Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona watu wengi tu huenda kufunguwa kesi za jinai polisi? kama hana ushahidi wa kutosha hata huy dpp atamshitaki nani? wewe umeona kuna ushahidi hapo wa kumshitaki mtu ukashinda?
Besides, nakubaliana na wewe kuwa kesi za EPA si za jinai kama wengi wanavyotaka ziwe. EPA ni madeni na kesi zake ni za madai na si za jinai. Ukilielewa hilo hapo ndio utajuwa kuwa Kikwete alipowataka waliochukuwa hizo pesa wazirudishe wenyewe, alifanya jambo la maana sana. Kwani ni wazi kabisa hizo ni kesi za madai na ukizifanyia papara kuzipeleka mahakamani unaweza kujikuta kuwa kesi inakuwa dragged kwa muda mrefu sana kiasi kuwa inakutia hasara zaidi na mwisho wake fedha usizipate na kesi ukashindwa.
Haya ya Kumtafuta RA na YM ni majungu tu, hakuna kesi hapo ni wajanja wachache wanajitafutia umaarufu. Na wajinga wengi wanaamini hapo kuna kesi. Nashangaa sana.
Mbona tuliambiwa na seriokali kagoda ni ya jeshi haiguswi, kumbe ni uwongo, my GOD.
Faiza kesi huwa hazifunguliwi polisi. Kesi zinafunguliwa mahakamani. Unapoenda polisi unaenda kuripoti au kulalamikia tukio ili polisi wafanye uchunguzi na kuchukua hatua zaidi. Wakishamaliza uchunguzi wao na kuona kuna ushahidi wa kumfungulia mtuhumiwa kesi mahakamani then wanapeleka faili kwa DPP ili afanye hivyo. Ukienda polisi kuripoti issue za madai sijui kama watakusaidia.
Umesema kuwa EPA ni madeni na kesi zake ni za madai na si za jinai. Sasa vipi mtu akigundulika kuwa alitumia jina au kampuni bandia kupata hela za EPA, utamfungulia kesi ya mada au ya jinai? Hata kama ingelikuwa tuhuma na kesi za EPA ni za madai, Msemakweli ataenda kushtaki kama nani? Anamdai nani?
Kuhusu swali lako kama naona kuna ushahidi wa kumshitaki mtu na kushinda, mie bado sijafika huko. Besides tumeambiwa kuna ushahidi zaidi ya uliowekwa hapa, so ni vigumu kutoa a definitive answer.
Huo wote ni ushahidi "circumstantial" na sio "solid" na ndio maana si Msemakweli wala Msemauongo wanaoweza kushitaki wao wenyewe na wanaupeleka kwa DPP, kwani wanajuwa kwa ushahidi kama huo, wakishindwa kesi! wanafilisiwa. Kwani hao watu unao "wapeleka" mahakamani dau lao ni kubwa.
Naona unashindwa kabisa kunielewa. Kesi nyingi sana zinafunguliwa polisi na wao wanzipeleka mbele kusikilizwa, mfano mtu akikuibia na ushahidi wote unao, unaenda mahakamani moja kwa moja? si unaenda kumshitaki kituo chapolisi na hata taarifa za wizi huwa zinapelekwa polisi. Tafadhali sana kwa hilo usitake tubishane. Nakushangaa sana.
Hayo ya msemakweli ndio hayo hayo nnayosema mimi, hana cha kushitaki wala hajui cha kushitaki wala hana ushahidi wa kushitaki na ndio maana kapeleka huo anaouita "ushahidi" kwa DPP na halafu aka leak huo "ushahidi" wake ili aonekane kafanya kitu. Soma posts zangu za mwanzo utanielewa.
Naona unashindwa kabisa kunielewa. Kesi nyingi sana zinafunguliwa polisi na wao wanzipeleka mbele kusikilizwa, mfano mtu akikuibia na ushahidi wote unao, unaenda mahakamani moja kwa moja? si unaenda kumshitaki kituo chapolisi na hata taarifa za wizi huwa zinapelekwa polisi. Tafadhali sana kwa hilo usitake tubishane. Nakushangaa sana.
Hayo ya msemakweli ndio hayo hayo nnayosema mimi, hana cha kushitaki wala hajui cha kushitaki wala hana ushahidi wa kushitaki na ndio maana kapeleka huo anaouita "ushahidi" kwa DPP na halafu aka leak huo "ushahidi" wake ili aonekane kafanya kitu. Soma posts zangu za mwanzo utanielewa.
Naomba Msemakweli apewe Ulinzi wasije wakamkolimba
Mbona unateseka sana kumuelekeza mtu ambaye hujionea fahari kubisha hata vitu asivyo vijua? Hata hivyo nakusifu kwa uvumilivu na busara zako.Faisa nimekuelewa vizuri kabisa. Mantiki yako ni kwamba kesi huwa zinafunguliwa polisi. Mantiki yangu ni kuwa kesi huwa zinafunguliwa mahakamani. Polisi wanachunguza tukio wakiridhika na ushahidi wanapeleka faili kwa DPP ili atumie mamlakaka yake ya kufungua kesi. Hakuna mahakama kwenye vituo vya polisi. Nafikiri tatizo hapa lipo kwenye matumizi ya neno "kesi". Zamani wakati tukiwa na wanasheria wachache, DPP ali delegate mamlaka fulani kwa polisi kuendesha kesi mahakani. Sidhani kama bado ndivyo ilivyo.
Kuhusu mtu akikuibia na ushahidi wote unao, unaenda mahakamani moja kwa moja? Simply, huwezi kwenda mahakamani mwenyewe kwa sababu wewe sio Jamhuri. Katika makosa ya jinai Jamhuri ndio yenye mamlaka ya kumshitaki mtuhumiwa. Wewe utakuwa shahidi tuu. Unapoenda kulalamika polisi, wao wanachunguza kama tuhuma zako ni za kweli. Wakikuta ni za kweli wanapeleka malalamiko yako kwa DPP ili Jamhuri ifungue kezi dhidi ya mtuhumiwa.