Nunua daftari na peni leo uanze safari yako ya mafanikio

Nunua daftari na peni leo uanze safari yako ya mafanikio

Naja naja

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
747
Reaction score
1,454
Ukitaka kufanikiwa kimaisha anza kwa kununua daftari na peni.

Hakikisha kila siku kabla haujalala umeshapanga kesho yako ufanye nini na nini na matumizi gani muhimu uyafanye.
Nini ufanye ili uboreshe utendaji kazi wako, maslahi yako, elimu yako, biashara yako nk.

Kesho yake kabla muda wa kulala, angalia jambo lipi na lipi ulilolipanga jana yake umefanikiwa kulifanya na lipi haujafanikiwa kulifanya, matumizi yapi umeyafanya kwa siku nzima, je matumizi yote yalikuwa yana ulazima? Siku yako umeitumiaje??

Ukiishi hivi ndani ya mwezi tu utafika mbali sana kimafanikio na itakusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na utajua kuutumia muda wako vizuri.
 
Kitu ngumu na waTz hawatak kusikia ni Mambo ya Kunote, kupanga ratiba na kuzifuata, kusave na kufuata nidhamu ya hizi ratiba&saving ulizopanga.

Ni kweli mafanikio huja baada ya mipango na mikakati kufanyika Kama ilivyopangwa.

Hutopata muda wa kulalama kama utakuwa umefanya jambo lako ndani ya muda uliotakiwa uwe umefanya, hata kama kipato chako kitakuja tofauti na ulichotarajia, lkn unaweza kujipa moyo kuwa ulilifanya jambo hilo within the time planned.

Hakuna kitu kinauma kama uharibu ratiba na kuharibu kipato chako sabbu hukujari muda na ratiba.

Pia kuna matumaini makubwa sana pale ufanyapo jambo ndani ya ratiba kamili kama ilivyopangwa.

Kuna muda unaweza kumuona mtu anakula sana bata, tumia sana pesa, wew ukamnotice kama mfuja mali, kumbe mwenzako hiyo ni sehemu yake pia ya ratiba aliyojipangia baada ya kutimiza majukumu fulan, then anajipongeza, lkn kwa usiyejuwa utamfitini na kumuona muharibifu na mtu wa anasa.

Tujaribu kuyapangilia maisha yetu, hakika mafanikio tutayapata
 
Ukiwa na Pesa Huwezi waza huu Ujinga.. pia elewa kuna Matajiri hawajui kusoma na kuandika. Wanajua hesabu ya pesa tu.
Bado hujui kitu wew, hakuna tajiri lofa akaacha kupangilia maisha yake, jifunze kukaa na waliofanikiwa utajifunza vitu ambavyo huwez vipata kwa watu machoka mbaya.

Mtu aliyefanikiwa hafanyi Jambo kwa bahati mbaya, bali kila afanyalo lilishpita ktk kikao ndani ya akili yake,

ndiomaana utasikia kuna tajir bahir ama ambaye hatabiriki why?, Sabbu hawez fanya jambo kwa kukulupuka, akisema leo nakupa/nakusaidia ni kweli atakusaidia kulingana na ratiba zake, na akisema hakupi, aisee hata ulie machozi hupewii kitu.

Achen kukalili maisha aisee
 
Yani hapo utaumiza kichwa, especially ukiwa na pesa hufikirii kalamu na daftari.....labda wale wavaa suti na moka wanaweza.....
 
Ukiwa na Pesa Huwezi waza huu Ujinga.. pia elewa kuna Matajiri hawajui kusoma na kuandika. Wanajua hesabu ya pesa tu.

Umewahi kuwauliza hao wenye pesa walianza vipi na walifanyaje?

Huo huo unaouita ujinga unaweza kuwasaidia wengi sana wakabadilika.

Hata hivyo unaposema ukiwa na pesa hauwezi kuwaza huo ujinga, unarejea pesa kiasi gani?
 
Bro wangu alifanya sana kitu kama hii. Alikuwa anaandika mipango yake kwenye karatasi nyeupe then anabandika ukutani kwenye getto lake. Asee, alijaza ukuta bila kutekeleza mpango hata mmoja.
😀😀😀.Sasa huoni kwamba huyo bro wako alikuwa nimzembe,

Kuwa na ndoto nyingi bila utekelezaji ni sawa na bure !
 
Niloka plan kula bia nne dakika ya mwisho nikala mpk kumi
 
Back
Top Bottom