Nukuu za wachambuzi maarufu Baada ya mechi ya Simba (wakimataifa)

Nukuu za wachambuzi maarufu Baada ya mechi ya Simba (wakimataifa)

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Baada ya mechi ya kibabe Jana kuisha Kwa mnyama kuchukua point 3 za nguvu pale Kwa mkapa hatoki mtu ( isipokuwa Raja Casablanca na Young Africans). Na kujihakikishia mguu ndani vs nje kwenda robo fainali.

MAONI YA WACHAMBUZI BAADA YA MECHI YA SIMBA DHIDI YA VIPERS

Hizi ni nukuu za baadhi wa wachambuzi maarufu hapa bongo .....wanaoufanya mpira usonge mbele ..

Shaffih Dauda - Mchambuzi CLOUDS
"Ni bahati tu Simba SC imeikuta Vipers na yenyewe ikiwa dhaifu, pamoja na ushindi Simba imeonesha kiwango cha chini sana"

1678257646897.jpg
 
Jemedari Said - Machambuzi EFM

"Ukweli mchungu ni kwamba mnyama KACHOKA na hawezi tena kufanya maajabu yake yaliyozoeleka. Imani kwa Simba ni kubwa kwenye haya mashindano miongoni mwa Wananchi ndo inafanya waamini ipo siku watabadilika, lakini ukweli timu iko UNGA kinoma"
 
"Nimemuangalia Chama, nimeuona Mchezo mzima tena kwa kiwango kizuri, lakini nimeiangalia Simba SC sijauona mchezo mzima kwa kiwango cha Chama .. Na hii ilikuwa dhidi ya Vipers FC, je dhidi ya AC Horoya itakuwaje? "

Abissay Stephen Jr - Mchambuzi EAST AFRICA
 
Sijui watu wanataka Simba wacheze mpira gani. Watu wamejiuliza game plan ya Simba jana ilikuwaje? Yule kipa wa Vipers karibia avunjike kiuno kwa saves alizokuwa anafanya.

Mchezaji ambaye naweza sema alicheza chini ya kiwango ni Saidoo na Kanoute. Kanoute hana kawaida ya kucheza chini ya kiwango kwa hiyo itakuwa aliamka tu vibaya. Kimekuwa kilio changu cha muda mrefu kuwa Saidoo asianze game ila kilio changu bado hakijasikika. 90% ya movement zake anapoteza mipira au anaanguka. Inawezekanaje mchezaji mwenye mwili kama wake anakuwa dhaifu dhaifu vile. Anajichekeshachekesha tu hovyo.

Phiri alikuwa tishio sana kipindi cha kwanza ila viungo waliacha kumlisha mipira kwa hiyo alipotea kidogo kipindi fulani. Nilitabiri angetolewa na kweli ikawa hivyo ingawa aliyestahili kutoka mapema ni Saidoo.

Ukiacha hayo muhimu ni point 3. Hii ni timu ya tatu Simba inaifunga nje ndani msimu huu bila kuruhusu goli kutoka kwao.
 
Sijambo mkuu..ww hujambo pia? Hahah eti wa rika langu 😄 😄
Mimi sijambo nafurahi tuu hapa jinsi vijana wetu walivyo tuokoa Jana.😅😅wee niwalika langu ndio au ulinidanganya wewe bado mdogo kwangu?😅😅
 
Kuna mtu anaitwa MATOLA , ...hakuna mtu anamuongelea...kuna kazi alikuwa anaifanya pale SIMBA... ila ndo hivyo kuna watu hawana bahati ( sudi/ charistimatic)...
Alikuwa na mchango Gani.....??? Mbna walikuwa wanataka aondoke
 
Sijui watu wanataka Simba wacheze mpira gani. Watu wamejiuliza game plan ya Simba jana ilikuwaje? Yule kipa wa Vipers karibia avunjike kiuno kwa saves alizokuwa anafanya.

Mchezaji ambaye naweza sema alicheza chini ya kiwango ni Saidoo na Kanoute. Kanoute hana kawaida ya kucheza chini ya kiwango kwa hiyo itakuwa aliamka tu vibaya. Kimekuwa kilio changu cha muda mrefu kuwa Saidoo asianze game ila kilio changu bado hakijasikika. 90% ya movement zake anapoteza mipira au anaanguka. Inawezekanaje mchezaji mwenye mwili kama wake anakuwa dhaifu dhaifu vile. Anajichekeshachekesha tu hovyo.

Phiri alikuwa tishio sana kipindi cha kwanza ila viungo waliacha kumlisha mipira kwa hiyo alipotea kidogo kipindi fulani. Nilitabiri angetolewa na kweli ikawa hivyo ingawa aliyestahili kutoka mapema ni Saidoo.

Ukiacha hayo muhimu ni point 3. Hii ni timu ya tatu Simba inaifunga nje ndani msimu huu bila kuruhusu goli kutoka kwao.
Hakika .....shida saido current kapunguza attempt za kupiga mashut nje ya 18
 
Back
Top Bottom