Pre GE2025 Ntobi avuliwa Uenyekiti Mkoa wa Shinyanga kutokana na utovu wa maadili na nidhamu dhidi ya Lissu

Pre GE2025 Ntobi avuliwa Uenyekiti Mkoa wa Shinyanga kutokana na utovu wa maadili na nidhamu dhidi ya Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni "precedent" kwa sababu wengine walifanyiwa? Retribution imeanza. Kinachofuata ni kuwafukuza wale wote waliothubutu ku mcritise messiah.

Yetu macho.

Amandla..
Kwa Ntobi ilikuwa wazi Sana, hakuna heshima wala adabu, kwenye mdahalo alikuwa anazungumza kama kalewa, huwezi ona ccm kiongozi wa mkoa akimdhalilisha makamu mwenyekiti eti mropokaji au mpiga mikwara ya ovyo Sijui nn
 

Kamati tendaji ya Kanda ya Serengeti katika kikao chake cha jana Jumatano Januari 08, 2025 kimefikia maamuzi ya kumvua Uongozi Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Bw. Emmanuel Ntobi kutokana na utovu wa nidhamu na maadili ikiwemo kuchafua Viongozi wa Chama chake Kitaifa kupitia mitandao ya Kijamii.

Akizungumza ma JamboTv Usiku huu (Januari 09, 2025) Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la CHADEMA Kanda ya Serengeti Lucas Ngoto ameiambia JamboTv kuwa maamuzi hayo ya Kikao yamefikiwa Kisheria ikiwa ni mara baada ya kumpa fursa ya kuweza kujitetea dhidi ya kauli na maandiko yake kadhaa yasiyokuwa na utu na heshima kwa Viongozi wa Chama Taifa.

Ntobi ambaye pia mwaka 2023 aliwahi kusimamishwa Uenyekiti wake kwa mwaka mmoja kutokana na makosa ya kinidhamu, amejitanabaisha mitandaoni kama muungaji mkono na Mpiga kampeni kwaajili ya Mhe. Freeman Mbowe kuweza kurejea tena madarakani kama Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, amekuwa na mfululizo wa maandiko kadhaa, yenye nia ya kumchafua, kumtweza na kumtusi Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Tundu Lissu ambaye pia ni Mshindani na mgombea mwenza wa Mhe. Mbowe kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Chadema taifa kwenye uchaguzi utakaofanyika baadae mwezi huu.

Miongoni mwa kauli zake ni pamoja na kumuita Makamu mwenyekiti huyo kuwa Mropokaji, Mmbea, sambamba na kumtuhumu kufadhili na kuunda kikosi kilichokuwa kinatumia jina la "Sauti ya Wananchi" akishirikiana na watu maarufu mtandaoni na maafisa wa CCM, idara ya usalama wa taifa na Diaspora kwaajili ya kumfitini Mhe. Mbowe

Aidha Ntobi amekuwa akimuhusisha na baadhi ya matendo yasiyofaa kimaadili kupitia maandikio yake akimuhusisha na "Mzungu" hasa pale Mhe. Lissu anapokuwa safarini nje ya nchi kama " Soon ataweka wazi faragha za Mzungu wake" pamoja na "Si tuliwaambia jamaa yenu kakimbilia kwa mtasha wake? kiko wapi?", mwisho wa kunukuu
Huyo hana masdili na hafai kuwa kiongozi. Avuliwe tu!
 
Kwa Ntobi ilikuwa wazi Sana, hakuna heshima wala adabu, kwenye mdahalo alikuwa anazungumza kama kalewa, huwezi ona ccm kiongozi wa mkoa akimdhalilisha makamu mwenyekiti eti mropokaji au mpiga mikwara ya ovyo Sijui nn
Kwa hiyo CDM ya Lissu itakuwa kama CCM? Kama sio mropokaji ana dhalilika vipi?

Amandla....
 
..lissu hakurupuki boss, ana cheza na maneno, ni mwanasheria yule, Ntobi aliingia live, huwezi sema makamu mwenyekiti Wako ni mropokaji
Kwa nini hawezi kusema Lissu ni mropokaji anaebebwa na diaspora feki? Au Lissu nae ni "dikteta uchwara"?

Amandla...
 
Unaweza kuta wanaandaa mazingira ya kuja kutaka kumvua Lissu uanachama. Tuwe makini sana.
Sidhani kama wanaweza kufanya hilo,litakuwa na madhara makubwa kwani itaonekana dhahiri amewashinda kwa namba tayari sasa wanamuengua ili wasiabike na hii itakuwa inadhirisha kuwa wanafuata maelekezo ya CCM ambao ndiyo waasisi wa kuengua wagombea wanaowaona wana nafasi kubwa ya kushinda. Anyway let's wait n see maana Waswahili wanasema sikio la kufa halisikii dawa.
 
Back
Top Bottom