Kindred Spirit
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 457
- 666
Nakubaliana nawe kuhusu kero na risks za kushare public transport kama vile usalama wa kiafya, kuibiwa, vurugu na kukoseana heshima. Hiyo ni kutokana na mifumo mibovu iliyoko nchini ambayo mamlaka husika zimeshindwa kusimamia kama wanavyofanya nchi za wenzetu. Nchi zilizoendelea wananchi wengi wanaopt usafiri wa umma kwa kuwa usalama na quality viko guaranteed.
Lakini sasa, hakuna sababu moja inayoweza kumfanya mtu anunue au asinunue gari. Lazima kupima faida na hasara zake. Na hapo ni kwa yule mwenye uwezo wa hata kupata huo mkopo wa gari. Wengine hawana hata uwezo wa kukopesheka.
Cha msingi kuzingatia ni kuwa, gari ni liability, itaendelea kukulia hela. Unaweza kuona hali ni shwari kama unajaza tu mafuta na service za kawaida, ila ikitokea uharibifu gari siyo rafiki yako kabisa.
Halafu simshauri mtu achukue gari used ya hiyo thamani uliyosuggest yaani milioni 6, unanunua tatizo hata kubwa zaidi na hutafurahia your first car experience. Kama unachukua gari agiza au nunua yard gari ambayo wewe ni second user, siyo third user. La uwe na uhakika anayeuza ana sababu nyingine za msingi, kwamba sababu siyo hiyo gari. Wengi tu wanaweza kuwa wanauza gari kwa sababu ya changamoto ya hiyo gari.
Having said so, naheshimu sana maamuzi ya mtu ya kutotaka kununua gari hadi afanikishe mipango yake mingine hasa kujenga nyumba, kusomesha, kusoma etc, it's perfectly fine and wise decision. Gari siyo kipimo cha maendeleo.