Nyalandu ulikuja CHADEMA kwa hiari umeondoka kwa hiari. Kaa kimya kutunza heshima yako

Ameandika kaka yangu Abdoulquarim Malisa, kada wa CCM wilaya ya Kinondoni.
______
Nyalandu unasema moja ya sababu iliyokuondoa Chadema ni kushangilia kifo cha JPM. Lakini tuliona Chadema na vyama vingine vikitoa salamu za pole na viongozi wake wakahudhuria mazishi. Je hao walioshangilia ulijuaje ni Chadema? Kwanini hukudhani ni ACT, CUF au CHAUMA? Au walipokua wakishangilia walionesha kadi za Chadema? Hovyo sana.

Juzi kwenye mkutano mkuu wa CCM ulisema watanzania wameishi bila furaha kwa miaka kadhaa. Na ukamuomba mama Samia aseme neno la faraja. Ulimaanisha watu walipoteza furaha kipindi cha JPM. Lakini leo unasema umesikitishwa na watu kushangilia kifo chake. Sasa hao walioshangilia si ndio umesema walinyimwa furaha? Kama kweli walinyimwa furaha na aliyewanyima kaondoka kwanini wasifurahi? Mbona unajichanganya Nyalandu?

Au umejishtukia kwamba juzi uliboronga uliposema Magufuli aliwanyima watu furaha, leo ukaona usawazishe kwa kusema umesikitishwa na Chadema kushangilia kifo chake. Acha unafiki wewe. Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.

Umesema wale watoto waliopata ajali Arusha ni JPM ndiye aliyetoa dhamana (Pesa) wakatibiwe Marekani (zaidi ya TZS 2Bil). Kama ni kweli mbona hukusema kipindi akiwa hai? Kwanini usubiri hadi afe ndipo useme? Mnafiki wewe.

Halafu huyu aliyewalipia matibabu watoto (tena bila kujitangaza) ndio umesema kwamba aliwanyima watanzania furaha? Acha hizi ngonjera aisee.

Wakati unaondoka CCM ulisema Lissu alishambuliwa na serikali, ukadai bunge limegeuka rubber stamp, ukalaani watu kutekwa na kupotea, ukasema CCM walikuchukia ulipomtembelea Lissu hospitali.

Sasa hebu tuambie hayo madai yamepatiwa majibu kabla ya kurudi? Je waliompiga risasi Lissu bado wapo serikalini? Je bunge limeacha kuwa rubber stamp? Je waliokua wakifanya matukio ya utekaji na kupoteza watu wamekamatwa? Je CCM imeacha kukuchukia kwa kumtembelea Lissu? Hebu jibu hizi hoja kwanza kabla ya kutengeneza majungu mapya.

Kipindi unaenda Chadema ulitoa Siri za CCM ili uaminiwe huko. Sasa umerudi unajifanya kutoa siri za Chadema ukidhani itakusaidia kuaminika tena. Lakini sisi tunajua huna MKIA. Kaa zizini utulie.!

GJ Malisa
 
Kama huo ndiyo udhaifu pekee wa chadema, sasa wewe una wasiwasi gani mpaka umzuie kuongea? Akitoka mtu ccm mnataka wawe na uhuru wa kusema, akitoka mtu chadema hamtaki waseme, huo uhuru unaenda wapi?
Huo nao ni udhaifu wa chadema.
Ningependa hio uhuru wa akina Nyalandu kwenda redio yoyote na kukosoa wapinzani bila bugudha na wapinzani wangekua nao.
Hebu fikiria watu mnaambiwa hakuna kufanya Siasa hadi wakati wa uchaguzi tu.sasa vyama vitapataje wanachama?
Kuna magazeti yalijaribu kuonesha kunga mikono hoja za wapinzani yakafungiwa.
 
Ameandika kaka yangu Abdoulquarim Malisa, kada wa CCM wilaya ya Kinondoni.
______
Nyalandu unasema moja ya sababu iliyokuondoa Chadema ni kushangilia kifo cha JPM. Lakini tuliona Chadema na vyama vingine vikitoa salamu za pole na viongozi wake wakahudhuria mazishi. Je hao walioshangilia ulijuaje ni Chadema? Kwanini hukudhani ni ACT, CUF au CHAUMA? Au walipokua wakishangilia walionesha kadi za Chadema? Hovyo sana.

Juzi kwenye mkutano mkuu wa CCM ulisema watanzania wameishi bila furaha kwa miaka kadhaa. Na ukamuomba mama Samia aseme neno la faraja. Ulimaanisha watu walipoteza furaha kipindi cha JPM. Lakini leo unasema umesikitishwa na watu kushangilia kifo chake. Sasa hao walioshangilia si ndio umesema walinyimwa furaha? Kama kweli walinyimwa furaha na aliyewanyima kaondoka kwanini wasifurahi? Mbona unajichanganya Nyalandu?

Au umejishtukia kwamba juzi uliboronga uliposema Magufuli aliwanyima watu furaha, leo ukaona usawazishe kwa kusema umesikitishwa na Chadema kushangilia kifo chake. Acha unafiki wewe. Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.

Umesema wale watoto waliopata ajali Arusha ni JPM ndiye aliyetoa dhamana (Pesa) wakatibiwe Marekani (zaidi ya TZS 2Bil). Kama ni kweli mbona hukusema kipindi akiwa hai? Kwanini usubiri hadi afe ndipo useme? Mnafiki wewe.

Halafu huyu aliyewalipia matibabu watoto (tena bila kujitangaza) ndio umesema kwamba aliwanyima watanzania furaha? Acha hizi ngonjera aisee.

Wakati unaondoka CCM ulisema Lissu alishambuliwa na serikali, ukadai bunge limegeuka rubber stamp, ukalaani watu kutekwa na kupotea, ukasema CCM walikuchukia ulipomtembelea Lissu hospitali.

Sasa hebu tuambie hayo madai yamepatiwa majibu kabla ya kurudi? Je waliompiga risasi Lissu bado wapo serikalini? Je bunge limeacha kuwa rubber stamp? Je waliokua wakifanya matukio ya utekaji na kupoteza watu wamekamatwa? Je CCM imeacha kukuchukia kwa kumtembelea Lissu? Hebu jibu hizi hoja kwanza kabla ya kutengeneza majungu mapya.

Kipindi unaenda Chadema ulitoa Siri za CCM ili uaminiwe huko. Sasa umerudi unajifanya kutoa siri za Chadema ukidhani itakusaidia kuaminika tena. Lakini sisi tunajua huna MKIA. Kaa zizini utulie.!

GJ Malisa

Aisee hoja nzito Sana hizo.
Sasa Hii ndio aibu niliyosema itamshushia heshima yake.
Sasa anaonekana njaa ndio zimemkimbiza Chadema.
Aisee wacha Chadema wajiite makamanda maana ukiwa legelege huweizi kuishia Chadema.
 
Na hiyo ndio ulikua sababu ya Mimi kumtahadharisha Kuwa atashusha heshima yake.atoke kimya,Chadema imeshindikana,mtu mwenye nguvu kuliko wote Tanzania alioshindwa Nyalandu ni sisimizi tu.
Aangalie sana siasa za kuchafuana zisije zikamrudia mwenyewe. Angenyamaza nadhani Chadema wange heshimu maamuzi yake, lakini akianzisha mambo ya kuchafuana asije akamsababishia maumivu mkewe Faraja Kota anayeheshimika na kupendwa na jamii kama mfano bora, Maana naye aweza kuchafuliwa na tope.
Siasa za kuchafuana hazijali nani anapata maumivu.
SHAURI YAKE
[/QUO
 
Mimi siungi mkono tabia ya kuzibana midomo, aachwe aseme udhaifu wote wa cdm ili atoe nafasi ya kujirekebisha kwenye mapungufu. Akizibwa midomo atakuwa anaitishia cdm kuwa nini siri zenu hivyo kaeni kimya la sivyo nitaziweka hadharani. Akisema ukweli ama uongo sisi ni watu wazima na tunaweza kupima huo ukweli wake.

Sawa kabisa Mkuu Tindo,
Pamoja na umahili wako wote lakini umeshindwa kutambua Kuwa Nyalandu hakua na nia njema ya kukosoa kwa lengo la kujenga,Nyalandu Yuko katoka mwendelezo wa kukosoa kwa kubomoa,angekua Ana nia njema angekosoa akiwa ndani,hata kama anondoka,amekaa kimya siku zote hakusema nakuja kusema siku amepokelewa chama kingine.

Hata hovyo Mimi sikumfunga mdomo,Bali ninemtahadhalisha Kuwa atashusha heshima yake.
Ndadhani mwenyewe umeona anavyojichanganya na watu wameanza kumjibu,mwisho wa siku anaonekana kuwa njaa imemkimbiza Chadema na zaidi alimkimbia Jiwe.
 
Katika muktadha wa uhuru wa kutoa maoni Nyalandu yupo sahihi.......CHADEMA wanatakiwa kukomaa kisiasa kwa kustahimili hoja na mijadala inayokinzana na utashi wao.........Hata Sumaye alipoondoka CCM aliinanga CCM hadharani na hata Lowasa vivo hivyo.....hivyo si jambo jipya kwa wanasiasa wetu.......
 
Sawa kabisa Mkuu Tindo,
Pamoja na umahili wako wote lakini umeshindwa kutambua Kuwa Nyalandu hakua na nia njema ya kukosoa kwa lengo la kujenga,Nyalandu Yuko katoka mwendelezo wa kukosoa kwa kubomoa,angekua Ana nia njema angekosoa akiwa ndani,hata kama anondoka,amekaa kimya siku zote hakusema nakuja kusema siku amepokelewa chama kingine.

Hata hovyo Mimi sikumfunga mdomo,Bali ninemtahadhalisha Kuwa atashusha heshima yake.
Ndadhani mwenyewe umeona anavyojichanganya na watu wameanza kumjibu,mwisho wa siku anaonekana kuwa njaa imemkimbiza Chadema na zaidi alimkimbia Jiwe.

Ndio maana nilitaka aongee ili apuuzwe, vinginevyo angebaki kutishia kuwa ana siri za cdm kumbe hana lolote. Huoni sasa ameongea ili kuwaimpress ccm kwa kutaka kuichafua cdm, lakini kaishia kudhalilika?
 
Nyalandu ulikuja vizuri take vizuri.
Kama kuna mapungufu waambie viongozi wa CHADEMA watayafanyia kazi, lakini kuongea na redio utashusha heshima yako.
Kwa kukusaidia tu.
Kuna nguli walitoka CHADEMA sio wewe mpita njia usie na msimamo,mtu laini kabisa.

Alitoka Zitto, huyu ni nguli wa Siasa za Upinzani na aliijenga Chadema.

Alitoka Wilbroad Sliaa huyu alikuwa nguli wa siasa za Upinzani na aliijenga CHADEMA,

Nguli wengine Ni
Kitila
Arfi
Mwigamba.

Vitoto vya nguli
Waitara
Shonza
Mwampamba
Mchage.
N.k

Wote hao waliijua CHADEMA nje ndani,wewe Ni mpita njia tu.
Ulitamani kuwa Mwenyekiti lakini ulikwama.

Na bahati nzuri wageni Kama wewe huwa mnaangaliwa kwa macho makini.

Udhaifu wa CHADEMA ni mmoja tu, nao ndio udhaifu mkubwa kuliko udhaifu wowote ule.

Udhaifu wa CHADEMA Ni kunyimwa Uhuru wa kikatiba wa kufanya Siasa.

Hao CCM unaowaona hawana udhaifu Ni kwa sababu wameshika dola,leo CCM wakiondolewa madarakani litabaki Jina tu.

Kama unabisha waulize Wakenya KANU iko wapi?
Huwezi kumuita Nyalandu mpita njia na hali alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kanda ya Kati. Ukiendelea hivi hata siku Mbowe anatoka Chadema utamwita mpita njia
 
Back
Top Bottom