Hahahaa sawasawa.
Mimi ni homebody. Napenda sana kukaa nyumbani. Nikitoka labda naenda gym kupasha misuli halafu narudi zangu nyumbani.
Napendelea zaidi kunywa lemonade.
Kwenye vile vinywaji vya watu wazima napendelea Heineken na viroba vile vya Konyagi.
Sivuti kabisa. Si bangi, si sigara, si crack cocaine.
Mambo ya klabu nilishaachana nayo zamani sana. Hata baa siendagi. Napendelea zaidi kunywa nyumbani. Na hata nikinywa si kunywa ile ya kilevi mbwa.
Nalala muda wowote tu ule. Hata mchana huwa nalala. Siku zingine nalala asubuhi. Ndo raha ya kuishi kwako hiyo. Kwa mama na baba huwezi kulala na kuamka muda wowote utakao wewe. Ukipitiliza wanakuja kukugongea uamke😀.
Ndo maana napenda kuishi kwangu.
Taste yangu ya muziki ni eclectic. Napenda muziki wa aina nyingi ili mradi masikioni mwangu uwe unasikika vizuri.
Napenda nyimbo za Marvin Gaye, Mariah Carey, Jokha Kassim, Mariam Khamis, Ali Kiba, Future, Gucci Mane, Justin Bieber, Shania Twain, Remmy Ongala, na kadhalika.
Napenda kuwa na watu wa aina zote. Wabongo, Waghana, Wanaija, Wajamaica, Wazungu, Wahindi, Waarabu, Wakorea, Walatino...sina kabisa ubaguzi.
Ili mradi mtu awe poa tu [na msafi...sipendi harufu za vikwapa]...sina tatizo naye kabisa.
Hapana kwa kweli.
Nina muda sana sijahudhuria shughuli za Watanzania.
Ninaotembeleana nao ni wachache sana. Hawazidi wawili.
Najua kupika vyakula vingi. Kwa mfano leo nimepika rice noodles zenye binzari. Ngoja baadaye ntaweka picha uone.
Huwa napika wali, maharage ya nazi, makande, mbuzi choma, kuku choma, maini rosti, mchicha, biryani la kuku, mayai ya kukaanga kama jicho la ng'ombe, omelette, maandazi, vitumbua, na vinginevyo.
Ugali siupendi [ajabu kwa sababu mimi ni ngosha] na kwa sababu siupendi hata kujifunza sijataka.
Uji nilikuwa najua lakini sijaupika siku nyingi sana hadi nadhani nitakuwa nishasahau.