Nunua gari Ndugu yangu. Aibu ndogo ndogo zinaepukika

Boss hata hayo maghorofa hujengwa kwa hatua leo una 8_10m unaweza anza na ukafikia huko unako pataka
Hakuna..

Kumbuka swala la Ujenzi linahitaji hela na umakini sana kuanzia ARDHI na eneo ilipo hiyo Ardhi.

Mil 8-10 kwa standard zangu mimi hiyo ni nusu au robo ya gharama za kunua ardhi achilia mbali ujenzi hapo.

Kama mtu unanunua kiwanja kwa mil 2 alaf umatak ujenge kwa mil 6 hiyo unaita nyumba au Banda la Mkaa?
 
Why are you not recommending hii kipenzi cha wengi "Tako la nyani" ...waweza toa elimu kdg?
 
UlaaniweπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€sio mimi,Mioyo ya watu.
Niliongeleshwa kama mtoto na jamaa yangu akiwa na Mkewe Jumapili.

Shem naye akawa ananipa maelekezo,unajuaaa magari mafuta shukia hapo tuπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Basi ikawa poa ni poa...nikajiuliza na kusema toka sasa nijitafakari.
Nikaweka azimio la WajapanπŸ˜€πŸ˜€
Nikakutana na mtu anauza gari na laptop ndaniπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€chuma ile inakimbia mbaya...ni Bwana mkubwa mmoja hivi...

Oya nikatia mibomba ileπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€chuma inaunguruma kama Nyati mwenye hasiraπŸ˜€πŸ˜€
 
Tunatofautiana staring point pia ww leo unaanza ujenzi hauna uwanja mwenzio mawazo ya kiwanja sio shida zake

Ukisema banda la mkaa unakosea sababu 90% ya wakazi wa dar na Tanzania kwa ujumla tunaishi mabandani
 
Kwa Dar kama unafanya kazi ya mshahara wa laki 5 basi angalau miliki ile Honda Today au Honda Click.

Jua la Dar lina viungo vyote ila ukiwa unazurura umekaa inapunguza machungu
🀣 umemaliza kila kitu…
Sasa kunaraia humu wanakwambia hela y Honda today ujengee nyumba.. ss hiyo n nyumba gani?
Labda kama ile ya wahadzabe 🀣
 
Huyu ni zwazwa yani mtu aanze kununua gari kabla ya nyumba!, sisi sio ndege ya kwamba tutaishi kwenye viota!..
Nyumba ni muhimu zaidi!.
au una maoni gani cocastic..?
Mimi nilianza kununua gari kabla ya kujenga. Inategemea na kipato chako. Nilinunua gari, then kiwanja, nikabadilisha gari mara 2, nikanunua kiwanja kingine na kanza kujenga. Sasa nipo kwangu. Na mwaka jana nimebadilisha gari.
 
Gari la m8 huku umepanga sio gari ni takataka na litakuzidishia ufukara tu kulihudumia.

Mtu huna pa kuishi unadema dema na wenye nyumba zao wakukodishie halafu unanunua gari la m8, m10 ni umasikini wa fikra.

Bora hata ungelipia kiwanja hiyo pesa ya kurekebisha gobogobo lako kila mwezi ukadunduliza ukajenga hilo banda ukaishi humo baada ya miaka kadhaa litapanda thamani.
 
Ikiunguruma pia Adrenaline inapanda.... sooo ni humu tuuu
 
S
Wengine tumeanza kununua gari then kujenga
 
Mimi nilianza kununua gari kabla ya kujenga. Inategemea na kipato chako. Nilinunua gari, then kiwanja, nikabadilisha gari mara 2, nikanunua kiwanja kingine na kanza kujenga. Sasa nipo kwangu. Na mwaka jana nimebadilisha gari.
Maisha hayafanani ukute mtu analipwa laki tano huyu kununua gari kwanza ni sawa nakujitakia kifafa cha maksudi!.. heri hiyo pesa ya gari aanzishe mradi ukianza kuingiza ndo anunue gari.. maana gari ni gharama likitumbukia tu mtaroni kinyenye kinaanza!
 
Mkuu, Mwanaume usitake mambo mepesi ujanani, mambo mepesi yanakuja ukiwa na miaka kuanzia 45 kwenda mbele hapo una nyumba yako standard. Hata ukivuta chuma used ikiharibika utapaki uwani kwako. Sio unanunua gari used mkweche linakufia hapo hapo mwenye nyumba anataka nyumba yake hujui utapaki wapi gobogobo lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…