NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

Ni jambo jema kama amepatikana mmiliki mpya. Sema tu hawana sababu ya kumficha huyo mnunuzi. Maana ni suala tu la muda kabla hajafahamika rasmi.
Umafahamu kwamba NSSF ilitumia Trillion 5 kwenye huo mradi halafu wanadanganya ni Bilioni 330?
 
Hatari thana...
AIP01SBV0DQ Imethibitishwa.Umepokea Tsh50.00 kutoka 219777 - M-PESA FAIDA tarehe 25/9/23 saa 12:39 AM Salio lako ni M-Pesa ni Tsh70.30.
AIM7ARL1ZTJ Imethibitishwa. Tsh50.00 imetolewa kwenye akaunti yako ya M-Pesa tarehe 22/9/23 saa 11:31 PM kama malipo ya huduma ya M-Pesa Songesha. Salio lako jipya la M-Pesa ni Tsh0.55. hatari na nusu🤠😂🤣
 
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.

Ata wafanyeje tutajua tu, hakuna siri Tanzania.
 
Siku hizi tumeona njia ya kimya kimya, ndiyo nzuri! Si umeona hata kwenye ishu ya bandari na DP WORLD?
Samia mwenyewe akisafiri kwenda kwa wajomba Uarabuni ni kimya kimya tu ingawa anasafiria ndege yetu!
Ukiona wanafanya kimya kimya ujue corruption is involved hivyo wanaficha!
Sintashangaa kama mnunuzi atakuwa sheikh Maktoum of 🇦🇪!!
 
Hizo hesabu umezitoa wapi Mzee?
Weka ushaidi anuwahi ikibidi tuingie mtaani.
Kakague mahesabu ya kipindi yupo yule Mwizi Dau, hivi kama Zahanati ya vyumba vitatu huko vijijini wanajenga kwa Bilioni 3, unaamini mradi kama huo wajenge kwa bilioni 300?!
 
Ambacho najiuliza mradi ukikamilika kama tatizo la ajira ambalo ni kubwa sana je hauwezi kuwa ghost town huo mji hapo wangap wako tayari kuishi uko na bei wataimudu sababu ya sheria zetu wageni ni ngumu kununua
 
Nabado hasara ya Bil330 kukaa kwa miaka 8 bila kuwa kwenye mzunguko.
Unapouza kitu huangalii ulinunua bei gani, unaangalia thamani ya hicho kitu leo,
Ukinunua pencil ✏️ kwa 50,000/- sio lazima uuze 60,000/-,
Utakuja kuuza kwa bei ya soko ambayo ni 200/-

Huo mradi wanasema wametumia pesa nyingi ila kumbuka zilipigwa sana pesa hapo, bei ya vitu zilikuwa inflated sanaaaaaa
 
kile siyo kijiji, ni kata (Eco ward).
Ukiona mafao tunayopewa na NSSF halafu ukaangali uwekezaji wa namna hii - kweli kuna watu watakuwa na maswali mengi ya kujibu kwenye ile hukumu ya haki
 
Kigamboni ni very strategic kwa ulinzi wa nchi kama lilivyo eneo la Pugu. Sasa anapolinunua mtu asiyejulikana, ni hatari sana. Mimi siyo mtabiri ila ni kama naiona Tanzania ikiingia katika machafuko yatayachukua miaka mngi sana kuisha
 
Karibu Ameer, hakikisha Riz1 hakushindi hahahahaha
 
Ni uamuzi mzuri.halafu ni mali ya umma ilipaswa itangazwe tender,mwenye interest ili wacompet
 
Ni uamuzi mzuri.halafu ni mali ya umma ilipaswa itangazwe tender,mwenye interest ili wacompet
Huo mradi ulitangazwa unauzwa zamani sana, labda kama hukupeleka dau,
Ila hujachelewa, wamesema hawajaconclude, wahi uwapindue
 
Ambacho najiuliza mradi ukikamilika kama tatizo la ajira ambalo ni kubwa sana je hauwezi kuwa ghost town huo mji hapo wangap wako tayari kuishi uko na bei wataimudu sababu ya sheria zetu wageni ni ngumu kununua
Ndio ujiulize, yule taahira Dau aliwaza kwa kutumia tumbo lake alipopeleka matrillion ya pesa za wanachama kule akijua afika bado sana kuweza kupata soko kwa kule.., kule pata changamka, ila nado decades to come.
 
Sababu uko kigamboni kuna sehemu kuna nyumba nyingi zimejengwa na hazina watu.Nikifatilia nchi zilizoendelea sehemu ambazo serikali ilijenga na hakuna kazi kumekuwa magofu watu wamekimbia
 
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.

Ni jambo jema lakini ni kweli hiyo bei ipo kwenye makaratasi kabisa?

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom