Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

Nipo nilikuwa nasoma nasubiri nafasi ya kuongezea.

Wow nimependa ulivyo. Ndio maana unakimbiza totoz za humu 😀😀😀

Tuambie juu ya social life yako ikoje..
Unapendelea kinywaji gani? unavuta chochote? unaenda night clubs sana au bar kulala kabla ya midnight? Unapenda miziki aina gani?

Huko unapenda kuwa na watu wa mataifa gani kizaidi?
Je unahudhuria shughuli za watanzania au hata kutembeleana?
Umesema siku hizi maisha ya kujipikia kizaidi, je unajua kupiga vyakula gani? Pia ugali na uji unajua?

Haya cocochenel pokea kijiti cha maswali. Ngoja wengine tukalale.

Nyaningabu, thanks for your time.
 
NN...

Unaamini uwepo wa Mungu..?
Kama Jibu"Yes"kwanini,

Na kama Jibu "No" kwanini,
Kama yes/no haupo kwa nini,

Mimi siamini uwepo wa mungu na pia sikani uwepo wake.

Hiyo ni kwa sababu bado sijaona ushahidi wowote ule wa kutosha na unaoniridhisha kwamba kweli yupo au hayupo.

Hivyo bado nasubiri kuuona huo ushahidi.

Unamtazamo gani na maoni gani katika Nchi za bara la afrika pamoja na wingi wa rasimali bado hali ya maisha ya watu wake imekuwa mbaya ukilinganisha na mabara mengine!

Dah!

Hilo ni suala pana sana kwa kweli.

Bila kwenda ndani sana, binafsi naona sisi wenyewe Waafrika ndiyo tatizo. Tuna matatizo.

Je! kunautofauti wowote uliouona Kati ya Elimu yetu na U.S.A...?

Sana tu na ni tofauti kubwa sana.

Mpaka leo nashukuru sana kuweza kupata fursa ya kusomea Marekani. Wigo wangu umepanuka sana.

Ushawahi kujiunga/upo katika forums tofauti tofauti Mfano(Nairaland forums-Nigeria)..? kama Ndio kunautofauti gani..?

Sijawahi kabisa.

Yapi maoni yako katika lugha hapa Tanzania,Kiswahili kitumike katika ufundishaji chekechea mpaka chuokikuu au kisitumike...?

Mimi ningependa kitumike katika kufundishia kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Kiswahili ni lugha nzuri sana. Sielewi kwa nini sisi waongeaji wake hatukienzi inavyopaswa.

Ningependa pia kitumike mahakamani.

Hebu fikiria, eti sheria ni zetu wenyewe lakini huwa zinaandikwa kwa lugha ya kigeni!

Hivi unadhani huko Ureno sheria zao na mahakama zao zinatumia lugha ya Kifaransa au ya Kichaga?

Mwisho,kwa Mtazamo wako Taifa la Tanzania Mambo gani yanatukwamisha na Mambo gani yafanyike ili kulivusha Taifa katika uchumi wa Juu zaiidi (number one Africa).

Huu nao ni mjadala mpana sana.

Ila sababu zote nikizijumlisha narudi kulekule kwa sisi wenyewe wananchi ndi tatizo kuu.[/quote]
 
Aaaah, nilisahau. Swali la mwisho toka kwangu.

Huwa unatoaga zawadi(iwe ya pongezi, admiration, shukrani.?) if yes, ni memba gani wa hapa JF ungependa kuwapatia zawadi.? Taja wa kike mmoja, na wa kiume mmoja.
 
NN Una majuto yeyote katika maisha yako???

Kwenye maisha yangu sina kabisa muda wala nafasi ya kuruhusu majuto.

Haya maisha ni mafupi mno kuruhusu majuto.

Ikitokea kuna mahala nimekosea basi najifunza, najirekebisha, maisha yanasonga.

So muda wa kujuta sina kabisa.

Umewahi kutoka na msichana yeyote humu??

Ndiyo, nimewahi.

..Inakuchukua muda/vitu gani kuweza kumuamini mtu humu Jf kabla ukajiexpose kwake

Hakuna muda wowote ule ulio maalumu. Inategemea zaidi na wewe mwenyewe unajisikiaje na huyo mtu.

Muhimu ni kuwa mjanja tu. Ujanja gani? Hilo siwezi kusema...ni siri yangu.
 
Naona umeulizwa maswali mengi na umejibu Vema.

Tafadhali tuambie;
Ungelipenda tukuulize swali gani na jibu lake lingekuwa lipi?.
 
Nipo nilikuwa nasoma nasubiri nafasi ya kuongezea.

Wow nimependa ulivyo. Ndio maana unakimbiza totoz za humu 😀😀😀

Hahahaa sawasawa.

Tuambie juu ya social life yako ikoje..
Unapendelea kinywaji gani? unavuta chochote? unaenda night clubs sana au bar kulala kabla ya midnight? Unapenda miziki aina gani?

Mimi ni homebody. Napenda sana kukaa nyumbani. Nikitoka labda naenda gym kupasha misuli halafu narudi zangu nyumbani.

Napendelea zaidi kunywa lemonade.

Kwenye vile vinywaji vya watu wazima napendelea Heineken na viroba vile vya Konyagi.

Sivuti kabisa. Si bangi, si sigara, si crack cocaine.

Mambo ya klabu nilishaachana nayo zamani sana. Hata baa siendagi. Napendelea zaidi kunywa nyumbani. Na hata nikinywa si kunywa ile ya kilevi mbwa.

Nalala muda wowote tu ule. Hata mchana huwa nalala. Siku zingine nalala asubuhi. Ndo raha ya kuishi kwako hiyo. Kwa mama na baba huwezi kulala na kuamka muda wowote utakao wewe. Ukipitiliza wanakuja kukugongea uamke😀.

Ndo maana napenda kuishi kwangu.

Taste yangu ya muziki ni eclectic. Napenda muziki wa aina nyingi ili mradi masikioni mwangu uwe unasikika vizuri.

Napenda nyimbo za Marvin Gaye, Mariah Carey, Jokha Kassim, Mariam Khamis, Ali Kiba, Future, Gucci Mane, Justin Bieber, Shania Twain, Remmy Ongala, na kadhalika.

Huko unapenda kuwa na watu wa mataifa gani kizaidi?

Napenda kuwa na watu wa aina zote. Wabongo, Waghana, Wanaija, Wajamaica, Wazungu, Wahindi, Waarabu, Wakorea, Walatino...sina kabisa ubaguzi.

Ili mradi mtu awe poa tu [na msafi...sipendi harufu za vikwapa]...sina tatizo naye kabisa.

Je unahudhuria shughuli za watanzania au hata kutembeleana?

Hapana kwa kweli.

Nina muda sana sijahudhuria shughuli za Watanzania.

Ninaotembeleana nao ni wachache sana. Hawazidi wawili.

Umesema siku hizi maisha ya kujipikia kizaidi, je unajua kupiga vyakula gani?

Najua kupika vyakula vingi. Kwa mfano leo nimepika rice noodles zenye binzari. Ngoja baadaye ntaweka picha uone.

Huwa napika wali, maharage ya nazi, makande, mbuzi choma, kuku choma, maini rosti, mchicha, biryani la kuku, mayai ya kukaanga kama jicho la ng'ombe, omelette, maandazi, vitumbua, na vinginevyo.

Pia ugali na uji unajua?

Ugali siupendi [ajabu kwa sababu mimi ni ngosha] na kwa sababu siupendi hata kujifunza sijataka.

Uji nilikuwa najua lakini sijaupika siku nyingi sana hadi nadhani nitakuwa nishasahau.
 
Ni ubora gani unauona ktk awamu ya tano tofauti na awamu zote zilizo pita za uongozi wa juu wa nchi yetu ya Tanzania?

Angali bado ni raia halali mwenye uraia wa nchi moja Tz( kama kweli). Unashirikije ktk prosperity ya nchi yako Tz?

Ni taasisi ipi ya kiserikali au mfumo gani was kiserikali unaamini unatakiwa reform ya lazima na haraka hapa Tz?

Ulisema ulisoma secondary, kama ulisoma Tz unaionaje elimu ya public schools kipindi unasoma na kipindi cha sasa ?
Ni jambo gani la lazima ambalo ukikutana ungependa umshauri/ kumuomba raisi kuhusu nchi na ujumla wake?

Umekuwa big fan wa lugha ya kingereza hasa unakiandika kwa ufasaha. Je unahisi ni kusoma kama somo, au lugha ya kusomea na kusomeshwa au kutokana na matumizi ya kila siku ughaibuni?

Unawezaje kuzungumzia brain drainage inayofanyika ktk nchi yetu kupitia shule binafsi hasa za kimataifa. Ambazo haziwaandai next generation kufit ktk mazingira ya Tz bali yale ya ughaibuni?

Natanguliza shukrani
 
NN
I'm interested in knowing your tribe,

My intelligent guess is Pare,
Prove me wrong brother kaka!
 
Kuna mtu ameuliza kuhusu kabila lako hapo juu nadhani si kwa nia mbaya.
Mi nikuulize tofauti kidogo kwa nia njema pia.

Kumekuwa na hali iliyoanza kujitokeza hivi karibuni kuwa watu wanaodhaniwa na wengine kubainika kuwa wanayoka mkoa mmoja, jamii rafiki na raisi kuanza kutetea kingozi yyte wa kiserikali anayetoka ktk mazingira
 
Ushaona wapi wewe Mercedes Benz kuwa teksi?.
Kweli. Njoo Uswisi pia Benzs na Beamers kuwa Taxi ni kawaida tu. Tena hapa naongelea S class na 7 series. Ila kumi ni Ferrari kuwemo kwenye pool ya a car sharing system iitwayo Mobility.
 
Mimi siamini uwepo wa mungu na pia sikani uwepo wake.

Hiyo ni kwa sababu bado sijaona ushahidi wowote ule wa kutosha na unaoniridhisha kwamba kweli yupo au hayupo.

Hivyo bado nasubiri kuuona huo ushahidi.



Dah!

Hilo ni suala pana sana kwa kweli.

Bila kwenda ndani sana, binafsi naona sisi wenyewe Waafrika ndiyo tatizo. Tuna matatizo.



Sana tu na ni tofauti kubwa sana.

Mpaka leo nashukuru sana kuweza kupata fursa ya kusomea Marekani. Wigo wangu umepanuka sana.



Sijawahi kabisa.



Mimi ningependa kitumike katika kufundishia kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Kiswahili ni lugha nzuri sana. Sielewi kwa nini sisi waongeaji wake hatukienzi inavyopaswa.

Ningependa pia kitumike mahakamani.

Hebu fikiria, eti sheria ni zetu wenyewe lakini huwa zinaandikwa kwa lugha ya kigeni!

Hivi unadhani huko Ureno sheria zao na mahakama zao zinatumia lugha ya Kifaransa au ya Kichaga?



Huu nao ni mjadala mpana sana.

Ila sababu zote nikizijumlisha narudi kulekule kwa sisi wenyewe wananchi ndi tatizo kuu.
[/QUOTE]
Shukran Kwa majibu yako!!

Moja ya watu niliopata kupitia michango yako na nilifurahishwa haswa katika uzi wa 2009 "why I am not a Christian by Bertrand Russell" ulioletwa na Bluray na
"Upi ukweli kuhusu kambona" 2007 huku mkiburudishana na Mwafrika wa kike.


Naomba udokezee japo kiduchu utofauti wa Elimu yetu na yao U.S.A.

Lugha:Fikra sahihu huja kwa lugha sahihi...huoni kama lugha yetu adhimu ya Kiswahili mpaka Sasa ni kikwazo kwa watu wengi kutopata Maarifa(Mfano vitabu) mbalimbali ambayo yamehifadhiwa kwa lugha ya kiingereza...?
 
Kweli uko sahihi ulipo mjibu mkuu swali alilokuuliza kuhusu wazungu kama wanatabia kama zetu za kiswahili,mfano kwenye hiyo video hapo madada wanapigana lakini hizo njemba haziamuulii Bali wana tumia simu zao kuchukua tukio
 
Haya sasa zamu yangu mimi..
Braza Nyani Ngabu heshima yako mkuu..
Mm napenda unijibu maswali ya ngu kwa kina sio kwa mkato ndio nitaelewa.
Nyani Ngabu.
Uliifahamu vp JF na ulijiunga lini humu?

Kwanini ulijiita nyani ngabu na lina maana gani hili jina?

Huyo kwenye avatar ni nani maana hadi Fb umemuweka huyo.

Una hisa (Share) yoyote JF?

Mara ya mwisho kuja TZ lini?

Nitaendelea
[HASHTAG]#Mondray2017[/HASHTAG]
 
Ni ubora gani unauona ktk awamu ya tano tofauti na awamu zote zilizo pita za uongozi wa juu wa nchi yetu ya Tanzania?

Awamu ya tano hata miaka miaka miwili haijafikisha bado.

Itakuwa si haki kuilinganisha na awamu zingine za uongozi wa nchi yetu.

So for me the jury is still out.

Walau ikikaribia kufikisha miaka mitano ikiwa madarakani ndo nitaweza kutoa a more balanced verdict.

Ngoja niwape muda kidogo....

Angali bado ni raia halali mwenye uraia wa nchi moja Tz( kama kweli). Unashirikije ktk prosperity ya nchi yako Tz?

Nalipa kodi.

Pia nasaidia watu wengi sana hususan ndugu wa karibu na hata wa mbali.

Ni taasisi ipi ya kiserikali au mfumo gani was kiserikali unaamini unatakiwa reform ya lazima na haraka hapa Tz?

Duh!

Sehemu na nyanja za kiserikali zinazohitaji mabadiliko ni nyingi sana.

Kuna mfumo wa elimu, afya, utoaji haki, uchukuzi, makusanyo ya mapato, na mengineyo mengi tu.

Nchi nzima inahitaji mageuzi.

Ila kama ni kuchagua moja basi naweza kusema ni mfumo wa utoaji haki.

Watu wenye kipato cha chini hususan kwenye mahakama za mwanzo huko huwa wanataabika sana.

Nalijua hilo, nimeshuhudia kwa macho yangu jinsi wanavyotaabika. Ningependa kuona mabadiliko ya kweli ili watu wapate haki zao wanazostahili.

Kulazimishwa au kuona kama unalazimika kuinunua haki iliyo yako ni jambo baya sana.

Haki siyo bidhaa. Haki ni haki. Haipaswi kununuliwa.

Ulisema ulisoma secondary, kama ulisoma Tz unaionaje elimu ya public schools kipindi unasoma na kipindi cha sasa?

Siwezi kulinganisha wakati wangu na sasa hivi kwa sababu sasa hivi sisomi tena.

Lakini nachoona sasa hivi ni rahisi zaidi kusoma/ kujifunza kuliko ilivyokuwa enzi nasoma.

Sasa hivi mtu huhitaji hata kwenda maktaba.

Mambo yote yapo kiganjani.

Sasa hivi hakuna kabisa sababu ya mtu kufeli [kama mambo mengine yako sawa].

Ni jambo gani la lazima ambalo ukikutana ungependa umshauri/ kumuomba raisi kuhusu nchi na ujumla wake?

Ningemwomba awe mfano mzuri wa uwazi katika matumizi ya pesa za walipa kodi na kutuambia tunamlipa mshahara kiasi gani.

Pia nitamwomba awashauri wabunge watunge sheria ya uwazi kuhusu malipo ya viongozi wote, sheria itakayolazimisha malipo ya viongozi wa umma yanakuwa ni public information.

Umekuwa big fan wa lugha ya kingereza hasa unakiandika kwa ufasaha.

Hata kuongea naongea kwa ufasaha sana. Juzi nilikuwa naongea na jamaa mmoja kutoka Ireland na nilipomwambia natoka Tanzania akashangaa sana kwa sababu naongea Kiingereza vizuri mno. Kwa hiyo siyo kuandika tu.

Je unahisi ni kusoma kama somo, au lugha ya kusomea na kusomeshwa au kutokana na matumizi ya kila siku ughaibuni?

Ni mchanganyiko wa mambo mengi.

Nikiwa mdogo kabisa, yaani nilipoanza kuongea, nyumbani wazazi walikuwa wananiongelesha kwa lugha mbili. Kiingereza na Kisukuma.

Walitaka nizijue hizo lugha tokea utotoni kabisa ili kurahisisha kuzimudu huku ukubwani. Na matokeo yake ndo hayo sasa. Najua Kiswahili, Kiingereza, na Kisukuma.

Unawezaje kuzungumzia brain drainage inayofanyika ktk nchi yetu kupitia shule binafsi hasa za kimataifa. Ambazo haziwaandai next generation kufit ktk mazingira ya Tz bali yale ya ughaibuni?

Brain drainage ndo nini? Sijawahi kabisa kuisikia hiyo. Hivyo kabla sijajibu naomba nifahamishe ni kitu gani ili hata nikijibu nijue ulichoniuliza ni nini.

Natanguliza shukrani

Ahlan wa sahlan.
 
Back
Top Bottom