Ntaifanya Tanzania kuwa na better ecosystem ya mpira wa miguu Africa

Ntaifanya Tanzania kuwa na better ecosystem ya mpira wa miguu Africa

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
5,559
Reaction score
8,747
Nikiwa Rais wa Tanzania ntatengeneza mazingira ili mpira wa miguu uwe unachangia kodi ya sh Trillion 1, ntahakikisha mtoto aliyezaliwa uganda, kenya, Rwanda, Dr Congo, Zambia, n.k anakua na ndoto za kuja kucheza ligi ya mpira ya Tanzania, wote tunafahamu culture ya mpira wa miguu Tanzania ni kubwa sana yaani watu wanapenda sana mpira wa miguu ila ubora wa ligi ni mdogo sana

Serikali yangu itatenga Trillion 2 kwa ajili ya kuboresha na kujenga
  1. Viwanja vya mpira vya kisasa
  2. Viwanja vya mazoezi vya kisasa
  3. Viwanja kwa ajili ya mechi za academy kuanzia
  4. Viwanja vya mazoezi vya academy kuanzia miaka 6

Viwanja hivi vya mpira vya kisasa na vya mazozi kwa timu ambazo ziko tayari watapewa kwa makubaliano ya kuilipa Serikali kidogo kidogo kwa mda flani ili waweze kuvimiliki, na hii itaongeza wigo kwa timu zetu kuwa na asset kwa sababu changamoto kubwa timu zetu hazina assets

Kutakuwa na mpango wa kuibrand ligi kuu ya Tanzania na kuiita Swahili Professional league, wadau watatoa hitimisho ya jina la ligi ambalo litakuwa linaendana na historia ya nchi

Mchanganuo wa kuhakikisha Timu za ligi ya Tanzania zinakuwa na uwezo wa kujiendesha

  • Broadcasting
Kila timu inatakiwa ipewe billion 3 na baadae itaongezeka maradufu-kutoka kwenye kurusha mechi za mpira wa miguu wa Tanzania, fedha wanayopewa timu za Tanzania ni ndogo sana na thamani ya ligi iko juu, na hapa anayerusha mechi za mpira wa miguu hatakiwi kuwa chombo kimoja kama ilivyokuwa azam pekee yake sio sawa hata kidogo vinatakiwa kuwa na vyombo kama vitatu hivi

  • Serikali
Serikali itakuwa inatoa billion 1, na baadae zitafika mpaka 5 kwa kila timu inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania na kwenye kila jezi ya timu kutakuwa na sehemu ya kuitangaza nchi ya Tanzania kama sehemu ya ku-compasate fedha wanayopewa nikimaanisha hawatapewa bure

  • Kuvutia makampuni wakubwa wa jezi kama Adidas, Nike, new balance
Ligi yetu ikiboreshwa itakuwa ni rahisi sana kuwavutia watengenezaji wakubwa na hii itaongeza mapato kwa timu zetu tofauti na sasa hivi watengenezaji wa jezi ni wababishaji kwa asilimia kubwa na timu hazinufaiki ipasavyo kutoka kwenye jezi zao

  • Matangazo kwenye jezi za timu lazima yawe na manufaa kwa timu
Sakata la simba la mmiliki kupata kigugumizi juu ya gharama za Matangazo kwenye jezi za timu limeleta maswali mengi saba na lazima liangaliwe kwa umakini mkubwa sana, nikimaanisha timu hatakama inamilikiwa na mtu iwe na uhuru wa kutangaza kampuni nyingine ambazo mmiliki hazimiliki

  • Ukaguzi
Kutakua ni sheria kwa timu zote kuwa zinafanyiwa auditing ili kujua namna ya fedha zinavyotumika

  • Kuzifanya timu za mpira za Tanzania ziweze kukopesheka
Timu za Tanzania zinatakiwa zitengenezwe kitaasisi ili ziweze kukopesheka sasa-hivi ni ngumu sana kukopesheka zimekuwa watumwa kwa kutegemea watu au vikundi vya watu

Mdhamini wa Timu atafuata utaratibu wa namna ya kuwekeza kwenye
sio sawa mwekezaji a aibu kama huko tu nakusema nimetumia kiasi flani mbona hasemi kiwango alichoingiza huu ni uhuni ambao unatakiwa ukataliwe na kupingwa, sakata la simba na mohamed Dewji limetufumbua macho lazima tuhakikishe kila upande (mwekezaji na timu zinanufaika

 
Ukiwa na agenda nzuri nzuri kama hizi huwezi PATA urais
 
Back
Top Bottom