Nyasi za Juncao: Suluhusho la malisho ya ng'ombe, mbuzi na kondoo

Wakati napanda watu wengi walijua napanda miwa, hadi zinakuwa watu wengi walijua ni miwa.Inawezekana sikuelewi au wewe ndiyo hunielewi.Kama una swali uliza ili nikuelewe.
una uhakika hii ni juncao mkuu.
 

Attachments

  • jaha.jpg
    874.4 KB · Views: 107
kuna hii pumba fulani zinazotoka kwenye mpunga aisee yani gunia moja mpaka 10k huku tulipo wakenya wanapanda bei sijui kuna siri gani na zinapelekwa sana nje hizi pumba kwa ajili ya mifugo.

Nipo interested na huo Mzigo,huko bei zipoje kwa gunia la kg 100? Ni sehemu gani?
 
Sio Viongozi ni swala la mtu mwenyewe kutafuta maarifa Duniani huko,
 
Kando kando ya mito yanaota sana. Pale Dumila nmekatia sana ng'ombe wa mzee hayo majani miaka hiyo.
Siyo hizo.
Kuna aina nyingi za napier na zinafanana mf.bana grass, elephant grass nk.
Juncao pia ni napier lakini tofauti Juncao inatoa machipukizi mengi na malisho mengi katika eneo dogo.
Google: Juncao grass.
 
Hizi unaweza agiza tu hakuna cha Serikali, ukikaaa kusubilia kila kitu Serikali utakaaa sana
Mimi ninazo ninalima mwaka wa pili huu nilitoa Rwanda.Rwanda zipo tangu 2006.Tanzania serikali ilizipata mwaka 2019/2020.
Atakayehitaji mbegu tuwasiliane 0756625286.
 
Mbona mmea huu nimeiona kwenye mashamba ya ng'ombe wa mzee wangu huko Iringa miaka zaidi ya 10 iliyopita! Aliletewa na wazungu miaka hiyo.
 
Mbona mmea huu nimeiona kwenye mashamba ya ng'ombe wa mzee wangu huko Iringa miaka zaidi ya 10 iliyopita! Aliletewa na wazungu miaka hiyo.

Ni sawa inawezekana lakini je mzee wako au wewe uliendeleza kwa kuuza na kusambaza nchini?

Au mliona kama majani ya kawaida tu
Hapo ndio tunapokwama
 
Kwetu kilombero tunayaita magugu maji ,kwasababu yameoteana sana pembezoni mwa mto
 
Kwetu kilombero tunayaita magugu maji ,kwasababu yameoteana sana pembezoni mwa mto
Hapa naona watu wengi wanachanganya,mbegu za Juncao zimeingia nchini 2019/2020 kutokea China,Rwanda ndiyo nchi ya kwanza Afrika kulima Juncao kwao mbegu zimeingia 2006.Huku Afrika China inatoa msaada wa mbegu wao ndiyo wanaosambaza.Watu wengi wanafananisha na elephant grass(mabingobingo)au matete.

Juncao ni aina ya napier,aina nyingine ya napier ni Bana grass, Elephant grass, Pakchong 1 nk.
Tofauti ya Juncao na hizo napier za aina nyingine ni uwezo wa kutoa malisho (majani)mengi.
Juncao inatoa machipukizi mengi,majani mengi na yanakuwa marefu.Hizo aina nyingine ya napier hazina sifa hizo,ingawa zinafanana kwa kiwango kikubwa kwa muonekano.
Mimi ninalima Bana grass,Juncao, Elephant grass na Buffel grass Ila hayo yote hayawezi kufikia ubora wa Juncao kwenye kutoa majani mengi na kiwango cha protini, Juncao yana kiwango kikubwa cha protini kuliko napier zote,yanatoa malisho mengi kuliko napier zote,yanakuwa marefu kuliko napier zote.
Unaweza kwenda Google andika tu Juncao grass utapata elimu kubwa.
 

eka 1 ya Juncao inatosha kulisha ng'ombe wangapi wa nyama zero grazing?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…