Hapa naona watu wengi wanachanganya,mbegu za Juncao zimeingia nchini 2019/2020 kutokea China,Rwanda ndiyo nchi ya kwanza Afrika kulima Juncao kwao mbegu zimeingia 2006.Huku Afrika China inatoa msaada wa mbegu wao ndiyo wanaosambaza.Watu wengi wanafananisha na elephant grass(mabingobingo)au matete.
Juncao ni aina ya napier,aina nyingine ya napier ni Bana grass, Elephant grass, Pakchong 1 nk.
Tofauti ya Juncao na hizo napier za aina nyingine ni uwezo wa kutoa malisho (majani)mengi.
Juncao inatoa machipukizi mengi,majani mengi na yanakuwa marefu.Hizo aina nyingine ya napier hazina sifa hizo,ingawa zinafanana kwa kiwango kikubwa kwa muonekano.
Mimi ninalima Bana grass,Juncao, Elephant grass na Buffel grass Ila hayo yote hayawezi kufikia ubora wa Juncao kwenye kutoa majani mengi na kiwango cha protini, Juncao yana kiwango kikubwa cha protini kuliko napier zote,yanatoa malisho mengi kuliko napier zote,yanakuwa marefu kuliko napier zote.
Unaweza kwenda Google andika tu Juncao grass utapata elimu kubwa.