Nusu Fainali Azam Sports Federation Cup: Simba 4-1 Yanga uwanja wa Taifa Dar es salaam

Acha kabisa halafu home kwangu wote nguvu moja na wote walivaa jezi. Uwiiiii!! Ilibidi niwe kapole tu mana si kwa kelele lile.

Lait viongozi wa Yanga wangekuwa na akili kama zangu angefungashiwa virago akasepa mana anatudhalilisha sana ujue.
Kiukweli Anachofanya Morisson hata sisi kinatukera ila nyie bado mtamchekea.

Pole sana Simba nguvu moja
 
Hahahahaaa. Kama nawaona mtakavyokuwa mnatupigia hizo kelele.

Ila asiyekubali kushindwa si mshindani. Jana soka nimeliona.
Hapo tu ndo nnapokukubali mwanachi wewe... lakini wananchi wenzio huku nnapoishi mimi huku kijijini mwali kabule matombo huku, eti wanasema jana tumenunua mechi na yule mghanaley eti katumika jana!
 
Kiukweli Anachofanya Morisson hata sisi kinatukera ila nyie bado mtamchekea.

Pole sana Simba nguvu moja
Hata na mie naliona hilo kwani ni mara kadhaa anarudia michezo yake ya kijinga na mpaka sasa uongozi umemkalia kimya tu as if amefanya kitu kizuri.

Nishapoa Mtani.
 
Hongereni watani zangu nawaza tu vile namna leo mtakavyowahi kazini ili tu mkatutambie. πŸ˜€

aminas
Bill.

Mi naumwa ntaenda kesho. 😎

Yaani Jana Nilikua Nakutamni Nakutamni Ila Nilikua Bizee Na Furaha Ya Ushindi Wa Mwaka Jana.

Ila Mtani Poleni Sana Na Hongereni Sana Vyamchangani Vinawahusu.
 
Inahitaji uvumilivu wakati mwingine viongozi na benchi la ufundi wanafanya usajili kwa shinikizo la mashabiki timu bora haipatikani kwa usajili bali wachezaji kukaa pamoja na kuzoeana muda mrefu
 
Hapo tu ndo nnapokukubali mwanachi wewe... lakini wananchi wenzio huku nnapoishi mimi huku kijijini mwali kabule matombo huku, eti wanasema jana tumenunua mechi na yule mghanaley eti katumika jana!
Thanks! πŸ™πŸ™

Mechi ya jana Kocha tu ndo alikosea hesabu zake na mi ndo nitamlaumu kwa hili hayo mengine sijayapa nafasi Mtani.
 
Timu yetu haina ubovu wa kufungwa goli zote zile bana.

Nadhani kocha tu naye alichemsha kuwaanzisha kina Tshishimbi ambao hawana match fitness.
Hata wangekuwa wazima tungewafunga tu.

Nyie ni wazuri kwa Mbeya city na timu nyingine ndogo ila si kwa Simba.

Kwa sasa ni bahati tu ndiyo mnaweza kuipata dhidi yetu ila kwa uwezo ni vyema mkafahamu bado mpo chini sana kwetu mtani fanyeni usajili msijifiche kwenye kivuli cha majeruhi[emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…