Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

Ni kitu/vitu gani ambacho ukipewa uwezo, power na kuwezeshwa ukaambiwa uwafanyie wananchi/raia wa kawaida, utawafanyia.?
 

I appreciate you man.
 
Je unaamini katika kusamehe.? If yes, kosa la kuchepuka unaweza samehe.? if no, huwa unajicontrol/act vipi unapokutana na mtu ambaye hujamsamehe.?

Je hasira zimeshawahi kufanya jambo ambalo ulikuja lijutia baadae.? If yes, Jambo gani.?
 
Nimeona sehemu katika post zilizopita kuwa hutotaka kuajiriwa tena, upo radhi uwe hata dereva wa Uber.

Je Huko ulipo madereva wa uber ndo wenye kazi zinazodharaulika.? Ama udereva wa uber ndo kazi yenye ujira mdogo kuliko zote.?

Hapana.

Marekani kazi ni kazi tu.

Sijawahi kuona kazi halali inayodharaulika Marekani.

Nimetaja Uber katika muktadha wa majadiliano na Watanzania ambao kuna baadhi ya kazi huwa wanazidharau.
 
Ni jambo gani ambalo ungependa kabla hujaondoka duniani uwe umelikamilisha.?

Je kuna legacy yoyote ambayo ungependa kuiacha.? If yes, Ipi.?
 
Wanaume wengi siku ya kwanza kutongoza huwa inakuwaga na kizungumkuti, kuna wengine hufikia hata kuandaa manual na kukariri verses za kutongozea, je Siku yako ya kwanza kutongoza kwako ilikuwaje.? Je ulimpata uliyemtongoza.? Ama ulicheza fyongo na kutoa mpira nje.?
 
NN...

Unaamini uwepo wa Mungu..?
Kama Jibu"Yes"kwanini,

Na kama Jibu "No" kwanini,
Kama yes/no haupo kwa nini,

Unamtazamo gani na maoni gani katika Nchi za bara la afrika pamoja na wingi wa rasimali bado hali ya maisha ya watu wake imekuwa mbaya ukilinganisha na mabara mengine!


Je! kunautofauti wowote uliouona Kati ya Elimu yetu na U.S.A...?

Ushawahi kujiunga/upo katika forums tofauti tofauti Mfano(Nairaland forums-Nigeria)..? kama Ndio kunautofauti gani..?

Yapi maoni yako katika lugha hapa Tanzania,Kiswahili kitumike katika ufundishaji chekechea mpaka chuokikuu au kisitumike...?

Mwisho,kwa Mtazamo wako Taifa la Tanzania Mambo gani yanatukwamisha na Mambo gani yafanyike ili kulivusha Taifa katika uchumi wa Juu zaiidi (number one Africa).

Shukran!!
 
Nahisi harufu ya mtu kutaka kudandia PAPUCHI za miteremkoo ya humu Jf...

Watu wana mbinuu[emoji125] [emoji125]
Hizo papuchi za mteremko zinapatikana Kona ipi humu jf? Nachojua wanawake wa humu graduated [emoji310] rich nigga wife training.....
 
Members wengi unajua wana wivu na wewe kwa sababu moja kubwa unaporingishia(USA baby yako ha ha haaaaa nahisi ndivyo waonavyo)

My gal Coco...nafurahi kukuona hapa. Ila mbona umechelewa hivyo? Au ulikuwa unawashughulikia Chadema kule siasani?πŸ˜€

na pia unatokea kuwa kama Nyani Ngabu mwenye nyota ya kuonewa wivu kwa ulivyo au na yako kutokana na maandishi.

Kwa kweli hata sijui tatizo lao ni nini hasa. Wana roho za kutu tu hao. Na huenda hawana furaha maishani mwao.

Je katika maisha yako upo hivyo, yaani unakutana na haya ya eatu kukuona kama unajisikia, unaringa na kutamani maisha yako?

Huku uraiani sijawahi kukutana na huo ujinga ujinga. Hiyo ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kunisemea mbovu usoni halafu akabaki salama. Mtu akiniletea ujinga nampa mangumi tu.

Sasa huku kwenye mtandao yeyote anaweza kusema chochote na kwa yeyote yule pasipo consequences zozote zile dhidi yake zaidi ya labda kupewa ban.

Nadhani, hata kimuonekano tu ninakuwa nina command respect flani hivi ambayo husababisha watu kutokunijaribu kwa sababu wanaweza kuisoma kirahisi lugha yangu ya mwili kwamba mimi sijaribiwi.

Kwa hiyo labda huwa wakiniona wanabaki tu kuugulia kimya kimya na kunisema bila ya mimi kusikia.

Je unajiwekaje na watu kama hao, najua huwa kuna wengine wanaweza kutaka kujaribu kukushusha kwa matendo au maneno kizaidi?

Yaani watu kama hao hawana nafasi kabisa hata ile ya kunisogelea tu. Nikibaini mtu huyu ni mzandiki na sabasi namfungia vioo fasta haraka upesi sana.
 
Mkuu Stunter interview ya kibabe sana....Safi sana..

NN Una majuto yeyote katika maisha yako???
Umewahi kutoka na msichana yeyote humu??..Inakuchukua muda/vitu gani kuweza kumuamini mtu humu Jf kabla ukajiexpose kwake
 
Je unaamini katika kusamehe.? If yes, kosa la kuchepuka unaweza samehe.?

Kuchepuka kwangu halisameheki.

if no, huwa unajicontrol/act vipi unapokutana na mtu ambaye hujamsamehe.?

Nampuuza tu.

Je hasira zimeshawahi kufanya jambo ambalo ulikuja lijutia baadae.? If yes, Jambo gani.?

Ndiyo.

Niliichomoa pete ya ndoa nikaitupa kichakani.

Halafu eti kesho yake nikaenda kuitafuta tena.

That was stupid and childish of me.
 

Mara yangu ya kwanza nadhani attraction ilikuwa mutual na wote tulisomana tu lugha za mwili tukaelewa kinachoendelea.

Hakukuwa na haja ya maneno mengi yaliyo matupu.

Wewe haijawahi kukutokea hiyo? Kwamba unamtazama mchuchu na yeye anakutazama na mwishowe mnajikuta mko wapenzi bila hata kujua nani alimwanza nani kumtongoza?
 

Nipo nilikuwa nasoma nasubiri nafasi ya kuongezea.

Wow nimependa ulivyo. Ndio maana unakimbiza totoz za humu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Tuambie juu ya social life yako ikoje..
Unapendelea kinywaji gani? unavuta chochote? unaenda night clubs sana au bar kulala kabla ya midnight? Unapenda miziki aina gani?

Huko unapenda kuwa na watu wa mataifa gani kizaidi?
Je unahudhuria shughuli za watanzania au hata kutembeleana?
Umesema siku hizi maisha ya kujipikia kizaidi, je unajua kupiga vyakula gani? Pia ugali na uji unajua?
 

Hahahaa, ishawahi nitokea kwa mchuchu mmoja hivi. Ila nilishatoa maboko mengi sana wakati najifunza kutongoza enzi hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…