Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Nashangaa, sijui baba yake yeye na nani
Mimi Magufuli siyo baba yangu
Kwanza hata neno baba hujawahi kulitumia tangia uzaliwe, kwa maana baba mwenyewe siajabu hauna, ndo maana unaona ishu, ...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nashangaa, sijui baba yake yeye na nani
Mimi Magufuli siyo baba yangu
Ubabe una mwisho. Kaburini hakuna jeshi la polisiTundu Lisu akitua tu anatiwa mbaroni hadi upelelezi ukamilike!
Akikujibu nitagUlitaka ajibu vipi kuhusu twiga nasi tunajua ufipa ni karai la kufulia mafisadi!
Nyalandu ana mke mzuri sana acha awe na woga tuuuKama sio huruma ya Magufuli, Nyalandu angekuwa jela sasa hivi
Hahaha asipanick kifipa unataka achekelee kilumumba? HahahahaMissile of the Nation,
Hata Mbowe humwita Rais Magufuli baba. Ni heshima ya kawaida bwashee usipanic kifipa!
Nyie kweli bado mpo kwenye majaribio, hamko serious na hamkipendi Chama chenu na hamjui mnataka niniNdiyo maana tunataka Tundu Lissu au Membe wasioweza kumpa heshima za Ubaba Magufuli mmoja wao amchallenge.
Kunywa maji kwanza gadhabu ipoe halafu tukufundishe siasa inavyotendwa wewe Mfipa;Nimesikiliza mahojiano baina ya Mtia nia wa kugombea uraisi wa Chadema ndugu Nyalandu na kituo cha redio cha wasafi.
Nyalandu ameulizwa swali kuhusu Twiga waliokuwa wakitoroshwa nje ya nchi kwa kupandishwa ndege.
Katika majibu yake Nyalandu anaonyesha kujibu huku akimrefer raisi Magufuli kama "Baba yetu".
Sikutegemea kusikia mgombea uraisi mmoja akimuita mgombea uraisi mwingine, wa chama kingine, tena wanaokaribiana umri kama "Baba"
Kauli hii ukiitafsiri kiundani, unaona wazi kuwa Nyalandu kamwe hawezi kuita sepetu ni sepetu pindi kama akiteuliwa kuwa mgombea, Kiufupi imemuonyesha Nyalandu kama mtu mwenye nidhamu ya woga, laini laini sana kuweza kupambana na rafu za Magufuli kwenye kampeni.
Lakini kitu kingine ni dhahiri Nyalandu kwa kauli hii ya kumuita mshindani wake "Baba" kamwe hatoweza kumshughulikia kwa matendo yake ya kuvunja sheria na katiba na maamuzi ambayo kayafanya nje ya utaratibu wa majukumu halali ya uraisi pindi akitwaa dola. Je ni nani anayeweza kumpeleka baba yake mahakamani?
Pengine mtu unaweza kusema kuwa Nyalandu alikuwa akijaribu kuwa muungwana au kufanya siasa za kistaarabu, Jivi siasa za kistaarabu ndo umuite rais aliyeko madarakani baba yako?, Kama unamheshimu kiasi cha kumuona kama baba yako kwa nini sasa uchukue fomu kumtoa madarakani?
Hizi tabia za wanasiasa kuleta mambo ya ubaba na umama katika kazi ndiyo mwanzo na wenyewe wakishika madaraka kutaka wapewe ufather au waonekana kama mababa ambao maamuzi yao hayapaswi kupingwa. Ndiyo maana nashangaa Mtia nia wa kugombea urais wa Chadema ndugu Nyalandu anamuona raisi Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi kama baba!
Hata kwenye chama cha Mapinduzi, Rais na mwenyekiti wao hawamuiti baba huwa wanamuita ndugu, Iweje leo Mgombea wa Chadema ampe heshima ya ubaba mtu ambaye hata chama chake hakijawahi kumuita hivyo?
Nyalandu kama unamuita Magufuli ni baba yetu, ya nini sasa wewe utake kumchallenge baba?
Au unaogopa Magufuli asifukue madudu yako ulipokuwa serikalini akakushughulikia?
Mtu anayepaswa kumchallenge Magufuli ni mtu shupavu, asiye na nidhamu ya woga, mtu asiye softsoft, mtu mwenye kumuona Magufuli kama rais na siyo baba yetu.
Kwa sasa sijaona mgombea mwenye ujasiri huo wa kutosha kabisa kabisa kama Tundu Lissu na Bernard Membe
Sitegemei kumsikia Lissu au Membe wakimuita Rais Magufuli kuwa ni baba yao, kufanya hivyo ni nidhamu ya woga, kujilegezalegeza mbele ya mgombea wa chama kingine.
Kunywa maji kwanza gadhabu ipoe halafu tukufundishe siasa inavyotendwa wewe Mfipa;
KWANZA
Wewe hauko fair kabisa kwani Mhe. Nyalandu kaongea mengi sana juu ya nchi na yeye kama Mgombea ni nini anacholenga kuboresha. Mfano kazungumzia
1. HAKUNA kiongozi ambaye ataingia madarakani na aamue kutupa kila kilichofanywa na mtangulizi wake hapa alizungumzia kuboresha zaidi shirika la Ndege la ATCL
2. Pia, kazungumzia utawala wa sheria katika Serikali atakayoiunda yeye.
Nk
Sasa wewe uchomoka na kamfupa tu umeacha nyama unakuja kutuambia kwamba yule ng'ombe kakonda sana na ushahidi ni huu mfupa kweli?
Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
LOOooo, hata kabla ya kwenda mbali tayari umekwishajionyesha mwenyewe msukumo wako ni nini?You just don't get it!
The main point hapa siyo kwamba Nyalandu ameportray heshima kwa rais bali ameportray uogauoga kwa Magufuli, na uoga huzaa unafiki na unafiki. huzaa uharibifu katika nchi!
Hatuhitaji mtu muoga muoga kusimama kumchallenge Magufuli kwenye uchaguzi wa October 2020
Unaweza kuimagine Biden amuite Trump "our father Trump"?
Nakuhakikishia Lissu kamwe hawezi kusimama na kutoa heshima ya nidhamu ya uwoga kama hiyo ya kumuita Magufuli Baba!
Kauli ya Nyalandu is too timid, too lame, hypocritical. Na hizo siyo sifa zinazomfaa mtu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!