NSSF yazidi kuumbuka: Ufisadi wa ujenzi wa Hoteli Mwanza, jengo la biashara Mzizima

Mbona hakuna mahali inaonesha hizo Billion16...
 

Msisahau na magodown ya Ubungo,Manji alikopa hela NSSF akanunua na kuyakarabti tena hayo magodown ambayo yalikuwa yanamilikiwa na NSSF na kuyauza tena kwa NSSF kwa hela ndefu.Majengo mengi ambayo ni''vitega uchumi''sasa yamekuwa magofu hayana wapangaji,nenda pale mjini Moshi Kilimanjaro baada ya Uchumi Supermarket kufunga shughuli zake hakuna tena mpangaji yoyote wa maana,hii miradi ilikuwa ni sehemu ya kufujia fedha za wafanyakazi na haina tija kwa shughuli za NSSF sababu haingizi mapato yoyote zaidi ya kutia hasara,ninaamini hayo majengo yalijengwa kwa kuwekea cha juu cha nguvu ambacho kilirudi mifukoni kwa waendeshaji wakuu wa NSSF,haya mambo ndio sasa yamerudia tena NHC na hadi kumfanya Waziri Lukuvi ashtuke,kuamuru menejimeny ya NHC kutoaanzisha tena miradi mipya,tukumbuke Msechu na timu yake wamekopa mabilioni katika mabenki hapa nchini je kwa miradi kama hii ambayo haina soko hizo hela(mkopo) pamoja na riba zake watarudisha kwa pesa ipi kama sio tena kwenda serikalini na kuomba kodi za wananchi ndio zilipe?wakati wao tayari wameshachukua cha juu ,nadhani ni wakati hawa viongozi wa mashirika/mifuko hii wachunguzwe mali na rasmali zao walizonazo kwa maana wana UKWASI wa kutisha,tusisubili tu akina FONSECA walipue mabomu ndio tujua watu wana vijisenti vyetu kwenye Offshore accounts,kama za Panama.
 
Jamaa anazidi kuvuliwa nguo ni sawa na mwanaume kamfumania mkewe halafu akakaa kimya bila kutoa adhabu kwa mke lazima akimbie dau sijui anamtazamaje magufuli sasa hivu
 
Hii nchi watu wachache waliitumia bila huruma kwa walio maskin..mungu jaalia mafisadi wote waumbuke
 
awamu hii chongeni mabenchi ya kukalia ofisinimuzoee kabisa ili siku ukienda kisutu usipate shida kukaa, pia kaeni na ndoo kwenye gari manake wengine watakuwa wanakamatwa hata maofisini wanapelekwa kisutu.
Kama walivyo fanywa wabunge wa ccm kwa tuhuma za rushwa
 
Mkuu tukisema tuingize udini kwenye ufisadi nchi hii wagalatia mtaumbuka.una habari kuna meli zaidi ya 65 zimepotea katika bandari ya Dar es Salaam?
 
Escrow account mkishirikiana na maaskofu mmechota sh.ngapi? Msiingize dini kwenye haya masuala tutaumbuana hapa.
 
hapa kwenye hili la Dau kuna chain ndefu,kuna mazito makubwa tunaweza yasikia.hata Magu anaweza kushindwa kutumbua hili jipu,maana kuna watu atawaonea haya
Unaweza kukuta mzunguko umeingia mpaka kuchangia kampeni zake.
 
Yaani huyu Alhaji Dr Dau pamoja na kujenga msikiti ofisini bado alikuwa ana tabia mbaya hivi? Kumbe hata huko Macca watu wanaenda kutalii tuu na sio kutubu na kuwa watu wema.
 
Kuna watu walikuwa wanampigia chapua mkuu wa NSSF awe waziri wa fedha. Sipati jibu ingekuwa vipi!
 
Mh! inaumisa kichwa ukiisoma hii habari
 
Duh noma sana ila hebu tujadilini pasipo kugusa mambo ya dini. Nchi ilikuwa nyang'anyang'a
 
Mkuu tukisema tuingize udini kwenye ufisadi nchi hii wagalatia mtaumbuka.una habari kuna meli zaidi ya 65 zimepotea katika bandari ya Dar es Salaam?
Kama mgalatia amehusika awajibike, nakemea udini kwa nguvu zote, ndo maana nilikuwa nawaona watu wanaomtetea dau kwa udini hawajielewi, sasa yanawatokea puani, usininukuu vibaya mkuu, siupendi udini ila nachukia kumtetea mtu kwa sababu ni dini yako
 
Hii filamu naifananisha ya ile ya january makamba..Mwisho wa siku Magu hatofanya lolote kwa dr dau.

Huo ndio ukweli sidhani kama anaweza kumwajibisha Dau kwa muda huu labda angekuwa ameshakabidhiwa kofia ya chama taifa ambayo kama haitakuwepo figisu yoyote uenyekiti atakabidhiwa mwezi June mwaka huu.Kwa sasa hivi Dau atakuwa na wengi wa kumtetea ndani ya chama na wanauwezo wa kumuamuru raisi kumwacha kwani hayo mabilioni hakufaidika nayo peke yake bali wapo na wakubwa.Ninachoelewa Magufuli akishakabidhiwa kofia ya chama taifa ataanza kukisafisha chama kwa kuwaondoa kwenye chama mafisadi wote waliojificha humo na kuwapeleka mahakamani pale penye ushahidi.Pia kosa la jinai halina muda maalumu unaweza kumpandisha mtuhumiwa mahakamani wakati wowote. Ninachoshauri raisi aache utaratibu wa kuwapangia kazi nyingine wote wanaoondolewa kwenye nafasi za uongozi kabla ya mhasibu mkuu kufanya uchunguzi alikotokea.
 
Sitashangaa kusikia mzee wa msoga amemtembelea JPM magogoni, no, I mean Chato
 
Mungu mkubwa , ila kuna watu wamekula hii nchi aisee, wanajifanyia tu wanavyotaka na ndio maana kila mtu anaweza afanye chochote awe kwenye hii mifuko ya Kijamii, miradi ya uwekezaji yote ni vizuri ikapitiwa la sivyo kuna hatari ya watu kukosa mafao yao.Nadhani hili suala la udini hapa halina nafasi kabisa na huu upigaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…