NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

Huo mradi ulitangazwa unauzwa zamani sana, labda kama hukupeleka dau,
Ila hujachelewa, wamesema hawajaconclude, wahi uwapindue
Ngoja ni kashindanie zabuni mzee [emoji383]
 
Ni jambo jema kama amepatikana mmiliki mpya. Sema tu hawana sababu ya kumficha huyo mnunuzi. Maana ni suala tu la muda kabla hajafahamika rasmi.
Mnunuzi asiyekuwa na mawaa yoyote, kuna sababu zipi hasa za kumfanya awe siri?

Huyu mnunuzi atakuwa amepewa upendeleo gani kiasi kwamba Serikali inaona shida hata kumtaja tu?

Kapewa RUZUKU ya Serikali kumsaidia katika ununuzi huo?

Au mnunuzi huyu, ni kikampuni cha akina 'Abdul Ameir' na wenzake wanaofaidi matunda ya kuangukiwa na embe chini ya mti wa mkungu?

Ni swala la muda tu, yote yatafahamika.

Na akitokea kichaa mwingine akaliongoza taifa hili, hawa siyo watu wa kuwaonea huruma hata kidogo.
 
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.

Bora wauze tu ili mwekezaji apaendeleze, miradi mingi tu Kigamboni na DSM nzima Magufuli ndio aliiuwa. tungekuwa mbali sana.
 
Bill Gates kashafanya yake hapo wanashindwa kusema tu sheria hairuhusu asiye mzawa kumiliki ardhi
 
ZIle kelele za kurekebisha sheria ili wageni wanunue nyumba nafikiri sio za bure, tunaandaliwa kisaikolojia.

Nchi ina watu wa hovyo hovyo sana hii
Huko mbali sana na ukweli.
Hilo ndilo lilikuwa lengo la marekebisho ya sheria zile.

Sasa pima picha itokee Samia kwa miujiza isiyojulikana, hapo 2025 akapewa upya kukaa kwenye nafasi hiyo anayoishikilia sasa, hili taifa tutabaki na kitu gani hapa?

Wakati akishikilia nafasi tu, ambayo kamwe hakustahili kuishika, kadiriki kufanya uchafu kiasi hiki, itakuwaje akipitishwa kwa nafasi yake mwenyewe?

Kama waTanzania hawawezi kushtushwa na haya waliyoyaona wakati huu, sijui ni jambo gani tena linaloweza kuwashtusha!
 
Kuna yule Azimio aliingia ubia na NSSF na kuithaminisha ardhi iliyotumika kwa bei ya kuruka mpaka akaingia kwenye ripoti za CAG, wamemalizanaje? Maana hisa zake zilikuwa 55%
Inawezekana sana mnunuzi ndiye huyo huyo.
Tega tu sikio,maswala ya aina hii hayafichiki.
 
ZIle kelele za kurekebisha sheria ili wageni wanunue nyumba nafikiri sio za bure, tunaandaliwa kisaikolojia.

Nchi ina watu wa hovyo hovyo sana hii
Napenda san jinsi unavyo ipendaga nchi yako pale inavyo fanya Mambo ya kipuuzi naona unaumizwa sna
 
Kama kuna miradi mingine inadorora iuzwe tu sababu hakuna namna.
Kucheka na wapiga deals kunaumiza watanzania wanyonge sababu raslimali zao zinapotea.
 
Nikitulia vzr niatupia picha ya kota za dege zilizotelekezwa kwawsio jua
 
bora wauze tu ili mwekezaji apaendeleze. miradi mingi tu kigamboni na dsm nzima magufuli ndio aliiuwa. tungekuwa mbali sana.
Wee jinga Kweli Sasa ikiuzwa kila kitu wanetu watakuja kuwa watwna ktk nchi Yao

HV unaifahamu huo mradi au zile gorofa au uliona picha tu
 
Ushafika kwenye mradi vitu vingi vimeibwa vitu ngivi vimeharibik
Kuna watu wanao ishi jirani na zile nyumba kipindi inasimamissshwa na mkandarasi kufukuzwa jamaaa waliingia ktk site ya mkandarasi wakaiba kila kinacho bebekaa Ni hasra kubwa imepatikana pale

Nina video nimeichukuwa mm kipindi nafanya Kaz mitaa hyo nikuoneshe jinsi mradi ulivyo telekezwa
 
Wee jinga Kweli Sasa ikiuzwa kila kitu wanetu watakuja kuwa watwna ktk nchi Yao

HV unaifahamu huo mradi au zile gorofa au uliona picha tu
shida yako ni kwamba kichwa chako kimejaa kamasi na hata hutaki kupeng'aa zitoke. mradi wa NSSF kigamboni uligubikwa na rushwa mno na yule ustaadh aliyekuwa na msikini ndani ya ofisi ya nssf kama unamkumbuka. Magufuli alipoingia alifukunyua hadi mradi huo ukakwama, kama kuna mwenye uwezo, awe mtanzania au sio mtanzania akinunua atapaendeleza. pesa waliyouza wanaweza kuwekeza kwengine kwenye faida zaidi kuliko huko kwenye real estate. waende wanunue hata corporate bonds tu BOT au wanunue hisa kwenye mabenki yenye faida, pesa itajigenerate. kwani kabla hawajauza, wewe na watoto wako mlikuwa mnamiliki nini kwenye yale majengo? au na wewe ni wale wasindikizaji tu?unaelewa nani huwa anafaidika na hayo mashirika? wewe ni mmoja wapo?
 
Wee Ni mjinga na umeonesha ujinga wako hapa tayari

Kwa Sasa sibishani na watu wajinga humu nawalia bati ndengelezi
 
Back
Top Bottom