KERO Nyaya za fiber zimekuwa kero

KERO Nyaya za fiber zimekuwa kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Zinapita pia chini, fiber zinafukiwa ila kuna sehemu inabidi zije juu kwa ajili ya kuunganishia watu majumbani.
Uko sahihi mitandao ya simu walianza hiyo project lakini walichokutana nacho sasa, makazi yetu Kwa ujumla mengi hayajapimwa Kuna ukakasi hapa kwenye upitishaji wa cable, mipango ya serikali nayo sio rafiki bomoa, chimba Jenga ni nyingi, so hakuna kampuni ambayo itakubali cost za maintenance mara Kwa mara
 
Wahusika wa usambazaji wa Fiber kazi yenu nzuri ila imekuwa kero, nguzo zenu zinadondoka sana, nyaya zenu zinalegea mno, hebu fanyeni kitu ziwe sawa, vinginevyo tutaanza zikata ili mje kuweka vizuri upya
Kweli aisee, jamaa wachovu sana, hapa getini kwangu inanisumbua , imeshuka kwa mara ya pili imebidi niikunje ili angalau iwe juu, ikishuka tena sitajali, nitajifanya siioni na kuipamia na gari. Mwisho wa ukuta kuna waya wa fiber wa kampuni nyingine umekatika kabisa uko chini, sijui hizo nyaya ni nyepesi sana au utaalamu wa kufix ndio haupo.

Vv
 
At least wangekuwa wanapangiana eneo fulani wawe labda TTCL na Airtel. Au eneo fulani ni SAVANNA na VODA lakini nadhani haipo hivyo.

Eneo kama la Upanda nyaya zimejazana vibaya sana. Au lah basi wawe wanazipitisha kwa chini, hii inaweza ikawa ni nzuri.
Uchumi wa solo?
Usijali deni la taifa ni himilivu
 
Back
Top Bottom