Nunua daftari na peni leo uanze safari yako ya mafanikio

Nunua daftari na peni leo uanze safari yako ya mafanikio

Ukitaka kufanikiwa kimaisha anza kwa kununua daftari na peni.

Hakikisha kila siku kabla haujalala umeshapanga kesho yako ufanye nini na nini na matumizi gani muhimu uyafanye.
Nini ufanye ili uboreshe utendaji kazi wako, maslahi yako, elimu yako, biashara yako nk.

Kesho yake kabla muda wa kulala, angalia jambo lipi na lipi ulilolipanga jana yake umefanikiwa kulifanya na lipi haujafanikiwa kulifanya, matumizi yapi umeyafanya kwa siku nzima, je matumizi yote yalikuwa yana ulazima? Siku yako umeitumiaje ??

Ukiishi hivi ndani ya mwezi tu utafika mbali sana kimafanikio na itakusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na utajua kuutumia muda wako vizuri.
Mmh mawazo na mbinu za kale hizi,siku hizi vitu vinawekwa kidigitari,kwenye cm,laptop,sio makaratasi
 
Kuna msemo "Mali bila daftari ..."

Hapo daftari laweza kuwa karatasi laptpop, nk.

Kupanga na kujitahidi kufuata mpango ni muhimu sana katika maisha.
 
Hasa kama kazi zako una watu uliowaajiri inabidi ufanye hivyo.

Maisha yangu sijawahi kuandika what to do hata nikijenga nyumba huwa siandiki nilichonunua maana huwa niko beneti na fundi.

Ukizoea kuandika siku moja mwambie mkeo nipe listi ya ile laki niliyokuachia asubuhi, utajua kwanini nchi inaongozwa na wao.
 
Ukitaka kufanikiwa kimaisha anza kwa kununua daftari na peni.

Hakikisha kila siku kabla haujalala umeshapanga kesho yako ufanye nini na nini na matumizi gani muhimu uyafanye.
Nini ufanye ili uboreshe utendaji kazi wako, maslahi yako, elimu yako, biashara yako nk.

Kesho yake kabla muda wa kulala, angalia jambo lipi na lipi ulilolipanga jana yake umefanikiwa kulifanya na lipi haujafanikiwa kulifanya, matumizi yapi umeyafanya kwa siku nzima, je matumizi yote yalikuwa yana ulazima? Siku yako umeitumiaje ??

Ukiishi hivi ndani ya mwezi tu utafika mbali sana kimafanikio na itakusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na utajua kuutumia muda wako vizuri.
Njaa ni mbaya sana imepelekea watu kama wewe kujitundika.
 
Acheni ubishi tafuteni/nunueni daftari na peni mfanikiwe.. mijitu ni mibishi banah
 
Ni wazo zuri Sana Kama mtu anacommitment na Mambo yake. ..wengine huwa Ni nguvu ya soda anaweza andika siku mbili tatu akaacha...suala la upangiliaji wa siku Ni tatizo wengi tunaamka siku itaenda mbele kwa mbele.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Maskini bana wanapenda sana kudanganyana fanya kaz mkuu mambo ya daftari na peni ni mbwembwe tu. Mwaka una sku 360’s utaishi miaka 50 utanunua madaftar magap kuandika malengo yako ya kla sku

Fanya kaz eshimu kipato ukipatacho panga mipango yako vzr tumia pesa uipataya kwa umakini fanya yale uliyopanga kufanya na pesa yako acha emergency zisizo za lazma acha matumizi yasiyo ya lazma punguza kutoa misaada

Mafanikio hayana formula relax
 
Haya mambo tuliyashafanya sana enzi za shule. Unaandaa ratiba ya kusoma lakini kuifata ilikuwa tatizo.
Now days kama unapesa utafanya mambo kwa wakati
 
Back
Top Bottom