FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Ili kuongezea msisitizo ... mwaka 1999 au 2000, kuna msichana (mwanafunzi wa UD) alibakwa na kesi ilipelekwa mahakama ya Kisutu. Kesi ile ili-draw attention ya watu kwa kuwa mbakaji alikuwa mfanyabiashara. Then kuna mambo yaliendelea nyuma ya pazia yakiwahusisha (waendesha mashitaka ambao ni polisi, hakimu, mtuhumiwa wa ubakaji na mbakwaji). Kulikuwa na madai kwamba kuna hela ilitembezwa (sina hakika na hilo). Then msichana aliomba kufuta hiyo kesi, na hivyo kesi ikawa imefutwa kinyemela (kimya kimya).
Magazeti yaliyokuwa yakifuatilia kesi hiyo kwa karibu yalipogundua hilo yaliandika juu ya ufutwaji wa kesi hiyo kinyemela. Jaji Mkuu aliposoma habari hizo aliomba jalada la kesi hiyo ili kuona mwenendo wa kesi yote mpaka kufikia uamuzi wa kesi kufutwa. Baada ya kupitia jalada hilo, kauli ya Jaji Mkuu ilikuwa ni kwamba kesi ilifutwa kimakosa. Mbakwaji hana haki ya kuomba kesi ifutwe kwa kuwa ni kesi ya jinai, mbakwaji ni shahidi namba moja. Mshitaki (Jamhuri) ndiye mwenye haki ya kuamua kuendelea au kutoendelea na kesi. So, kesi hiyo ilirudishwa mahakama ya Kisutu ili iendelee kusikilizwa. Kwa bahati mbaya mbakaji alikuja kufariki kwenye ajali na hivyo kesi ikafa.
Kwa hiyo dada yangu Faiza linapokuja swala la kesi za jinai, mwananchi wa kawaida hawezi kushitaki moja kwa moja, yeye anabaki kuwa shahidi tu na si vinginevyo na ndio maana Feleshi (DPP) ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ya kuendelea ama kutoendelea na kesi. Feleshi akisema nafuta kesi, hakuna mtu wa kumuuliza.
Hoja kwamba kesi za EPA ni za madai, pamoja na ukilaza wangu wa sheria, hilo siyo kweli. Auditors ambao walikagua mahesabu ya Account ya EPA walisema kwamba document zilizotumika zilikuwa ni za kughushi kwa kuwa mikataba ya kuuza hayo madeni ilisainiwa kwa kipindi kifupi kana kwamba hizo kampuni (za nje) ambazo zilikuwa zinauza madeni yake zote zilikubaliana kuwa Dar within hicho kipindi kifupi na ndipo walipoona dalili za wizi. So, jinai ya kwanza ni kughushi documents, jinai ya pili ni kujipatia hela kwa kutumia documents ambazo zimeghushiwa. Hapo hakuna kesi ya madai bali ni kesi ya jinai.
Hoja kwamba JK alitaka hela zilipwe kwanza kwa kuwa kesi zinaweza kuchukua muda mrefu sana, hilo ni changa la macho. Ujanja aliotumia Kikwete ilikuwa ni kupoza watanzania kwamba hela tume-recover kwa hiyo hakuna haja ya kupelekana mahakamani. Mtu akiiba ng'ombe wako na ukamshika na ukaweza kuwarudisha hao ng'ombe haimaanishi kwamba yeye siyo mwizi. What if angefanikiwa kuishia nao kimoja, ungeweza kuwapata? Kitendo cha hao akina KAGODA na wengineo kukubali kurejesha hizo hela ilikuwa ni ushahidi wa wazi kwamba wanakiri kuwa waliiba na ndiyo maana wamekubali kurudisha fedha. Kama yangekuwa ni madai ya kawaida, wangeweza kugoma kurudisha hela ikitegemeana na status ya kampuni zao ambazo zilichota hizo hela.
Nadhani umeshindwa kuelewa nadharia.
Kesi hii na ushahidi uliotolewa unamuhusisha vipi wizi RA na YM? hakuna ushahidi kabisa hapo. Inabaki kuwa madai na hakuna criminal case hapo.
Sijui kama unanielewa au na wewe ni katika wale wanaong'ang;ania visivyo kuwepo.
Nakumbuka walipokuwa wanashabikia humu JF Dowans wafutiwe mkataba, nilijaribu sana kupinga hilo na nikasema litigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha. Hakuna aliyenielewa. Matokeo tunayajuwa.
Na kwa hili nakuambieni hakuna "incriminating evidence" kwa RA wala YM. pelekeni mahakamani, mtakuja kuniambia matokeo yake. Hata huyo DPP kwa "ushahidi" uliowekwa hapa haifikishi hata mahakamani labda na yeye awe punguani.
Hata kesi ya Richmond ilipopelekwa mahakamani nikasema watashinda na tumeona kimekuwa nini. Kumbukeni, wengi wenu mko so emotional kwa mapenzi ya chama chenu, hamna uwezo wa kuuona ukweli ikiwa mtakuwa emotional kwa mapenzi yenu ya chama.
Nakwambieni tena hakuna kesi hapo, au hakuna ushahidi wa kumtia hatiani RA wala YM.
Yusuph Manji kuhamisha pesa kupitia bureau ni moja katim ya ushahidi wa kijinga sana niliouona hapa. Hivi Yusuf Manji ana hamisha mamilioni mangapi kila siku kupitia bureau yake kwa biashara zake. Akiitowa list yake hata hakimu atamuona alioleta huo ushahidi ni punguani.
Kuweni na mtazamo bila kuwa washabiki. Watanzania ushabiki wa huku tumefunga macho na masikio unatuponza kwenye mengi sana. Na hii ni kwa ngazi zote si kwa wana JF tuu. hata maamuzi mengine ya maana yanatolewa kiushabiki na si kama ilivyo. Mfano mdogo ni kufuta mkataba wa Dowans, ulikuwa ni ujinga wa hali ya juu. Na wahusika wote walifanya hivyo kufuata ushabiki ama kwa maslahi yao au ya vyeo vvyao.