Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siku moja babu yangu alinisimulia hadithi hadithi ambayo mpaka leo naitafakari.
Babu yangu alinisumulia umuhimu wa mtoto wakiume ktk familia na kwa nini kila alipo kuwa akimuagiza mama alimwambia nenda na Yusuph.
Historia ya kijiji chetu kina manyani wengi na sio kwamba niwengi ila niwakorofi wameumiza sana watu na wamejeruhi sana wanawake kiasi wapo walio poteza maisha kwa kichapo cha manyani.
Nyani hawa kwa ukorofi wao hata nyumbani wakati mwingine wakijuwa yupo mwanamke basi watakuja nakufanya fujo na kujeruhi watu ila ajabu nimoja pakiwa na mwanaume hata kama mtoto yatakaa mbali na nyumba yakiamini kuna ulinzi.
Hii siri ilinifanya kukaa nakumuliza Babu yangu siri yakwanini alipenda nimsindikize mam na dada zangu wakati mwingine nikitamani kwenda mtoko naye aliniambia baki na mam ulinde nyumba.
Babu akavuta kiko chake nakuanza kunisimulia. Mjukuu wangu mtoto wakiume ni lulu hata akiwa mjinga anabaki kuwa mlinzi wa familia. Mtoto wakiume ameumbwa kwa utisho wakimungu na ndio maana mjukuu wangu napenda uwasindikize ndugu zako au ubaki nyumbani kulinda nyumba. Kweli ni mdogo ila kama beberu anavyo toa harufu maadui wabaya wakijuwa yupo mwanamme huwogopa kuitisha familia au kuidhuru.
Unaona kovu la jicho la mama yako ninyani walimshambulia akiwa anatafuta kuni akiwa peke yake hana kiongozi mtoto wakiume ila kama sio ukaidi asingekuwa chongo. Siku hiyo alienda porini asubuh na nikamshauri muende wote akakataa nahayo ndio madhara yake na toka siku hiyo anaenda na wewe au mm kuepuka madhara aliyapata.
Mjukuu wangu nitafurahi kama utakumbuka mwanamke akiendaporini basi aende na mtoto wskiume kuepusha hasara ataipata kwa kwenda mwenyewe. Nayni hamuheshim mwanamke hata akiwa na silaha ila anamuheshim mtoto mdogo wakiume akimfukuza kwa kijiti shiiii shii... na atakimbia...
Nyani ametuzidi maarifa na ndio maana Mungu akasema watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa. Basi na kwakuwa mmenikataa na Mimi nimewakata.
Mfumo dume uliokomaa kichwani kwako na mifano isiyo na uhalisia.....
Wewe MISOGYNYIST unatesekea kutokea wapi ?!!
Taifa limejaa think tanks wanaoona kuwa nchi iko vyema chini ya hao unaowabeza na kuwakebehi.....
#Ni yuleyule pilot wetu superwoman!