Uchaguzi 2020 Nyalandu kwa Interview hii umepoteza uhalali wa kumkabili Dkt. Magufuli kwenye uchaguzi wa Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Nyalandu kwa Interview hii umepoteza uhalali wa kumkabili Dkt. Magufuli kwenye uchaguzi wa Oktoba 2020

Halafu utasikia "... October tunamtoa ikulu..."
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kungine kilicho nisikitisha ni kuzisifu sana ndege za ATCL, hivi Nyalandu huu ujio wa ndege umesababisha mashirika mangapi ya ndege kufa? Nauli zimepanda maradufu, Deni la taifa limeonagezeka maradufu, badala ya magu kunyanyua kilimo anakimbilia midege, nyalandu jitafakari upya mzee?
 
Povu lote na la nini mtoa hoja!!?

Kugombea si kuhasimiana, na hakukatazi kuheshimiana kwa kutokana na utofauti wa umri, madaraka, na hadhi katika jamii. Usije ukaacha kumheshimu mchungaji/padre/ ama imamu wako kwa kisingizio chochote kile!
 
Ndiyo maana tunataka Tundu Lissu au Membe wasioweza kumpa heshima za Ubaba Magufuli mmoja wao amchallenge.
Nyie kweli bado mpo kwenye majaribio, hamko serious na hamkipendi Chama chenu na hamjui mnataka nini

Yaani, Membe yuleyule wa CCM maisha yake yote ya kisiasa kafanyia CCM uje kumweka upinzani agombee unategemea nini?

Hamjajifunza Kwa Edo siyo?

Membe ndg zake wengi wako CCM na si Chama kingine chochote

Na kingine usichokijua ni kwamba, Kaa utulie, Uchunguze, Kisha fikiria Kwa kina, mwisho wa siku utakuja kujua kwamba, Siku Baba wa Taifa alipoamua kupokea na kutia saini kwamba, nchi yetu inaingia kwenye ushindani wa Vyama vingi, ilikuwa ni bosheni Tu kuwaridhisha hao Mabeberu waone kuwa tayari kuna Vyama Vingi Tz

Hembu fikiria, Kwani Vyama pinzani haviwezi kuwa na mtu anayeweza kuitingisha CCM mpaka atoke CCM?

Na hata kama akitokea, itakuwa ni uchaguzi wa mhula mmoja tu, mf Dr Silaa, na Mzee Mlema

Na baada ya hapo tayari Chama hicho kitaingiliwa kijasusi na siasa za CCM

Na hata hivyo, binafs yangu, Naamini hata hao viongozi wa Vyama pinzani wanajua na wanauishi mfumo huo, watake wasitake

Taifa letu na siasa zetu, mfumo wake ni kama Putin na China ingawa Sisi kunadanganya toto, na hii yote Kwa sababu Taifa letu ni tegemezi sio kama nchi hizo nilizotaja, ngoja Tz ifikie kwenye levo ya kutotishiwa Kwa maneno uone kama hatukakuwa na siasa za mfumo wa nchi hizo waziwazi

Tuendeleeni kupiga mayowe, siku ziende, nchi hii kutawala mpinzani haitatokea,

Kwanza wananchi wake hawajui kuungana na viongozi wa upinzani kudai hicho wanachodhani ni uonevu.

Ni nchi moja ya maajabu ya Aina yake Duniani,

Fanya yako Ila usivunje Sheria, hakuna wa kukutetea, mwangalieni kijana wenu asiyejua kusoma nyakati, ndug Mdude, ataozea jela, kelele za mitandaoni zilimchochea ujinga, akakubali kununuliwa na ujinga wa mitandaoni akajikuta Hana mtetezi baada ya kudakwa

Kspige Kura, mchague umtakaye Kisha nenda zako Kwa amani ingawa maoni yako nayakubali Kwa asilimia zote
 
Nimesikiliza mahojiano baina ya Mtia nia wa kugombea uraisi wa Chadema ndugu Nyalandu na kituo cha redio cha wasafi.
Nyalandu ameulizwa swali kuhusu Twiga waliokuwa wakitoroshwa nje ya nchi kwa kupandishwa ndege.
Katika majibu yake Nyalandu anaonyesha kujibu huku akimrefer raisi Magufuli kama "Baba yetu".

Sikutegemea kusikia mgombea uraisi mmoja akimuita mgombea uraisi mwingine, wa chama kingine, tena wanaokaribiana umri kama "Baba"

Kauli hii ukiitafsiri kiundani, unaona wazi kuwa Nyalandu kamwe hawezi kuita sepetu ni sepetu pindi kama akiteuliwa kuwa mgombea, Kiufupi imemuonyesha Nyalandu kama mtu mwenye nidhamu ya woga, laini laini sana kuweza kupambana na rafu za Magufuli kwenye kampeni.

Lakini kitu kingine ni dhahiri Nyalandu kwa kauli hii ya kumuita mshindani wake "Baba" kamwe hatoweza kumshughulikia kwa matendo yake ya kuvunja sheria na katiba na maamuzi ambayo kayafanya nje ya utaratibu wa majukumu halali ya uraisi pindi akitwaa dola. Je ni nani anayeweza kumpeleka baba yake mahakamani?

Pengine mtu unaweza kusema kuwa Nyalandu alikuwa akijaribu kuwa muungwana au kufanya siasa za kistaarabu, Jivi siasa za kistaarabu ndo umuite rais aliyeko madarakani baba yako?, Kama unamheshimu kiasi cha kumuona kama baba yako kwa nini sasa uchukue fomu kumtoa madarakani?

Hizi tabia za wanasiasa kuleta mambo ya ubaba na umama katika kazi ndiyo mwanzo na wenyewe wakishika madaraka kutaka wapewe ufather au waonekana kama mababa ambao maamuzi yao hayapaswi kupingwa. Ndiyo maana nashangaa Mtia nia wa kugombea urais wa Chadema ndugu Nyalandu anamuona raisi Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi kama baba!

Hata kwenye chama cha Mapinduzi, Rais na mwenyekiti wao hawamuiti baba huwa wanamuita ndugu, Iweje leo Mgombea wa Chadema ampe heshima ya ubaba mtu ambaye hata chama chake hakijawahi kumuita hivyo?

Nyalandu kama unamuita Magufuli ni baba yetu, ya nini sasa wewe utake kumchallenge baba?

Au unaogopa Magufuli asifukue madudu yako ulipokuwa serikalini akakushughulikia?

Mtu anayepaswa kumchallenge Magufuli ni mtu shupavu, asiye na nidhamu ya woga, mtu asiye softsoft, mtu mwenye kumuona Magufuli kama rais na siyo baba yetu.

Kwa sasa sijaona mgombea mwenye ujasiri huo wa kutosha kabisa kabisa kama Tundu Lissu na Bernard Membe

Sitegemei kumsikia Lissu au Membe wakimuita Rais Magufuli kuwa ni baba yao, kufanya hivyo ni nidhamu ya woga, kujilegezalegeza mbele ya mgombea wa chama kingine.

Kunywa maji kwanza gadhabu ipoe halafu tukufundishe siasa inavyotendwa wewe Mfipa;

KWANZA
Wewe hauko fair kabisa kwani Mhe. Nyalandu kaongea mengi sana juu ya nchi na yeye kama Mgombea ni nini anacholenga kuboresha. Mfano kazungumzia

1. HAKUNA kiongozi ambaye ataingia madarakani na aamue kutupa kila kilichofanywa na mtangulizi wake hapa alizungumzia kuboresha zaidi shirika la Ndege la ATCL

2. Pia, kazungumzia utawala wa sheria katika Serikali atakayoiunda yeye.

Nk

Sasa wewe uchomoka na kamfupa tu umeacha nyama unakuja kutuambia kwamba yule ng'ombe kakonda sana na ushahidi ni huu mfupa kweli?

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
Kunywa maji kwanza gadhabu ipoe halafu tukufundishe siasa inavyotendwa wewe Mfipa;

KWANZA
Wewe hauko fair kabisa kwani Mhe. Nyalandu kaongea mengi sana juu ya nchi na yeye kama Mgombea ni nini anacholenga kuboresha. Mfano kazungumzia

1. HAKUNA kiongozi ambaye ataingia madarakani na aamue kutupa kila kilichofanywa na mtangulizi wake hapa alizungumzia kuboresha zaidi shirika la Ndege la ATCL

2. Pia, kazungumzia utawala wa sheria katika Serikali atakayoiunda yeye.

Nk

Sasa wewe uchomoka na kamfupa tu umeacha nyama unakuja kutuambia kwamba yule ng'ombe kakonda sana na ushahidi ni huu mfupa kweli?

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app

Kaonyesha usoft soft kwa mgombea wa CCM
Hupaswi kumuita mgombea mwenzako Baba.
 
Mbali binafsi kutoona tatizo kwa Magufuli kuitwa baba, ila Jamani lazima tukubali kuwa siasa ni 'science' haiitaji hisia peke yake ili kuweza kuimudu.

Lakini pia kusafia kwa baadhi ya mmb mazuri yaliyofanywa na Serikali iliyo madarakani si dhambi na ukifanya hvy wala haikuondolei sifa ya kuwa mpinzani. Imefika muda sasa tuwe realistic na kuacha kupinga tu kila Jambo.

Nyalandu kama mwanasiasa mbobevu na anaetaka kujipambanua kivinge tofauti na ilivyo mazoea ktk kuelekea uchaguzi mkuu, anajaribu kuzichanga karata zake vyema ili aweze kuwawin watu wengi na wenye milengo tofauti. Kuna muda katika mapambano si vibaya kubadilisha mbinu za kukabiliana na adui yako, na katika muktadha huu na Zama hizi ambazo Mambo yote ambayo wapinzani walikuwa wakiyapigia kelele kuwa yanafanywa ndivyo sivyo au yanafanywa si ktk kiwango cha kuridhisha, lkn Sasa yanafanywa kwa uzuri au kwa kiwango Cha kuridhisha ktk awamu hii ya JPM, Ni vyema atakaekuja kumchallange aje na approach ya tofauti kidogo.
 
Baba ambaye akili yake haina akili, hafai kuwa baba.
Nyarandu umeniangushasana..

#LISSURAIS2020
 
Mimi kwa maoni yangu hajakosea kumwita Magufuri Baba! Hizo ni siasa za kistaarabu.
 
You just don't get it!

The main point hapa siyo kwamba Nyalandu ameportray heshima kwa rais bali ameportray uogauoga kwa Magufuli, na uoga huzaa unafiki na unafiki. huzaa uharibifu katika nchi!

Hatuhitaji mtu muoga muoga kusimama kumchallenge Magufuli kwenye uchaguzi wa October 2020

Unaweza kuimagine Biden amuite Trump "our father Trump"?

Nakuhakikishia Lissu kamwe hawezi kusimama na kutoa heshima ya nidhamu ya uwoga kama hiyo ya kumuita Magufuli Baba!

Kauli ya Nyalandu is too timid, too lame, hypocritical. Na hizo siyo sifa zinazomfaa mtu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
LOOooo, hata kabla ya kwenda mbali tayari umekwishajionyesha mwenyewe msukumo wako ni nini?

Nilitaka kukupa 'benefit of the doubt', pamoja na kwamba naifahamu misimamo yako ilipo katika siasa za Tanzania; sasa tayari huna hata subira kuji'expose' tena?

Basi, tulimalize hili, kwa sababu hakuna jipya; ni mwendelezo wa yaleyale ya siku zote.
 
Huyu Nyalandu akafanye biashara ndiyo talent yake, na kama anataka siasa arudi CCM siasa za upinzani za nchi hii haziwezi kabisa. Huyu ni kama Lowassa tu wazee was mipango ya chini kwa chini lakini majukwaa ya kisiasa hawayawezi.
 
Back
Top Bottom