Sio kila silaha ya Marekani ni superior. Kwenye vita hata kama unapigana na Burundi kuna sehemu anajua au anatoa upinzani. Hiyo smart bomb ni joint direct attack munition (JDAM) ambayo ni kit inaongezwa kwenye dumb bombs au gravity bombs kuzipa accuracy. Hizo JDAM hazijatengenezwa direct kwamba ni smart kama guided missiles au guided rockets.
Kuna njia ya kufanya jamming ya GPS au satellite communication ndio maana makombora huwa satellite guided na yanaongezewa na vitu kama inertia navigation, terrain following, TV guided (hasa Urusi wanapenda hii), n.k.
Kwanza Urusi kwenye vita hii wameonekana wako vizuri kwenye electronic warfare kwa ground based systems.