Nyaraka inayothibitisha kwa Mangi Marealle alimuunga mkono Julius Nyerere UN hii hapa. Uongo kwamba Marealle alipinga uhuru ni kwa maslahi ya nani?

Nyaraka inayothibitisha kwa Mangi Marealle alimuunga mkono Julius Nyerere UN hii hapa. Uongo kwamba Marealle alipinga uhuru ni kwa maslahi ya nani?

..Marealle alisema elimu isambazwe kwa Watanganyika wote. Hakuzungumzia elimu kwa watoto wa Machifu.

..Mangi mkuu hakuomba uhuru hivyo hakuna haja ya ku-imagine yeye kukabidhiwa nchi ya Tanganyika.

..Ushahidi unaonyesha kwamba Marealle aliunga mkono uhuru kwa Watanganyika wote.

..Na hapo nyaraka zinaonyesha anaisema vizuri Tanu kuliko Utp. Kwa hiyo habari kwamba alipinga uhuru, au Tanu, ni habari za uongo na zenye nia mbaya na nchi yetu.

..Kwa taarifa yako Lake Province walikuwa wako vizuri sana kifedha. Kwa msingi huo walikuwa na uwezo wa kujiendesha. Kuna kipindi michango ya Lake Province ilikuwa ndio inakibeba chama cha Tanu.
Maadam nyaraka zipo na waandishi tupo, lets correct the history iliyopotoshwa and make it right kwa vizazi vijavyo, na kwa vile kuandika kitu cha kusomeka ni kipaji, tumuombe Mkuu Maalim Mohamed Said atusaidie kama alivyofanya kwa Baba na Babu zake!.
P
 
..Marealle alisema elimu isambazwe kwa Watanganyika wote. Hakuzungumzia elimu kwa watoto wa Machifu.
Hizo zote ni hoja za kujengwa ili kuonyesha Marealle alikuwa na jambo. Ukisoma nyaraka kwa umakini hakuna mahali amesema elimu kwa watoto wa machifu.
..Mangi mkuu hakuomba uhuru hivyo hakuna haja ya ku-imagine yeye kukabidhiwa nchi ya Tanganyika.
Wamesoma na wanajua ukweli huu, waliopotoshwa wanajua ukweli huu, hata hivyo ni ngumu sana kuondoa grudge au grievances , hata yule bwana alienda na chuki katika msingi huo huo, huenda hakujua ukweli
..Ushahidi unaonyesha kwamba Marealle aliunga mkono uhuru kwa Watanganyika wote.
Watu wapo katika denial, itachukua muda kuelewa lakini kama watakuwa tayari kuelewa, wakigoma hakuna namna. Ushahidi upo hapo
..Na hapo nyaraka zinaonyesha anaisema vizuri Tanu kuliko Utp. Kwa hiyo habari kwamba alipinga uhuru, au Tanu, ni habari za uongo na zenye nia mbaya na nchi yetu.
Ushahidi upo katika maandiko ya UN
..Kwa taarifa yako Lake Province walikuwa wako vizuri sana kifedha. Kwa msingi huo walikuwa na uwezo wa kujiendesha. Kuna kipindi michango ya Lake Province ilikuwa ndio inakibeba chama cha Tanu.
Kuna Familia kubwa kama ya Bomani, lakini lazima shutuma zielekwezwe north.
 
..mwalimu wetu wa somo la siasa wakati tuko a-level alitufundisha kwa mangi thomas marealle alipinga uhuru wa Tanganyika, badala yake akadai uhuru wa "nchi ya wachagga."

..kwa kuwa niliwahi kusoma hotuba ya mwalimu nyerere uno aki-pettion uhuru wa Tanganyika, nilikuwa na shauku ya kusoma hotuba ya mangi marealle akidai uhuru wa kabila lake.

..shauku hiyo ya miaka mingi ndiyo iliyoniunganisha na archives za UN ambazo zina nyaraka nyingi za kihistoria kuhusu taasisi hiyo.
Pole Mkuu. Kama mwalimu wako alikuwa ni yule Mzee wetu humu jf basi ulilishwa matango pori ya kutosha in favor of his people (ummah)!
 
Maadam nyaraka zipo na waandishi tupo, lets correct the history iliyopotoshwa and make it right kwa vizazi vijavyo, na kwa vile kuandika kitu cha kusomeka ni kipaji, tumuombe Mkuu Maalim Mohamed Said atusaidie kama alivyofanya kwa Baba na Babu zake!.
P
Na hii ndiyo point kubwa. Si suala la kuandika tu, sote tutumie ushahidi kukanusha uongo dhidi ya Marealle.
Hili ni moja ya mambo yanayochangia chuki, hata yule bwana kaenda na funda lake dhidi ya watu wa kanda ile pengine kwa upotoshaji au kutojua tu!

Kwa sehemu fulani kuna hoja dhidi ya hoja nyingine.
Wale wanaosema Nyerere aliacha historia ya Wazee wao kwa udini, watasema nini kwa hili la Marealle?
Hakuna mahali Nyerere alisahihisha upotofu dhidi ya Marealle hata pale ulipofundishwa shuleni, tunajua Marealle alikuwa Mkristo...
 
Pole Mkuu. Kama mwalimu wako alikuwa ni yule Mzee wetu humu jf basi ulilishwa matango pori ya kutosha in favor of his people (ummah)!

..mwalimu wetu wa siasa alitufundisha kwamba mangi marealle alipinga uhuru wa Tgk, badala yake aliomba uhuru wa "kilimanjaro." mimi niliamuamini mwalimu wetu.

..Na kwasababu ya udogo hata sikujua kwamba miaka ya 1950, wakati uhuru unapiganiwa, mkoa wa kilimanjaro ulikuwa haujaundwa.
 
Yule aliye sema katika vya kuogopa hapa duniani ni Mungu na teknolojia alikua sahihi.

Ipo siku hakuna uongo ambao hautasahihishwa kuwa ukweli, asante mleta mada kwa kuleta ushahidi wa masahihisho ya uwongo tulio fundishwa dhidi ya chief wa wachaga.

Pamoja na mazuri mengi ya mwalimu Nyerere kuna vitu vingi haswa harakati za utafutaji wa uhuru alificha au alidanganya lakini taratibu teknolojia itatupa masahihisho.
 
Sijui kama unajua, hizo nafasi za masomo ng'ambo sio kwa ajili ya Watanganyika wowote bali watoto wa machifu. Nimebahatika kusoma primary na Mjukuu wa Mangi Mkuu, mwenzetu toka sekondari kaenda London!. Nilipokwenda London, akanikaribisha kwake, kumbe Mangi Mkuu wana a big family house in London!.

Tuweke siasa pembeni, ni jimbo gani in Tanzania lilikuwa tayari kujitawala kwa kujitegemea zaidi ya Northern Province?.
Can you imagine kama uhuru ungetolewa kwa Mangi Mkuu badala ya kwa Nyerere saa hizi Tanzania tungekuwa wapi?.
P
Mayalla hili swali lako umelileta kiuoga, naona ni kama vile nawe kwa namna fulani unaungana na wale walioficha huu ukweli kwa sababu mimi nazoona za kiuoga tu.

Hivi kuna kosa gani mtu anapokuwa mbele kufikiria kabla ya wengine mpaka aonekane adui?

Pale mtu anapokuwa na wazo lake, kisha akaanza kulifanyia kazi kwa capacity yake kwangu sioni tatizo, tena nikwambie tu, badala ya kuwaona wale jamaa kama maadui...

Kama vile vichwa vyao vingetumika kuliongoza hili taifa naamini leo tungekuwa mbali zaidi, uoga wetu ndio umaskini wetu, tatizo letu wenye vision tunawatenga, wajinga tunawakumbatia.

Hapa ndipo nimekumbuka huwa kuna maneno kwamba kuna makabila mawili Tanzania Nyerere alisema hayafai kuongoza hili taifa, sijui kama hii kauli kweli aliitoa Nyerere, lakini kama ni kweli aliitoa, basi alikosea sana.
 
Mkuu denooJ, huu pia ni uongo, hakuna popote Nyerere aliwahi kutamka maneno hayo, ila kwenye kufuta ukabila Tanzania, Nyerere sio tuu alifuta uchifu, bali alijitahidi kuondoa nepotism, kati ya makabila yote 120 ya Tanzania, kuna makabila mawili yanaongoza kwa akili, yaani IQ, intelligence, brightness na developmental drive, tungewatumia hawa watu, tungekuwa mbali sana kimaendeleo, ila pia wana matatizo ya nepotism, ukabila na ubaguzi, dharau na kujisikia sana wao pekee ndio the best, hivyo showee nyingi, vingereza vingi na kiukweli ndio wanaongoza kuvuta mandinga makali!. Mifano ya nepotisim yao ipo maeneo walipokuwa wakuu wa taasisi, walijaza watu wa kabila yao!. Hivyo ikitokea moja ya makabila hayo akawa rais wa JMT, sijui itakuwaje maana...

Hata enzi za Blaza, kuliibuliwa tuhuma za ukabila, kwanza nilimtetea Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi! kisha nikalishauri Bunge letu lichunguze Wito kwa Bunge letu tukufu: Mkithibisha hii Nepotism ya ajabu na zile Boeing ni TT, then hatufai!. tatizo enzi hizo Bunge letu lilikuwa ni bunge hili Bunge butu linaloingiliwa na kunyamaza, linapojikomba na kujipendekeza kwa Rais, linaweza kweli kuisimamia Serikali?! badala ya Bunge kuchunguza, mtoa hoja ndio aliitwa kuhojiwa!.

Hapa unaji contradict. Nyerere alifuta uchifu na ukabila ni kweli. Umesema yapo makabila mawili yanaongoza kwa IQ, hili si kweli. Hakuna tafiti yoyote iliyobaini kuwa Wahaya au Wachaga (target yako) wana IQ kubwa.

Pili, mfumo wa elimu ya kikoloni ulioambatana na ujio wa dini uliyaendeleza makabila hayo.
Mfano ni wa akina Marealle au Kadinali Rugambwa ambaye alikuwa kadinali wakati tunapata Uhuru.

Nyerere akichukua nchi kulikuwa na graduate wasiozidi 50, hivyo aliwatumia waliopatikana na kuendeleza walioweza kuendelezwa hata kama ni wa aina moja.

Mfano wakati huo akina Eliufoo , Elinawinga n.k. walikuwa mawaziri , sasa utashangaa ni hao hao waliovunja mfumo wa elimu ya mitihani ya Taifa na kugawa nafasi kwa mikoa to disadvantage ya Kagera/K'njaro

Nyerere hakuacha maeneo mengine, aliwatumia waliokuwa na elimu kuyanedeleza ndiyo maana shule za misheni zikataifishwa nyingi zikiwa Kagera na K'manjaro na watu wa maeneo mengine wakaenda kusoma

Maana ni moja, kwamba, Nyerere hakuwa na choice alilazimika kuchukua walioweza kumsaidia

Yule bw aliyekwenda hakuwa na tatizo la wasomi, alikuwa na chuki akiisema wazi wasubiri.
Yeye hakuwa na nepotism bali pia discriminations ya kutisha. Funda la chuki ambalo wafuasi wamebaki nalo

Tutazunguka mbuyu, hatutaweza kuzunguka ukweli. JokaKuu kavuta Nyaraka ya UN, tumpinge kwa nyaraka nyingine.
 
Mkuu denooJ, huu pia ni uongo, hakuna popote Nyerere aliwahi kutamka maneno hayo, ila kwenye kufuta ukabila Tanzania, Nyerere sio tuu alifuta uchifu, bali alijitahidi kuondoa nepotism, kati ya makabila yote 120 ya Tanzania, kuna makabila mawili yanaongoza kwa akili, yaani IQ, intelligence, brightness na developmental drive, tungewatumia hawa watu, tungekuwa mbali sana kimaendeleo, ila pia wana matatizo ya nepotism, ukabila na ubaguzi, dharau na kujisikia sana wao pekee ndio the best, hivyo showee nyingi, vingereza vingi na kiukweli ndio wanaongoza kuvuta mandinga makali!. Mifano ya nepotisim yao ipo maeneo walipokuwa wakuu wa taasisi, walijaza watu wa kabila yao!. Hivyo ikitokea moja ya makabila hayo akawa rais wa JMT, sijui itakuwaje maana...

Hata enzi za Blaza, kuliibuliwa tuhuma za ukabila, kwanza nilimtetea Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi! kisha nikalishauri Bunge letu lichunguze Wito kwa Bunge letu tukufu: Mkithibisha hii Nepotism ya ajabu na zile Boeing ni TT, then hatufai!. tatizo enzi hizo Bunge letu lilikuwa ni bunge hili Bunge butu linaloingiliwa na kunyamaza, linapojikomba na kujipendekeza kwa Rais, linaweza kweli kuisimamia Serikali?! badala ya Bunge kuchunguza, mtoa hoja ndio aliitwa kuhojiwa!.
P
Mayalla nimekusoma.

Lakini nakuona unachokizungumza kuhusu Nepotism kama kweli kipo, basi kipo kwa upana zaidi; ndio maana licha ya kuyalaumu hayo makabila mawili, lakini bado imeonekana hata kwa Magufuli alipokuwa Rais nae alionekana kupendelea kwao.

Hii maana yake nini? maana yake ni kwamba kama tukianza kujitazama nani aliyemtakatifu kati yetu ndie atuongoze, basi mtu huyo hayupo, hivyo tusiendelee kupoteza muda hapo.

Ila nimependa zaidi ulipokiri hayo makabila mawili wana IQ kubwa, kama kweli wanayo basi kwangu hiyo ndiyo tunahitaji ili kuongoza hili taifa, sio kutafuta IQ ndogo eti kwasababu tu haina Nepotism, ndio maana tunadumaa kama taifa.
 
Hii maana yake nini? maana yake ni kwamba kama tukianza kujitazama nani aliyemtakatifu kati yetu ndie atuongoze, basi mtu huyo hayupo.

Ila nimependa zaidi ulipokiri hayo makabila mawili wana IQ kubwa, kama kweli wanayo basi kwangu hiyo ndiyo tunahitaji ili kuongoza hili taifa, sio kutafuta IQ ndogo eti kwasababu tu haina Nepotism, ndio maana tunadumaa kama taifa.
Una akili sana( una IQ kubwa sana(
[emoji108][emoji108][emoji109][emoji2935][emoji1666]
 
Hapa unaji contradict.
Where is the contradiction?
Nyerere alifuta uchifu na ukabila ni kweli. Umesema yapo makabila mawili yanaongoza kwa IQ, hili si kweli. Hakuna tafiti yoyote iliyobaini kuwa Wahaya au Wachaga (target yako) wana IQ kubwa.
Kumbe unasubiri matokeo ya tafiti?. Tungeweka dodoso la dini na makabila na kuangalia literacy levels amongs different tribes, you would be surprised!.
Hata mimi mwanzo niidhani Moshi na Bukoba ni shauri ya mission na zao la kahawa, mimi nimezaliwa mjini na kuna tuliozaliwa nao mijini na kukulia mijini lakini madarasani jamaa hawa wametukimbiza sana hadi vyuo vikuu!. Ikifanywa sensa ya makabila ya ma prof, lectures, na Ph.D holders, you will be surprised!.
Pili, mfumo wa elimu ya kikoloni ulioambatana na ujio wa dini uliyaendeleza makabila hayo.
Mfano ni wa akina Marealle au Kadinali Rugambwa ambaye alikuwa kadinali wakati tunapata Uhuru.
Mwanzo na mimi nilidhani hivyo, its not!. Tukubali tukatae hawa jamaa ni vichwa na niliwahi kuuliza humu Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?
Yule bw aliyekwenda hakuwa na tatizo la wasomi, alikuwa na chuki akiisema wazi wasubiri.
Yeye hakuwa na nepotism bali pia discriminations ya kutisha. Funda la chuki ambalo wafuasi wamebaki nalo

Tutazunguka mbuyu, hatutaweza kuzunguka ukweli. JokaKuu kavuta Nyaraka ya UN, tumpinge kwa nyaraka nyingine.
Duh...!.
P
 
Mayalla nimekusoma.

Ila nimependa zaidi ulipokiri hayo makabila mawili wana IQ kubwa, kama kweli wanayo basi kwangu hiyo ndiyo tunahitaji ili kuongoza hili taifa, sio kutafuta IQ ndogo eti kwasababu tu haina Nepotism, ndio maana tunadumaa kama taifa.
Kiukweli ili Tanzania ili tuendelee tunahitaji kuwatumia hawa akili kubwa kutuongoza, tunakwama sana kwasababu ya kuwatumia na kuwategemea vilaza na akili ndogo!.
Si mmeona tulivyo leap kwasababu naniliu alikuwa ni akili kubwa!, hivyo kwa vile sasa nanii sio akili kubwa, ili tupae, lazima akubali kuwatumia akili kubwa!.
P
 
At the invitation of the President, Mr. Fletcher-Cooke, special representative of the Administering
Authority for the Trust Territory of Tanganyika, Marealle II, Paramount Chief of the Chaggas, and Mr. Julius K. Nyerere, President of the Tanganyika African National Union, took places at the Council table.

HEARING OF PETITIONERS (concluded)

1. Mr. RIFAI (Syria) asked Mr. Nyerere whether
he had referred to the United Tanganyika Party
(DTP) as a pro-Government party simply because it
supported the Government and its policies or because
he thought that the Government financed the Party
or encouraged the inhabitants to join it.
2. Mr. NYERERE (Tanganyika African National Union) replied that although the UTP did not receive
financial help from the Government it had originally ?een formed by members of the Legislative Council, It supported the Government's policy of multiracialism
and it was opposed to the principles for which the
Tanganyika African National Union (TANU) stood.
Furthermore, the attitude of the Government had given
many Tanganyikans the impression that it favoured
the UTP more than it did TANU. He himself had
heard of many cases in which district officers had held
meetings for the purpose of attacking T ANU and
recommending Tanganyikans to join the UTP. More-over, chiefs could join the UTP without being harassed
by government officials, whereas chiefs who join or favoured T ANU were afraid to make their sym-pathies known.

11. Mr. RIFAI (Syria) asked Chief Marealle II if
there were members of both parties in the area under
his control and if so what was the proportion of membership in each.
12. Chief MAREALLE II replied that T ANU had
members in his area but that he did not know of any UTP members there.

13. Mr. KIANG (China) asked Chief Marealle II
what had been his reaction to Mr. Nyerere's suggestion
that African representation in the Legislative Council should be increased to 5O per cent.
14. Chief MAREALLE II replied that he did not
think it would be asking too much to suggest that
Africans should occupy half the seats as soon as the
necessary administrative arrangements could be made

21. Mr. LALL (India) asked Chief Marealle II
whether he and his fellow chiefs had had meetings
with representatives of any other parties besides the UTP and whether they had felt that any of those parties
more nearly represented the aspirations of the Tanga-nyikan people.
22. Chief MAREALLE II replied that he did not
know whether other parties had had similar meetings
with chiefs elsewhere in Tanganyika. The meeting to
which he had referred had given him and his advisers
the impression that while the UTP was inspired by
high ideals it did not truly represent African aspirations
and even seemed to fear majority rule, which would
in effect be democratic rule. It was the hope of the Chagga people that Tanganyika would eventually have
a government in which Africans would be in the majo· , rity, an aspiration which the UTP representatives had not seemed to share.

23. Mr. LALL (India) asked whether in the event
of a distinct Tanganyikan citizenship being established
Tanganyikan Africans would be willing to give equal
rights of citizenship to Asians and Europeans residing
in the country. If so, it was surely conceivable that
the question of rule by a particular racial group would
disappear.
24. Chief MAREALLE II said that in that event it
would be immaterial to what race the leaders of the
country belonged and the principle of rule by majority
would be followed. It was not yet possible to disregard
entirely the question of the racial composition o~ Tan· ganyika society but it was to be hoped that wtth the
passage of time the members of all communities woul.d
shed their prejudices and cease to be conscious of thetr
racial differences.

25. Mr. NYERERE (Tanganyika African National
Union) agreed that if Tanganyikan citizenship were
eventually established with equal rights for all citizens
the racial origin of the country's leaders would be of
no importance.

Marealle II, Paramount Chief of the Chagga's, and Mr. Julius K. Nyerere, President of the Tanganyika
African National Union, withdrew.

cc Mohamed Said, Pascal Mayalla, Nguruvi3, johnthebaptist, MALCOM LUMUMBA, Mzee Mwanakijiji
Lete video clip.
Hayo mahojiano hata mimi naweza kuyatengeneza.
 
Binafsi naamini historia baada ya uhuru haikutenda haki. Ilichagua nani imuandike vizurina na nani imuandike vibaya na nani isimuandike kabisa. Kuna nimejaribu kuelezea hata namna upotoshaji wa kihistoria aluofanyiwa Chifu Mangungo kuonejana kana Chifu mjingawakati ukweli ni kwamba naye aliwapokea Wszungu kama wawekezaji katika eneo lake kwa mtazamo wake kwa wakati ule hivyo hakuna haja ya kumlebo kana mjibga ilihali sisi leo tunafanya kile kile cha kuwapojea wazungu kama wawekezaji
 
Mkuu vijana wanajiapiza kwasababu hii dhana imeachwa bila kusahihishwa kwa muda mrefu

Nyerere 'inner circle' walijua ni hoja nzuri sana inayopunguza nguvu za Uchifu na hata historia
Ukichanganya na ukweli kuwa Chief Marealle alikuwa na uwezo wa elimu na fedha na ile 'aggressiveness' ya watu wa kaskazini katika education and business ni rahisi kabisa mtu kuamini Marealle alitaka kuanzisha republic yake na hivyo alipinga uhuru kinyume kabisa na ukweli.

''Dhambi' kubwa katika hili ni wasomi kukalia kimya ukweli. Pili, Mwl naye anasehemu yake, kwa kutoandika 'Memoir' tunakosa ukweli kutoka kwa wahusika

Joka, hivi tungekuwa na 'presidential Library' nyaraka hizi si zingepatikana !!
Hili la Presidential Libraly ni muhimu sana, maana kwa sasa hatujui kama nyaraka muhimu bado zipo na ziko wapi, mfano HOJA ya nyaraka ya Muungano bado iko palepale, Iko wapi? na Je ni kweli ipo?
Nakumbuka wakati wa Bunge la katiba Lissu alipoleta hoja hiyo JK alikuja na COMPUTER printed document!
Ambayo siamini kama ilikuwa ndiyo!!!
 
Mayalla nimekusoma.

Lakini nakuona unachokizungumza kuhusu Nepotism kama kweli kipo, basi kipo kwa upana zaidi; ndio maana licha ya kuyalaumu hayo makabila mawili, lakini bado imeonekana hata kwa Magufuli alipokuwa Rais nae alionekana kupendelea kwao.

Hii maana yake nini? maana yake ni kwamba kama tukianza kujitazama nani aliyemtakatifu kati yetu ndie atuongoze, basi mtu huyo hayupo, hivyo tusiendelee kupoteza muda hapo.

Ila nimependa zaidi ulipokiri hayo makabila mawili wana IQ kubwa, kama kweli wanayo basi kwangu hiyo ndiyo tunahitaji ili kuongoza hili taifa, sio kutafuta IQ ndogo eti kwasababu tu haina Nepotism, ndio maana tunadumaa kama taifa.

..jamani mtaniharibia hoja yangu kwa kuingiza mambo ya IQ.

..nawaomba mjadili hoja ambazo unaweza kuzitetea kwa ushahidi; ama wa nyaraka, au matokeo ya utafiti.

..naamini Pasco anataka kuchafua hoja na mjadala wetu kwa kuchomekea mambo ambayo yamekuwa chanzo cha CHUKI kubwa ktk taifa letu.

..hili la kudai Mangi Marealle alipinga uhuru wa Tanganyika ni hoja imetumika kwa muda mrefu sana kujenga chuki.

..Hoja nyingine ni hizo anazochomekea Pasco naomba wachangiaji mzipuuze.
 
Hoja ikiwa mtambuka wacha ijadiliwe kwa mapana yake, lakini kuwazuia wengine kama unavyofanya ni sawa na kuwafinya watu kifikra.

Kwangu kama yupo mwenye hayo makaratasi unayotaka muache aje nayo, lakini hata mwenye channel nyingine inayotokana na chimbuko la hoja yako naye usimpuuze, muache ailete, hapo ndio mjadala hunoga.

Lakini kulazimisha kila mmoja aje na makaratasi hapa, simply naona umefukuza wachangiaji kwenye hoja yako, hata mahakamani huwa wanatumia "authority" na "logic" pia.
 
Mkuu JokaKuu kwanza hongera kwa bandiko zuri .

Nionanvyo mimi historia ya Tanganyika & Zanzibar ifundishwayo mashuleni imechujwa sana na chama chakavu lengo kuu likiwa ni watu waendelee tu kuwa wakusifia na kuonekana hakuna mahali serikali ilichemka hili liko wazi ndio maana yule jamaa alipata nguvu tena ya kusema vitabu vya somo la historia vichapwe bila review hata ya mtaala akawa yuko mbioni kuleta somo jipya.

Niko Interested kujua ukweli juu ya mapinduzi ya Zanzibar na maisha ya John Okello baada ya mapinduzi.
 
Back
Top Bottom