Sijui watu wanataka Simba wacheze mpira gani. Watu wamejiuliza game plan ya Simba jana ilikuwaje? Yule kipa wa Vipers karibia avunjike kiuno kwa saves alizokuwa anafanya.
Mchezaji ambaye naweza sema alicheza chini ya kiwango ni Saidoo na Kanoute. Kanoute hana kawaida ya kucheza chini ya kiwango kwa hiyo itakuwa aliamka tu vibaya. Kimekuwa kilio changu cha muda mrefu kuwa Saidoo asianze game ila kilio changu bado hakijasikika. 90% ya movement zake anapoteza mipira au anaanguka. Inawezekanaje mchezaji mwenye mwili kama wake anakuwa dhaifu dhaifu vile. Anajichekeshachekesha tu hovyo.
Phiri alikuwa tishio sana kipindi cha kwanza ila viungo waliacha kumlisha mipira kwa hiyo alipotea kidogo kipindi fulani. Nilitabiri angetolewa na kweli ikawa hivyo ingawa aliyestahili kutoka mapema ni Saidoo.
Ukiacha hayo muhimu ni point 3. Hii ni timu ya tatu Simba inaifunga nje ndani msimu huu bila kuruhusu goli kutoka kwao.