biganana kwetu
New Member
- Feb 11, 2018
- 4
- 0
Nahitaji Refractometer Kwa ajili ya kupimia ubora wa asali.nipo dar
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari Mwl.RCT,ni site gani nayoweza kupata quality used laptop kwa bei nzuri?[emoji778]UTANGULIZI
Je Kuna bidhaa unataka kununua toka nje ya nchi kwa sababu hapa Tanzania umetafuta na umekosa kuipata?
Je kuna huduma unahitaji kulipiwa mtandaoni?
Kama jibu ni NDIO basi hii thread inakuhusu.
Thread hii ni maalumu kwa wanaohitaji kununua bidhaa yeyote toka nje ya nchi. Bidhaa ambazo
Hivyo thread hii itajikita katika nyanja kuu mbili:
- Hazipatikani hapa nchini au
- Hata ukipata ghalama yake huwa ni kubwa mara mbili zaidi, ukilinganisha na ghalama ya Kununua nje + Ghalama ya usafirishaji + Kodi
[emoji778]1. BUY4ME : Manunuzi ya bidhaa mtandaoni toka mataifa 15: ITALY, UAE, CANADA, UK, USA, JAPAN, FRANCE, CHINA, INDIA, GERMAN, MALAYSIA, SINGAPORE, SPAIN & SOUTH AFRICA. Huduma hii nitaiita BUY4ME.
(a) Kupitia huduma hii ya Buy4me Utaweza kununua bidhaa kutoka katika masoko* yaliyo bora yasiyouza na kusafirisha bidhaa nje ya nchi zao.
(b) Pia ununuzi wa bidhaa toka masoko* ambayo yanaweza tuma bidhaa nje ya nchi zao, kuja huku Tanzania (Africa)
*Masoko = Online shopping site
Jukumu langu ni (i) KUKUNUNULIA (ii) KUKUSAFIRISHIA (iii) KUKUFIKISHIA mahala ulipo pindi bidhaa yako ifikapo hapa nchini.
[emoji778]2. PAY4ME : Malipo ya dharula ya hapo kwa hapo kulipia huduma na bidhaa
Kutokana na kadi yako kuisha mda wake au kadi yako inashidwa kufanya miamala kwa wakati huo ambao unashida.
Yamkini upo safarini na unahitaji ufanyiwe malipo kwa haraka.
Na iwapo pia huna kabisa access na online payment system yeyote.
Huduma hii itajulikana kwa jina la PAY4ME .
Mfano:
Kulipiwa domain name, webhosting , licence keys kwa software au program yeyote uitakayo mtandaoni , Kulipiwa huduma au uanachma katika tovuti mbalimbali mfano Netflix au HBO n.k
[emoji778]UTARATIBU WA KUNUNUA BIDHAA - BUY4ME
Utafuata hizi hatua
1. Tafuta bidhaa unayoihitaji toka tovuti tofauti tofauti.
2. Chagua bidhaa husika unayohitaji katika tovuti uliyo chagua mfano kama ni ALIEXPRESS, SOUQ, AMAZON (.com, .in, .uk ) au EBAY (.in, .com, .uk)
3. Nipe link ya hiyo bidhaa unayohitaji na uliyochagua.
Utanipa link kupitia email au whatsapp au PM
4. Nitaikagua link husika na Nitakujulisha gharama kwa TSH inayotakiwa kulipwa.
5. Utafanya malipo kwa utaratibu wa malipo uliowekwa.
6. Ndani ya dakika 5 - 45 tangu ufanye malipo nitakuwa nimelipia bidhaa yako na kukupa ushahidi wa:
- Payment Invoice,
- Picha (Screen shot) ya Bidhaa yako baada ya malipo kufanyika.
- Uthibitisho wa email niliyopokea baada ya muamala kukamilika.
- Hatua hii nitahitaji email yako au namba ya whatsapp ili kukutumia hivi vielelezo.
7. Utasubiri ndani ya saa 24 – 72 ili kupata tracking number ya mzigo wako kwa mizigo yenye tracking number.
8. Mzigo wako utachukua kati ya siku 9 – 21 kukufikia mahala ulipo.
![]()
![]()
[emoji778]GHALAMA UTAKAZONILIPA
- Kwa huduma ya BUY4ME utanilipa kwa makubalino baina yako wewe na mimi kutegemea thamani ya mzigo wako. Kiwango utakacholipa ni kati ya USD $2.5(Minimum) hadi USD $50 (maximum)
- Kwa huduma ya PAY4ME hii utalipia kiasi cha USD $2.5 hadi USD $5 Tu.
- Viwango kwa TSH vitakokotolewa kulingana na EXCHANGE rate ya US dola kwa siku husika malipo yanafanyika.
[emoji778]MAKUNDI MAWILI YA TOVUTI MASOKO
[emoji778]KUNDI A – Wauzaji wanatuma moja kwa moja bidhaa kuja Tanzania (East Africa) -
Ambapo ghalama ya usafirishaji inajumuishwa wakati wa manunuzi ya bidhaa husika. (Napendekeza masoko ya kundi A yatumike Zaidi ili kupunguza ghalama.)
[emoji778]KUNDI B - Wauzaji wake hawatumi bidhaa kuja Africa, Nitawajibika kupokea mzigo wako katika nchi husika (viz UAE, USA, CHINA, JAPAN etl) .
Na mzigo ukishapokelewa ndipo unatumwa kuja Tanzania (Africa)
- Ambapo ghalama ya kutuma Mzigo Tanzania (Africa) itatokana na uzito wa mzigo. Gharama HAZIKADIRIWI kwa mujibu wa mita za ujazo (Volumetric Weight W*L*H) (Angalia kipengele cha ghalama ya usafirishaji hapo chini)
- Tracking number utapewa mpya ambapo utaweza ku_track mzigo wako ukiwa Njiani kuja TZ (Africa).
- Waweza kutrack mzigo kwa njia Mbili (a) Kwa kutumia mfumo wa SMS katika simu yako, au (b) kwa kutumia tovuti kwa njia ya simu au computer.
[emoji778]GHALAMA ZA USAFIRISHAJI MZIGO – TOKA MASOKO KUNDI B
1. Iwapo umenunua bidhaa kutoka katika soko la kundi A. Ghalama ya usafirishaji hulipwa wakati wa ununuzi.
Pia kwa baadhi ya masoko kwa bidhaa zote au baadhi ya bidhaa wauzaji, hutoa FREE SHIPPING, hivyo kunakuwa hakuna ghalama ya ziada baada ya ununuzi wa bidhaa yako.
2. Iwapo umenunua bidhaa toka soko kundi B – Ghalama ya kusafirishia hutegemea UZITO wa bidhaa husika katika KILO (Kg) au katika POUND (LB) na kiwango cha fedha hutokana na kila 0.5kg ya bidhaa yako. kwa huu utaratibu
[emoji778]Mfano:
a) 0.1 - 0.5kg Gharama ya kusafirisha ni USD 20.34
b) 0.6 – 1kg Ghalama ya kusafirisha ni 33.14 USD
c) 1.1kg – 1.5kg Gharama ya kusafirisha ni 43.94 USD
d) 1.6kg – 2kg Gharama ya kusafirisha ni 56.74 USD
Hivyo pindi ununuapo bidhaa kwenye Soko kundi B – Hakikisha unaangalia uzito halisi wa bidhaa yako. Ili kujua kiasi cha fedha kitakacho hitajika kusafirishia mzigo.
Na gharama hii ya usafirishaji italipwa Pindi mzigo uondokapo kwenye nchi husika kuja nchini Tanzania.
[emoji778]NB:
1. Gharama ya usafirishaji yaweza kulipwa ndani ya SIKU 1 hadi 5 Tangu upewe taarifa ya ghalama ya usafirishaji, kutoka nchi husika KUJA TANZANIA. ( Ni vyema ukalipa mapema).
2. Tracking number utakuwa nayo tayari hivyo utajua wazi mzigo wako umefika wapi au hatua ipi ya usafirishwaji.
[emoji778]KODI UTAKAYOLIPIA PINDI MZIGO UKIFIKA
[emoji778]NJIA YA MALIPO (KUTUMA FEDHA)
- Pindi ununuapo bidhaa toka nje kumbuka kuna swala la kodi pindi bidhaa ifikapo nchini. (Kuna baadhi ya bidhaa huwa hazina nakodi – Mamlaka husika ndio huainisha bidhaa zipi zisizotozwa kodi)
- Utawajibika kwa malipo yote yatakayohitajika na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa bidhaa uliyonunua na iwapo utatakiwa kuilipia kodi.
- Gharama ya kodi hujulikana baada ya kuwa mzigo umekaguliwa na maafisa ushuru wa forodha hapa nchini.
- Iwapo kutakuwa na charges zingine Toka kwa shipping agent baada ya mzigo kufika utajulishwa na utawajibika kulipia.
- Malipo yote utakayofanya utapewa stakabadhi husika.
Malipo yote yanapitia Benki, Chagua njia mojawapo kati ya hizi kufikisha fedha yako benki.
(a) Kwa kwenda benki na kuweka kiasi husika au
(b) Kwa kutumia Mobile Banking - kwa mtandao wa Tigo au VodaCom (kama ilivyoelekezwa hapa chini)
[emoji778]MALIPO YOTE NI KWA NJIA YA MPESA / TIGO PESA KWA HUU UTARATIBU
1. Piga *150*00# AU *150*01# (kwa Tigo PESA)
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa na 4 kwa Tigo Pesa
3. Mpesa Chagua 4. Weka namba ya kampuni au Chagua 3 kwa Tigo Pesa
4. Tafadhali weka namba ya kampuni No. 261122
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo. (Nitakupa namba hii Baada ya kuwasiliana nami)
6. Weka kiasi (mfano: 50,000/=)
7. Weka namba ya siri.
8. Bonyeza 1 kuthibitisha:
** (BAADA YA MUAMALA KUKAMILIKA, TUMA KWANGU UJUMBE UTAKAOPOKEA- KAMA UTHIBITISHO)
[emoji778]NJIA ZA MAWASILIANO
Wasiliana nami kwa moja ya hizi njia
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: 0717 54 57 62 au 0768 92 48 41 au 0784 496 856
2. Barua Pepe (Email): mw1rct @ outlook.com
3. Whatsapp: +255 784 496 856
4. Skype: mw1rct
5. Telegram: @mw1rct
[emoji778]MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram - Utajibiwa
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.
Iwapo unamazungumzo marefu na unahitaji kupigiwa simu niandikie kwenye ujumbe “CALL PAY4ME” au “CALL BUY4ME” na nitakupigia bila gharama yeyote.
IWAPO UNAWEKA LINK KWENYE HII THREAD TUMIA HUU UTARATIBU
View attachment 505857
[emoji815]BAADHI YA MAONI YA WADAU WA JF[emoji815]![]()
Mwalimu, nataka niagize samsung led flat screen 55" . sijajua bei yake na gharama zote zipoje, ikiwezekana unisaidie wewe maana nmeona umewasaidia wengi humu na hakuna utataTumia hizi link kufanya uchaguzi wa simu utakayohitaji
Code:1. https://www.ebay.com/rpp/samsung-galaxy 2. https://goo.gl/gW57dS
PICHAMwalimu, nataka niagize samsung led flat screen 55" . sijajua bei yake na gharama zote zipoje, ikiwezekana unisaidie wewe maana nmeona umewasaidia wengi humu na hakuna utata
https://www.amazon.com/Samsung-Electronics-UN55MU6300-55-Inch-Ultra/dp/B06XGJX3SH/ref=dp_ob_title_ce
kwa uzoefu wako, kodi wanaweza sema bei gani?PICHA
View attachment 720998
MODEL: UN55MU6300 55-Inch 4K Ultra HD Smart LED TV (2017 Model)
BEI: 2,845,134 (Manunuzi na Kuifikisha DSM )
KODI/ VAT: Itajulikana baada ya mzigo kufika nchini, Mamlaka husika watatupatia kiwango cha fedha cha kulipia
MUDA: Ndani ya siku 14 mzigo utakuwa nchini Toka USA
LINK
NJIA YA MALIPOCode:https://www.amazon.com/Samsung-Electronics-UN55MU6300-55-Inch-Ultra/dp/B06XGJX3SH/ref=dp_ob_title_ce
(a) Bank deposit au
(b) Mobile Banking
Nitakujulisha zaidi ukiwa tayari kufanya malipo.