Hizo tuhuma zako hazina uthibitisho wa moja kwa moja kuhusika na uchawi kama simba ilivyofanya SA waziwazi.
Ni wazi misimu ya hivi karibuni Yanga alikua bora zaidi yenu, hilo liko wazi.
Kichaka cha rank unachojifichia ni mafanikio ya misimu ile minne iliyopita. Ni kama Mazembe nae kwenye rank anaonekana ni giant lakini kwa sasa uwezo wake si kama ule wa zamani.
Ndivyo mpira ulivyo.
Na pia kwa mashabiki kunakua na maoni tofauti tofauti, hilo la kusema "ninyi mlisema hivi" ni kauli ya ujanjaujanja maana sio kweli kwamba Yanga/simba wote walisema hivyo kwa kauli moja.
Nimeshakuambia kwamba kwenye kila derby timu yenu huwa ina tabia ya kuingilia geti lisilo rasmi, na ule muda wa wachezaji kupeana mikono maxi huwa anawazunguka wachezaji wa simba akiwa kashika chupa mkononi, sasa hayo siyo matukio ya wazi au unaona ni mambo ya kawaida kwenye football
Ukiniambia kwamba hayo matukio siyo uthibitisho wa moja kwa moja kwamba ni uchawi, nami nitakuuliza na wewe una uhakika gani kama simba walichokifanya kule sa ni uchawi na si kitu kingine, na kama ni kupigwa faini walipigwa faini sababu ya kuharibu tu uwanja wa watu na siyo kisa walifanya uchawi
Halafu umekazania hilo la uchawi tu kana kwamba ni mimi ndiye ninayeamini hayo mambo, wakati hiyo ni mitazamo ya viongozi wenu wenye akili ndogo hizo kashfa nyingine za wazi hujaziona, au kisa tff na tplb wanawanyamazia kimya wanaogopa kuwashitaki caf na fifa sababu watawakwaza wakubwa wa nchi
Hizo rank ni za misimu minne ya hivi karibuni na siyo misimu minne iliyopita usijitoe ufahamu, simba imefika hapo kwa sababu ya kufanya vizuri kimataifa kwenye misimu minne ya hivi karibuni na si kabla ya hapo, halafu hao tp mazembe unaowasemea msimu juzi tu hapo walifika nusu fainali caf usijisahaulishe
Ni msimu jana tu ndio waliflop sababu walifungiwa na fifa kufanya usajili na walikuwa tayari wameshauza karibu top cream yao yote, wakalazimika kuchukua baadhi ya wachezaji toka kwenye academy yao wasio na uzoefu ndio maana waliishia makundi, ila haimaanishi kwamba ni timu mbovu eti kisa ninyi mmeifunga bado tp mazembe atabaki kuwa moja ya giants wa africa
Halafu ngoja nikupe mfano ahly mara ya mwisho kumfunga mamelodi ilikuwa mwaka 2021 baada ya hapo hadi hii leo tunavyoongea ahly hajawahi kumfunga tena mamelodi kwenye mechi zote zaidi ya nane walizokutana ni either draw au mamelodi ashinde, yani mamelodi yuko radhi afungwe na timu yoyote ila siyo ahly lakini mwisho wa siku ahly ndio anafanya vizuri zaidi kimataifa kuliko mamelodi kwahiyo hatuwezi kusema mamelodi ni bora kuliko ahly kwa kigezo hicho tu, kwa sababu pengine tutajuaje labda mamelodi akikutana na ahly huwa anakamia tu hachezi kwa uwezo wake halisi na hiyo ni sawa na ninyi mnavyoona kwamba tp mazembe ni wabovu kisa tu ninyi huwa mnawafunga
Na kwa kutumia mfano huo huo pia najaribu kusema kwamba yanga kuwafunga simba kuna sababu nyingi na si kwa sababu wamewazidi ubora ukiacha mbinu za nje ya uwanja sababu nyingine mojawapo inaweza kuwa hiyo niliyoisema hapo juu, kwamba pengine yanga wakikutana na simba wanakamia sana mechi kuliko wakikutana na timu nyingine ndio maana ninyi mko radhi kudondosha points kwa timu ndogo kama jkt na mbeya city ila siyo kwa simba, lakini simba ukiangalia msimu jana kwenye ligi hawajafungwa na timu yoyote zaidi ya yanga tu sababu simba uchezaji wake ni ule ule huwa hawachagui mechi za kukamia na hiyo ndio maana halisi ya timu bora