% which means ni almost 15m kwa Mwaka kisha hiyi yote unairudisha UTT kila
Mwaka kwa 10 years.

ukifanikiwa kufanya hivyo maana yake utakuwa ndan ya miaka 10 umewekeza UTT 150m huku ukiwa
Umezalisha profit ya 120m plus

So ikifika Maturity ya Govt Bond yako, hiyi 100m yako itakuwa imekuwazalishia 270m (150m kutoka Govt Bond na 120m UTt) faida tu hapo hatujazungumza maokoto mengine uliokuwa unatupia kukuza mtaji nje ya ile direct fixed ya Govt Bond,
 
Mkuu kwani mimi napinga uwepo wake? Wala sipingi kuwa kuna watu wameshaweka fedha na kutoa. Nimesema tu kwangu mimi, ningekuwa na fedha siwezi kuweka sehemu kama hiyo.
Wateja wa UTT ni tasisi na watu binafsi na UTT yenyewe hizo pesa inawekeza kwenye mabank na Govt Bonds. Custodian wa UTT ni CRDB bank

Kama linapokuja swala la kununua hisa za makampuni mfano CRDB au Cocacola na TBL huna hofu basi hupaswi kuwa na hofu na UTT maana ndio kitu kilekile ndio

Kuna risk moja tu ambayo itapelekea UTT kufilisika na kupoteza pesa zote nayo ni Nchi kufilisika .. sasa linapokuja swala la nchi kufilisika haijalishi pesa yako umeiwekeza wapi.. itapotea tu.. reference ni venezuela walipo default na zimbabwe.

Ukiona kuna biashara ambayo ili ife inabidi inchi ifilisike .. that is the highest bussiness security you will ever get kwenye bussiness

Mwisho jifunze "FIAT MONEY" ndio utajua kwa nini Mutual Funds mfano wa UTT zipo
 
Watanganyika kila jambo wanahisi ni utapeli tu, iruhusu akili yako kujifunza kila uchwao.
Yote sababu ya maisha ya kujikimu tu nayoishi, ujue mfumo wetu wa maisha ni wa kujikimu so mtu kila kidogk anachokioata anawasiwasi nacho na pia kimfumo tumefundishwa biashara ni za kununua vitu na kuuza au kutoa huduma.. hatujui kuna biashara ya kuwekeza fedha kupata fedha.. (hisa na hati fungani)

Ndo maana huyo huyo mwenye wasiwasi na UTT utashangaa anapigwa kwenye miradi ya pyramids schemes kama Mr. Kuku au yale mambo ya wekeza tukulimie tukutafutie masoko
 
Wakuu msaada,hivi ukiwa unapokea gawio la kila mwezi kutoka bond fund,je lile ongezeko la riba la kila mwezi utakua unapata pia au?
LitaongezekA kwa asilimia. Chache nahis ni moja au mbili Kwa sababu faida yako wewe unaitoa ( ushahidi ni
Mie nina pata gawio ila amount ya mtaji inapanda ).
 
Yote sababu ya maisha ya kujikimu tu nayoishi, ujue mfumo wetu wa maisha ni wa kujikimu so mtu kila kidogk anachokioata anawasiwasi nacho na pia kimfumo tumefundishwa biashara ni za kununua vitu na kuuza au kutoa huduma.. hatujui kuna biashara ya kuwekeza fedha kupata fedha.. (hisa na hati fungani)

Ndo maana huyo huyo mwenye wasiwasi na UTT utashangaa anapigwa kwenye miradi ya pyramids schemes kama Mr. Kuku au yale mambo ya wekeza tukulimie tukutafutie masoko

"Maisha ya kujikimu" a.k.a hand to mouth.
Umesema ukweli haswaaa. Na wengi ndiyo tupo hapo... tunaogopa avenues nyinginezo za wealth generation ambazo zinaweza msaidia mtu kusurvive maisha hata pale nguvu za utafutaji zinapoisha (kuzeeka au maradhi ya kudumu).
 
Utt below 50miiion ni kupoteza muda ,labda kama unafanya saving
Pesa inakuwa ndugu yangu with compounding effect. Inategemea lengo lako ni nini? Kama mtu anataka hela za haraka haraka, UTT sio mahali pake. Ila kama mtu ana long term perspective, mifuko ya uwekezaji inamtoa. 10 years and above unaona matokeo makubwa. Wengi humu, nikiwemo mimi, ni mfano
 
Mkuu habari, nilitoa 60ml nikatupia kwenye hisa za CRDB bank. Kuna Uzi niliuleta humu waweza check. Katika speculations na Taarifa nilizopata nimeona CRDB itatoa return nzuri kuliko UTT. Ila nimebaki na akiba ya 8.2ml nazo nataka nikanunue hisa za Nicol coz nazo zitakuwa vizuri mwaka huu
Safi. Ni Malengo tu. Mimi nimejipa miaka 10 mengine ijayo. Nawekeza kiasi kila mwezi bila kutoa wala kuacha. Nataka kuona matokeo wakati huo ukifika 2035. Mungu atusaidie katika safari zetu
 
Wateja wa UTT ni tasisi na watu binafsi na UTT yenyewe hizo pesa inawekeza kwenye mabank na Govt Bonds. Custodian wa UTT ni CRDB bank

Kama linapokuja swala la kununua hisa za makampuni mfano CRDB au Cocacola na TBL huna hofu basi hupaswi kuwa na hofu na UTT maana ndio kitu kilekile ndio

Kuna risk moja tu ambayo itapelekea UTT kufilisika na kupoteza pesa zote nayo ni Nchi kufilisika .. sasa linapokuja swala la nchi kufilisika haijalishi pesa yako umeiwekeza wapi.. itapotea tu.. reference ni venezuela walipo default na zimbabwe.

Ukiona kuna biashara ambayo ili ife inabidi inchi ifilisike .. that is the highest bussiness security you will ever get kwenye bussiness

Mwisho jifunze "FIAT MONEY" ndio utajua kwa nini Mutual Funds mfano wa UTT zipo
Natamani kujua CRDB wanavyohusika na UTT maana nahisi kuna baadhi ya wafanyakazi kwa baadhi ya matawi hawana uelewa na namna CRDB inahusika na UTT. Ningependa kujua kama:-

1. Naweza kufungua akaunti ya UTT kwenye branch yoyote ya CRDB?

2. Naweza kuweka na kutoa akiba zangu za UTT kupitia branch yoyote ya CRDB?

3. Branch zote za CRDB nitakuta form za UTT? (Nafahamu kuwa registration ya online ya UTT haikamiliki bila kufika ofisini)

Kama una uelewe na hili tafadhali
 
CRDB ni custodian wa UTT

1 . Unaweza kununua vipande vya UTT kupitia CRDB na bank zingine kadhaaa mfano NBC, Stanbic, NMB na kupitia mitandao ya simu

2. Unaweza kuuza vipande vyako vya UTT na hiyo pesa itatumwa kwenye account ambayo umeianisha kwenye form yako uliojaza wakat wa kujisajili kwenye mfuko

3. Utaratibu wa kufungua account ya UTT unaanzia kwenye cm kwa kupiga *150*82# na kufata maelekezo au kwa kutumia app baada ya hapo unaweza ukaanza kununua vipande .. kisha unaweza kuchukua form online au kwenda ofcn kwao ukajaza form za ule mfuko ambao ulijiunga nao kupitia cm na utaweka account namba ambayo uliipata ulipofungua kupitia kwenye cm

Unaweza ukafungulia account kwenye cm ukaanza kununua vipande hata kwa miaka 5 ila kama unataka kuuza au kuanza kupokea gawio ndio uhitaj wa kujaza form unapokuwepo ili ujaze taarifa zako za ziada mfano account namba addrss yako na beneficiary wako
 
Now nimehamishia majeshi kwenye hisa hasa za CRDB na NICOL. UTT just for emergency....,.. kifupi nawekeza wanapowekeza UTT na kupata faida. Mwaka huu nahamia kwenye Bond za serikali. Uoga wako ndio umaskini wako
 
Back
Top Bottom